Tanzania: Kushuka kwa thamani ya shillingi, mfumuko wa bei na siasa zetu!

...Utapambana vipi na mfumuko wa bei wakati Serikali iliyopo madarakani ni Serikali taahira? Hilo haliwezekani kabisa....Sasa hivi mfumuko wa bei umefika 20% miezi sita ijayo utafikia 25%. Na siajabu muda si mrefu ujao tutakuwa na hali kama waliyokuwa nayo Zimbabwe miaka michache iliyopita.
 
Ni kweli mkuu hebu tutafakari kwa kina. Mi naweza changia kidogo hebu angalia ofisi zetu binafsi na za umma utakuta furniture zote ni kutoka abroad sasa kama kweli tunataka kupunguza ukosefu wa ajiri inabidi tuwe na sera kuhusu hili kwamba furniture zote maofisini ziwe home made na kama tutaona zinazotengenezwa hazina ubora tuwekeze. Ni kwa njia hii tu tutaweza kutatua tatizo la ajira, hebu angalia tuna ofisi ngapi nchi nzima? Na ni soko kubwa sana kwa bidhaa zetu kama tukiamua. Hii ni njia mojawapo ila kuna nyingine nyingi wenzangu watachangia.
 
Njia pekee ni kuongeza uzalishaji wa vitu ili tuweze kulitumia soko la ndani ambalo sasa limekuwa jalala.
 
Maisha bora kwa kila mtanzania " watanzania tulilogwa kuchagua wehu". hakuna wanalojua zaidi ya kujilimbikizia wao na watoto wao. wako tayari watanzania wote wafe ili mradi wao wapate. Dogo RIZ ana yafuatayo jao hana kazi ( Dalbit- kampuni ya kusafirisha mafuta nje ya nchi na ina semi trailer kama mia tano, Lake oil, makone radio- mtwara, makonde lodge, gorofa karibu na GBP sinza na mengine ambayo hayafai kuelezea. Mtwara kaweka Range ya kutembelea), sasa haya maisha bora kwa kila mtanzania tunayapata wapi? Angalia picha za mzee. Akiambiwa jamaa zake wanaifilisi nchi yeye kucheka tu. View attachment 45772
 
Maisha bora kwa kila mtanzania " watanzania tulilogwa kuchagua wehu". hakuna wanalojua zaidi ya kujilimbikizia wao na watoto wao. wako tayari watanzania wote wafe ili mradi wao wapate. Dogo RIZ ana yafuatayo jao hana kazi ( Dalbit- kampuni ya kusafirisha mafuta nje ya nchi na ina semi trailer kama mia tano, Lake oil, makone radio- mtwara, makonde lodge, gorofa karibu na GBP sinza na mengine ambayo hayafai kuelezea. Mtwara kaweka Range ya kutembelea), sasa haya maisha bora kwa kila mtanzania tunayapata wapi? Angalia picha za mzee. Akiambiwa jamaa zake wanaifilisi nchi yeye kucheka tu. View attachment 45772

Kama ni kweli hayo uliyo yataja,nafikiri miaka si mingi itabidi atujuze watanganyika hizo mali kazipa vipi!
 
[h=6]Ndugu wanajukwa hali ya maisha ya watanzania inazidi kuzorota kila kukicha na hili tunaliona wazi kwenye nyanja nzima ya uchumi wetu. Mfumuko wa bei unazidi kupanda kila kukicha watanzania wahali ya chini tunazidi kutaabika na mfumuko huu wa bei ambao sasa upo 19.8% na inaonesaka Serikali yetu haiweki mikakati ya kutosha kutatua swala hili. Mbali na matatizo ya kiuchumi katika bara zima la Afrika na Duniani kwa ujumla ila hatuweza tukatumia kama kisingizio cha kusema kuwa hatuwezi kutatua kwa kutumia baadhi ya fursa tulizo nazo. hivi ikiwa gharama ya Umeme inapanda na pia mbali na kupanda umeme wenyewe umekuwa hadimu tunategemea uchumi utakuwaje?

