Tanzania kuwa mfano katika mapambano dhidi ya Corona?

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
188
169
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na baraka. Yeye ndiye agawaye kwa wote pasipo kuangalia.

Ni takribani week tatu sasa toka wananchi tusikie takwimu mpya za wagonjwa wapya wa COVID-19. Hakika hii inaweza kuwa jambo jema na kutokana na kauli za viongozi wetu kuwa maambukizi yanapungua kwa kiwango kikubwa. Pongezi ziwaendee viongozi kwa namna ya mapambano yalivyokuwa na kuchukuliwa mapema.

Pia viongozi wanatuambia kuwa kuna vingi vimefanywa katika mapambano hayo na mengine si ya kuzungumza hadharani.

Tanzania mapema kabisa iliwekeza katika kuielimisha jamii dhidi ya adui huyu mpya, kwa kuwaelekeza wananchi njia mbalimbali za kujikinga kama vile kunawa mikono, kupunguza miingiliano isiyo na ulazima na kwa kufunga shughuli zote za masomo mwanzoni kabisa. Njia hii ilikuwa ni kupunguza kasi ya maambukiazi na hakika kwa kiasi chake imeweza kuleta mafanikio.

Pia njia hizo zilikuwa ni nusu ya kile ambacho watu wanakiita lockdown kwani ni kundi kubwa sana la wanafunzi walifanya isolation na kupunguza kasi ya maambukizi.

Pia ushirikishaji wa vyombo vingi vya mawasiliano kama vile television na radio, umeweza kuongeza ufahamu wa wananchi kuhusu mapambano haya mapya dhidi ya adui asiyeonekana. Hakika hakuna mtanzania atakayesema kuwa hajapata walau elimu ya kujikinga na Corona.

Wakati Tanzania ikisema kuwa maambukizi ya Corona yamepungua kwa kiasi kikubwa bado inakabiliwa na tishio lingine kuu. Tishio hilo ni nchi jirani kuendelea kuripoti ongezeko kubwa la wagonjwa. Hii inapelekea Tanzania pia kuwa katika hatari ya kukumbwa na maambukizi mapya toka nchi jirani.

Je ni wakati sasa wa kujiuliza njia zile zilizotumika awali ziendelee kutumika au yabidi kubadirisha mikakati.

Ni hakika kuwa Corona itaendelea kuwepo kwa mda mrefu na inabidi pia tujifunze namna ya kuishi nayo huku maisha ya kawaida yakiendelea, lakini hiki kisiwe chanzo cha kuregeza yale yaliyofanyika katika mapambano ya awali.
Kama nchi ya Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa katika mapambano ya Corona, basi nchi nyingine pia zinatakiwa kuiga yale yaliyofanywa ili kufanya maambukizi ya Corona yasiendelee kukua kwa kasi kama inavyoonekana katika nchi jirani.
 
Back
Top Bottom