Tanzania kuwaandaa watu wake kuajiriwa zaidi kuliko kuajiri

masomo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
208
46
Iwapo fao la kujitoa halitarudishwa serikali itakuwa imeweka mpango wa kuwaandaa watu wake kwa wingi zaidi kuajiriwa zaidi kuliko kuajiri.Wajarisia mali wangi hujipatia mitaji yao ya awali kupitia ajira na baadae kutengeneza ajira,na mitaji hii iwanipata kwa njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na fao la kujitoa pamoja na mikopo.Utaratibu uliokuwepo ulikuwa mzuri sana hasa kwa wafanyakazi wa migodini ambao ajira zao hazidumu,na mifano iliyotolewa ya nchi ya kenya na zanzibari si za msingi kwani nchi hizo hazina migodi kama Tanzania.Hili la kutojitoa halitaongeza maendeleo bali litaongeza ufisadi tu na kudidimiza hali ya maisha ya mtanzania.
 
Kwa wale tunaofanya ajira za mikataba,kwenye mkataba wa hali bora nadhani tukubaliane na mwajiri pesa za NSSF tuwe tunapewa wenyewe.Maana serikali hii imekuwa nyag'anyi.Mtu ujisomeshe(whether through loan board/mzazi pocket),kazi ujitafutie halafu NSSF yako inyang'anywe!Inauma sana.
 
Back
Top Bottom