kama pia kunamfumuko wa bei kwa kiwango hichi tunategemeaje kuzalisha ajira? hali ya ajira ni mbaya na itaendelea kuwa mbaya kama jitihada za makusudi hazitafanyika. na hivyo kwa hali hii mbona kazi ipo Mwaka huu. mchele ni 2200 na 2500, Unga 1000 na 1200, maharage Sh. 2,300 na Sh. 2,500, sukari Sh. 2,200 hadi Sh. 2,600. Vitunguu Sh. 5,500 kwa kisado. nyanya 1kg Sh. 4,000. Viazi Sh. 14,000. Watendaji wamepuuza swala la kiuchumi sambamba wanasiasa pia wamepunguza hili swala. Vyama pinzani tuliona mmelishikilia bango kwa kipindi ila sasa nanyi tumeona mmepoa. hivi kwel kama bado watanzania tunaishi chini ya dola 1 tunaweza kupata angalau Mlo mmoja kwa siku? ifike wakati Watawala (Rais, Waziri Mkuu, Wabunge n.k) waweke hili swala kuwa kama kipaumbele cha kwanza kwa sasa.

siasa pembeni maisha ya watanzania kwanza.
[/h]

Umeme 40% juu kwa wananchi wabangaizaji while hao wanaowaita wawekezaji uchwara ambao me naona ni wachukuaji waliotufanya watanzania tuishie kwenye uchuuzi wa bidhaa fake za nje wamepata nafuu ya umeme!huu si utahaira huu!watanzania tuamke!siasa si ushabiki kama wa mpira tu,siasa ni maisha
 
Kama ni kweli hayo uliyo yataja,nafikiri miaka si mingi itabidi atujuze watanganyika hizo mali kazipa vipi!

kwa sasa baba kashikilia mpini hatuwezi kuhoji. Lakini ukweli mzee ndo anapakua na kuwekeza kwa mtoto.
 
Tukumbushane kidogo bei za zamani kama unakumbuka na kulinganisha na garama ya sasa je ni sawa
Jana gazeti la mwananchi 500 leo ni 8oo
2oo5 m/taa 400 leo.....................
 
Mkate mwaka 2005 ulikuwa=TSH 250 sasa Tsh 1500
Sukari mwaka 2005 ilikuwa=TSH 500-1000 sasa Tsh 2500
Mchele Mwaka 2005 ulikuwa=Tsh 500-1000 sasa Tsh 2500-3000
Nauli ya Daladala tsh 150 sasa Tsh 300 mpaka 400
Posho ya Wabunge Tsh50,000 sasa Tsh 330,000/=
 
Nakumbuka betry za national tulikua tunanua sh100 sasa ni sh600.

Ndoo ya maji bombani ilikua sh5 sasa ni sh100
 
Nilinunua lita moja ya Petrol 486 Mwaka 2004 mwishoni lakini sasa ni zaidi ya 2000 toka wakti huo mpaka sasa mshahara wangu uliongezeka kwa 20%
 
chumvi ilikuwa 100 sasa hv 300,soda 200 sasa 600. Bia 700 sasa 1500
 
kiberiti sh.20mwaka 2006 na sasa sh.100 jojo sh 10 mwaka 2006 na sasa sh.50
 
Nauli kutoka Morogoro kwnd Singida mwaka 2004 ilikuwa 8500..Sasa 22,000.
 
Zamani ukiingia na 500 hotelini inatosha breakfast, sasa hivi hadi 2000 na kuendelea,
chapati ilikuwa 50/= sasa hiv 300/=
 
2005 pale sewa buguruni short time ilikuwa sh. 1000-2000, 2012 sh. 5000 na kuendelea

2005 salama 3 (pakiti 1) sh. 100, 2012 (pakit 1) sh.400
 
Mwaka 2003 kilo ya nyama mkoani Tabora iliku wa sh.700.sasa ni 4000.viazi fungu ilikuwa 100 sasa 500.gunia la mkaa lilikuwa 3000 sasa 10000.kodi ya chumba ilikuwa 3000 mpaka 5000.sasa ni 10000 mpaka 25000
 
Back
Top Bottom