Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,873
Ili mambo yaweze kwenda kwa kasi kubwa na kufikia adhima ya serikali kwamba ifikapo 2025 Tanzania kuwa power house ya economic hapa afrika.
Watu wengi bado wapo kwenye mawazo ya zamani hawataki kubadilika. Na katika safari ya kisonga mbele inakuwa ni shida sana kuwa na watu ambao hawapo tayari kubadilika. Lakini jambo jema ni kuachana na watu hao na kusonga mbele.
Wanachotakiwa waendelee na mawazo yao lakini wasijaribu kukwamisha jitihada za serikali katika adhima ya kusonga mbele kwa kasi. Hakuna mabadiliko yanayoweza kutokea kwa kuendekeza vitu ambavyo vinarudisha nyuma jitihada yetu.
Watu wenye fikra zilizo dumaa na kubaki katika mawazo mfu ya nyuma ni kuwaacha na sisi kusonga mbele. Lazima taifa lijengwe katika misingi ya kufuata sheria na utaratibu. Sio kuutumia uhuru kwa nia ya kukwamisha jitihada ya kusonga mbele.
Hakuna mtu asiyependa mafanikio ya nchi hii. Lakini kuna baadhi ya watu hasa vyama vya upinzani kila kukicha kuombea tuweze kukwama. Lengo lao ni kwamba wanadhani ni wao wenye dhamana ya adhima ya serikali kufikia uchumi mkubwa.
Hawa watu ninawafananisha na watu huku mitaani wenye roho za korosho. Kila kukicha wanawaza kwamba kwanini yeye apate?
Nchi hii ni ya watanzania na chama cha mapinduzi ndio chenye dhamana ya kuiongoza.
Ninapenda kunukuu maneno ya Shibuda alisema kwamba kama watu wawili wanashidania kumposa binti na bahati mmoja akakubaliwa na akaweza kumuoa, basi huyo wa pili anatakiwa kukaa kimya na kuacha chokochoko za kutaka kuvuruga ndoa. Naye akialikwa kwenye arusi hana budi kwenda. Na huo ndio uungwana.
Yale maneno ya chonganishi wakati wewe umeshindwa hayawezi kujenga zaidi ni kubomoa.
Lakini kwakua serikali iliyo madarakani imeona tatizo hilo la roho za korosho. Itahakikisha inawachukulia hatua wote wanaotaka kuturudisha nyuma. Hapa hakuna kuangalia sifa ya mtu.
Ni hayo. Mawazo huru.