TANZANIA kutokuwa na NYAMBIZI ni aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZANIA kutokuwa na NYAMBIZI ni aibu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BornTown, Sep 15, 2011.

 1. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi nimasikitiko yangu kwa nchi yetu hii ya TANZANIA kutokuwa na hata "kanyambizi kadogo tu!" hivi kweli nchi yetu hii inaulinzi gani madhubuti kiasi cha kujiamiki kutokuwa na nyambizi kwa ajiliya usalama wa nchi yetu. Juzi tumekumbwa na na ajali ya meli ya Mv. Spicer tumekosa wazamiaji tumeomba wa South Africa ni jambo la aibu ikiwa tuna chuo cha Marine na kila mwaka kinatowa wahitimu, haijatosha jirani na ndugu wa karibu South Africa imetusaidia wazamiaji haya wamefika wamekuta meli ndio hiyo ipo kwenye kina kirefu ambapo hawana uwezo wa kufikia hapo wanahitaji Nyambizi ya kuifikia meli ili waweze kuopowa Miili ya wapendwa wetu imeshindikana hadi waombe tena Nyambizi nyumbani kwao.

  Swali langu ni je miaka 50 ya Uhuru tumeshindwa kununua hata kijinyambizi kidogo tu cha watu hata 10 kweli???

  Tanzania inajiamini nini kutokuwa na Nyambizi kwa ajili ya usalama wa nchi. Jeshi la Polisi kitengo cha majini wanafanya nini? ama wao kazi zao ni kuzunguka na boti tu!

  Utajiri wote huu tuliopewa na Mwenyezi Mungu tunashindwa kununua NYAMBIZI!
  Je! Nyambizi moja inagarimu kiasi gani?

  Naomba kuwakilisha!
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu BornTown.

  Tanzania tuko busy kuzalisha mikoa mipya mambo ya nyambizi hayana nafasi.
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red, kumbuka hata MV Bukoba tulipata msaada wa wazamiaji kutoka South Africa, hivi tumewahi kujiuliza kuwa inatumia muda gani kutrain mwanamaji? (miaka 15??? - tangia mkasa wa MV Bukoba mpaka leo si wengekuwa wamefuzu!?)
  Hivi hizo Nyambizi zinakuwa chini ya wizara gani!? ...Ulinzi!? ...kama ni Ulinzi, Ina maana inakuwa chini ya Mh. Hussein Mwinyi, Bw. D. Mwamunyange, Mh. Shimbo nk. ...je inagharimu kiasi gani??? ....je, ni zaidi ya TRILION TATU (3TR)???
  Well, labda watanunua baada ya huu mkasa wa Spice Island. Tusubirie majubu ya tume
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  na kweli yani watawala hawafikirii vitu vya maendeleo hata tone!badala ya kubana matumizi ya administration ktk mikoa wao wanaongeza hivyo more ma vx,majengo,wafanyakazi wa kuhudhuria semina badala ya madaktari na waalimu!sii ajabu waziri mkuu hajui matumizi ya nyambizi.halafu mchango wa jeshi letu la maji mbona sijauona ktk janga hili?
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kiukweli Nchi yetu inatia aibu... mambo ya msingi kwa usalama wetu hayapewi kipaumbele ila yasio ya msingi yapewa kipaumbele kikubwa. Kweli sijaona faida ya kuongeza mikoa, semina elekezi zao kwani hakuna wafanyacho zaidi ya kula pesa za wanyonge, matumizi yasio yalazima ya magari ma VX na V8 nk
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu unazungumzia nyambizi wakati hata wapiga mbizi hatuna????????? Huwa nawashangaa sana wakuu wa serikali kwa kujiona wana hadhi ya hali ya juu wakati hata basic paramedics around them hakuna!!!!!
   
 7. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Si hao tu hata kwenye ajali za barabarani traffic police wanafika bila hata kasha la first aid bali notebooks na peni ku-record dimensions za ajali wakati majeruhi wakiendelea kuumia na hatimaye kupoteza maisha!!!
   
Loading...