Tanzania kuwa Taifa masikini nini tatizo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kuwa Taifa masikini nini tatizo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babalao 2, Sep 13, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Hii imekaaje wtz wenzangu
  Kama viongozi wakuu tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanashindwa kujua ni kwa nini nchi yetu inaendelea kuwa maskin katika dunia ya leo na ni kweli hata sisi hatujui au tunajua ila tumeridhika na hali ilivyo?
  Je nini kisababishi cha hayo yote?
  Je ni kweli ya kuwa tatizo ni
  Rais kutokusimama kwenye nafasi yake.
  Wasaidizi wa rais kushindwa kumshauri boss wao vizuri
  Chama kushindwa kutoa watu safi na wazalendo kwa nchi yao.
  Wataalamu wa nyanja mbalimbali kukosa utaalamu wa kutosha.
  Watanzania kwa ujumla tu wavivu wa kufanya kazi kwa bidii na ubora au
  Ni katiba ndiyo imetufikisha hapa na kushindwa kujua ni kwa nini sisi tumebaki masikini wa kutupwa.
  Tusisahau kwamba MUNGU AMETUPA RASILIMALI KARIBU SOTE ZINAZOHITAJIKA. TATIZO NININI JAMANI.
  MAONI TAFADHALI.
   
 2. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  watz weng ni wajnga, wavivu, mfomo mbovu ndo maana wanasiasa hasa ambao wako serekalin wana2fanya kama mifugo!
   
 3. M

  MTK JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa hayati baba wa taifa ili tuendelee na kupata ustawi wa kitaifa tunahitaji mambo yafuatayo:
  1. Raslimali: Watu, Ardhi, madini, maji n.k - hivi vyote tunavyo kwa wingi
  2. Siasa (sera) safi - Zipo japo linazungumzika kama kweli tuna siasa safi!!
  3. Uongozi bora hatuna na hilo halina mjadala; mwenye macho haambiwi tazama! Uongozi uliopo ni dhaifu, umejawa na roho za ubinafsi, ufisadi na kula rushwa na ubabe

  Elimu imeporomoka sasa tumebaki na bora elimu kwa gharama kubwa sana, wakulima hawawezeshwi pembejeo, wanakopwa mazao yao, wafanyakazi hawana maslahi mazuri kwa hiyo tija katika sehemu za kazi na mashambani ni duni, raslimali zote za nchi zimegenishwa, viongozi wanakula mrahaba mkubwa kuliko hazina ya taifa, hebu fikiria shilingi billioni 300 zilizoko uswisi wakati watoto wetu hawana madawati, mama zetu wanalazwa mzungu wa nne hospitali wakienda kujifungua, mahospitali hayana dawa,


  Jiulize ukimsikia mkuu wa nchi anauliza swali kama ulilouliza wewe hapa unapata mawazo gani?

  je wafanya kazi wanapotishiwa na mkuu wa nchi kupigwa manundu kwa kudai maslahi yao au walimu kuburuzwa mahakamani kwa kudai mishahara bora au dakitari kutekwa na kuteswa kwa kuongoza madai ya maslahi unajisikia je? Tatizo letu ni uongozi uliosahau wajibu wake wa kuongoza taifa wakajiona wamekwenda pale kusimamia ufisadi na kula rushwa tu. To most of our leaders; UONGOZI is not about the country and her peoples but about themselves and thier closest relatives.
   
Loading...