Elections 2010 Tanzania Kuzaliwa Upya Oktoba 31/10/2010

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,238
24,097
b00vhfwt_640_360.jpg

Vuguvugu za Watanganyika kutaka uhuru 1961 zinafanana na vuguvugu la mwaka huu 2010 wa uchaguzi ambapo Watanzania wameonyesha uchu na matumaini ya kufanya mabadiliko makubwa.

Mwaka 1961 Mwl. Nyerere aliongoza vuguvugu la kuwaletea matumaini Watanganyika kupatiwa uhuru wa kisiasa ili wananchi waweze kufaidi matunda ya rasilimali ya nchi yao.
Makabwela wasiokuwa na fedha ndio walikuwa wadau wakubwa kumuunga mkono Mwl. Nyerere kuwa kiongozi wao wa kuleta mabadiliko.

Miaka takriban 50 baadaye chama cha CHADEMA kina kila dalili ya kuwaletea matumaini mapya ya kuamsha vita vya kweli dhini ya maadui ujinga, maradhi na umasikini kwa kupitia Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA,Wabunge wa CHADEMA na Madiwani wa CHADEMA.

CHADEMA kwa kupitia mgombea Dr. Slaa wameweza kuwasilisha ujumbe unaoeleweka kwa Watanzania, kiasi kila mpiga kura anaelewa kuwa '' KURA YAKO YA UCHAGUZI KWA CHADEMA NI ELIMU NA AFYA KUWA BILA MALIPO, pesa zao za kodi kutumiwa vizuri kwa kujenga miundo mbinu bora kuchochea uchumi kukua kumuondoa adui umasikini n.k

Hakika mwaka huu wa uchaguzi Chama kikongwe lazima kigaragazwe kwa kupitia sanduku la kura, ndio inawezekana kuking'oa chama kikongwe kilichochoka cha CCM.

Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.
 
Tulitoka tanu tukaja ccm akuna jipya na tunasubiri ama kubaki ccm ama kurudi chadema(kama mwandishi wa habari hizi alivyoandika) wewe kujiweka sawa kwenye system ikitokea yoyote wasikuaribie maiha yako..kumbuka kuna watu wengi baada ya ucgahuzi hasa wafanyabiashara watafilisika aama kuhama nchi inategemea na upepo..ama kuacha kabisa biashara haya ndio mambo yaliomfanya sadoki akaona abalance isiwe tabu
i salute sadoki..kwa huyu yoyote atakaeingia lazima arudishe hela zake..
 
Back
Top Bottom