Tanzania kutembelewa na wageni mashuhuri duniani mwezi huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kutembelewa na wageni mashuhuri duniani mwezi huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Feb 10, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  VIONGOZI mashuhuri watano duniani wakiwemo Rais wa China Hu Jintao na Katibu Mkuu wa Umoja Ban Ki- Moon wanatarajiwa kufika nchini mwezi huu ili kuimarisha uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.


  Wageni hao pia watakagua miradi ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na nchi zao.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema ujio wa wageni hao utakuwa wa manufaa kwa watanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.


  Akifafanu alisema pamoja na Rais wa Zambia Rupiah Banda kuwa nchini tangu jana, Rais wa China atawasili Februari 14 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, atawasili nchini Februari 25.


  Membe alisema viongozi wengine watakaotembelea nchi ni Rais wa Uturuki Abdullah Gul na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Kamalesh Shama.


  Kuhusu ujio wa Rais wa China , Membe alisema kutokana na urafiki kati ya nchi hizo, Rais huyo anakuja kwa lengo la kuangalia miradi iliyofadhiliwa na nchi yake pamoja na kupanga mikakati mipya ya kuboresha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya nchi mbili.


  Katika hatua nyingine, waziri Membe alifafanua kuhusu mambo yaliyoafikiwa katika mkutano wa Umoja wa Afrika katika kuunda serikali ya Umoja wa Afrika na kusema Umoja huo hauwezi kuundwa kama miundombinu muhimu haitaboreshwa kwanza.


  Alisema viongozi wa Umoja huo waliazimia kuboresha kwanza miundombinu hususani ya barabara na kwamba fedha za kutekeleza masuala hayo, zingine zitatokana na mpango mpya wa kutoza dola mbili za marekani kwa kila tiketi ya ndege za kimataifa katika Bara la Afrika.


  Alibainisha kuwa katika kufanikisha hilo kila tiketi moja ya ndege itatozwa kiasi cha dola mbili ambazo zitaingia katika mfuko wa kuboresha miundombinu Afrika.


  Kuhusu miundombinu ya barabara, Membe alisema barabara sita zitapewa kipaumbele hususan zile zinazoanzia kaskazini hadi kusini mwa Afrika ambazo ndizo njia kuu za kuweza kuinganisha Afrika kibiashara na kurahisisha mawasiliano.


  Barabara hizo ni za kati ya Cairo hadi Cape Town inayopitia Tanzania na nyingine ya kuanzia Tripol Libya hadi Cape Town kupitia Afrika Magharibi


  Pia barabara nyingine ni ile itakayotokea katikati ya Jangwa la Sahara hadi Sudan kupitia, Libito hadi Kenya na Beira hadi Kinshasa.

  Source:Mwananchi
   
Loading...