Tanzania kwa mwendo wa kubebana tutafika?

Andindile

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
304
16
Habari kutoka Monduri zinadai kuwa halimashauli ya wilaya imeidanganya kamati ya bunge kuhusu mapato na matumizi kwa mara ya pili. Uongo mmojawapo ni kuwa halmashauri hiyo ilitumia sh. 30 million kujenga nyumba ya mwalimu wakati ukweli ni kuwa nyumba hiyo ilijengwa na TANAPA. Halmashauri hawakugharimia chochote bali walipewa ffunguo za nyumba. Cha kushangaza ni kuwa watu hao wafujaji wamesamehewa na kamati ya bunge chini ya yule mbunge maarufu wa kufoji vyeti Samweli Chitalilo na kuwaambia hao watendaji waandae report nyingine kwa mara ya tatu. Adhabu waliyopewa ni kukatwa 15% ya mshahara kwa mwezi mmoja tu.

Je kwa mwendo huu wa kubebana tunakomboka kiuchumi?

habari kamili soma mwananchi 9/4/2009 au www.mwananchi.co.tz
 
Mara nyingi wabunge ambao ni mawaziri huwa wainfluence nani awe mkurugenzi wa halmashauri wa wilaya wanayoiwakilisha; huwa wanafanya hivyo ili iwe rahisi kwao kupitisha fedha kupitia kwa halmashauri ambazo wao wanazitumia kwa mamboyao ya kupatia kura [kuhonga]. Inawezekana kabisa hizo sh. 300 millioni ambazo zinasemekana zilitumika kujenga nyumba ya mwalimu huko Monduli, huku nyumba ilijengwa na Tanapa, fedha hizo zikawa zimeishia kwa fisadi Lowassa!! Alivyokuwa waziri mkuu alimhamisha mama mmoja DED kutoka Moshi kwenda Monduli ili kufaniksha ufisadi wake huo!! Haiwezekani fedha nyingi namna hiyo zikapotea katika wilaya yake na yeye akae kimya bila kujua, haiwezekani.
 
Back
Top Bottom