Tanzania kuwasilisha ombi UN kuongezewa eneo la bahari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kuwasilisha ombi UN kuongezewa eneo la bahari

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jan 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. (PICHA: OMAR FUNGO)


  Tanzania imetangaza kuwasilisha maombi Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani, kudai umiliki wa eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) katika Bahari Kuu ya Hindi, ili iweze kulifanyia utafiti zaidi kuhusu rasilimali zilizoko chini ya bahari kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi.

  Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, rasilimali hizo ni pamoja na mafuta, gesi na madini.

  Eneo hilo linatokana na ongezeko lingine tena maili 150 na hivyo kufanya jumla ya mpaka hadi maili 350, ambazo ni sawa na kilomita 560 kutoka kwenye ‘baseline’.

  Waziri Tibaijuka alisema maombi hayo yanatarajiwa kupelekwa na jopo la wataalamu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na wajumbe wawili kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, litaongozwa na Waziri Tibaijuka.

  Alisema wanatarajia kuwasilisha andiko la utafiti wa kisayansi la kudai eneo hilo katika Shirika la UN Linaloshughilikia Mikataba Sheria za Baharini (UNCLOS) kesho na kwamba, baadaye Aprili, mwaka huu, watakwenda tena UN kutetea andiko hilo.

  Alisema baada ya kutetea andiko hilo huko UN, Kamisheni ya Masuala ya Baharini itafanya uamuzi kuhusu maombi yao na kwamba, anaamini hatua waliyoifikia watafanikiwa.

  Waziri Tibaijuka alisema kazi ya kukamilisha andiko hilo iliyoanza mwaka 2007 na kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 5.2, imesimamiwa na wizara yake na tafiti zimefanyika kwa kutumia wataalamu kutoka sekta za ardhi, maji, mawasiliano, sayansi na teknolojia, sheria na wataalamu wa masuala ya baharini kutoka vyuo vikuu.  SOURCE: NIPASHE
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  safi.....
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Futa hilo
   
 4. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa inabidi mipango kama hii pia iendane na kuiongezea JWTZ uwezo wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kulinda hilo eneo (wese) maana linazidi kuwa kubwa...:eyebrows:
   
 5. b

  bagamoyo1 Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  madafu 5,2 billion . kuandika mchakato sisi watanzania ni matajiri sana , najuwa tukipewa go ahead inalipa sna a, lakini wataalamu wa kibongo walilipwa hichi kiwango ???
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi kama Zanzibar wakishajitenga huo mpaka itakuwaje? Huo mpaka utaongezwa au?
   
 7. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watanzania kwa michakato hata usa tunawashinda hata tukiongeza ukubwa wa mipaka tutabaki palepale miaka yote tupo na bahari lakini visamaki vinavyoliwa dar mifupa mitupu wakati meli za wafilipino zinakuja kuvua kwenye mipaka yetu samaki wakubwa ambao kila mtanzania alishangaa ukubwa wake.
   
Loading...