Tanzania kutembelewa na matajiri wakubwa zaidi duniani ndani ya mwezi mmoja, inamaanisha kitu fulani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kutembelewa na matajiri wakubwa zaidi duniani ndani ya mwezi mmoja, inamaanisha kitu fulani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fazili, Jul 12, 2011.

 1. f

  fazili JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,192
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Tumeona mwezi wa sita mwishoni na mwanzoni mwa mwezi huu wa 7 Tanzania ikitembelewa na Bill Gates ambaye ni tajiri number 2 ? duniani na pia Mukesh Ambani ambaye ni tajiri number 4 duniani.

  Wote wameahidi kuwekeza Tanzania. Wakati Bill Gates akiahidi kuwekeza kwenye utafiti wa afya na kilimo, Ambani atawekeza kwenye mahoteli na usafiri wa anga.

  Ujio wa watu hawa Tanzania waweza kumaanisha neema ama balaa, kwani kama watanzania tutaweza kuhakikisha kwamba uwekezaji huu unakuwa na tija kwetu basi itakuwa neema. Vinginevyo tukifanya mikataba ya kupuuzi basi tutaishia kunyonywa nguvu zetu na jasho letu litakwenda ama Marekani au Asia huku tukiachwa maskini wa kutupwa.
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hizi maliasi hatafaidi watanzania.
   
 3. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  acha waje tushazoea...
   
 4. JS

  JS JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yani unaonekana/unasound ushakata tamaa kabisa huna imani na chochote tena.....usiwe hivyo bana jaribu kuwa positive kidogo.Tuombe tu wasiwe walaghai lakini hawa wajamaa huwa si walaghai ila watekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na matajiri hawa ndo huwa walaghai.
   
 5. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  kwa interests zao siyo taifa letu.
   
 6. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tufanyeje sasa kula anakula mkubwa. ndo hivyo hivyo 2.
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Hata wakitaka kununua mlima kilimnjaro,watauziwa na mafisadi
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  halafu hii beggar's mentality ya viongozi wenu
  inatia simanzi kwa kweli

  wao wanafikiri matajiri ni kama watu fulani wenye miujiza

  wakati ukiweka mazingira mazuri tutaweza zalisha hapa hapa
  matajiri wakubwa wa halali....level hizo za kina ambani
   
 9. M

  Milano Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ujio wa matajiri hao hakuna ubaya, maana yake nchi yetu inavutia wawekezaji. Tusiwe na mtazamo mbaya kwa kila kitu, cha msingi hapa tunakosa viongozi wazuri ambao. Tungekuwa na viongozi makini ujio wa watu hao ni neema, maana hawa mabilionea wakishatia mguu hapa makampuni mengi yatakuja wekeza halafu tuje kuwa kitovu cha uchumi afrika mashariki na kati, ila tu uzuzu wa viongozi wetu ndio tatizo.

  Makampuni makubwa ya wamarekani na ulaya yaliwekeza huko Japan, na baadaye China, Korea na nchi nyingine za ukanda wa Indonesia leo wako mbali. Tuvute subira tupate viongozi wazuri hapa neema itakuja tu. Kumbuka huwezi kupendelewa kupata wawekezaji kama huna hali inayovutia wawekezaji kama rasilimali, soko, nchi kandokando tunazopakana nazo ambazo ni soko la uhakika.

  Tunataka Arusha iwe Jeneva ya Afrika yakhe, na wazenj watashangaa kuona tunaenda kwa magari kwa dakika 40 tu, wakijitenga watajutia kuzaliwa.
   
 11. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa Bill Gate sina wasi naye kwani anawekeza ktk maeneo yatakayomfanya yeye ndo aingie mfukoni zaidi kutusaidia sisi na isitoshe huyu jamaa ana roho ya kinadamu kwani pesa zake nyingi amezielekeza kwenye nchi maskini.


  Huyo Mukesh naye labda anaweza kutuumiza hapo kwenye mahoteli ambayo nadhani yatachukua maeneo makubwa huko mbugani lakin kwenye anga wala hawezi kutugusa sisi wavuja jasho ambao hatufikirii hata kupanda hizo ndege.
   
 12. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa ufinyu wa raisi tulienae madarakani hata aje Yesu ama Muhammad hasaidiki na hatafanya chochote cha maana manake hana clue ya ku-run hii nchi wala hana vision yoyote kazi kusafiri tu, akingojea miaka yake mitano iishe ajilimbikizie aingie mitini.
   
Loading...