Tanzania Kushawishi Nchi za SADC Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wataalamu wa Mazingira kutoka Tanzania wanaoshiriki katika mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa SADC wameanza juhudi za kuzishawishi nchi wanachama wa SADC kupiga marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ili kudhibiti uharibifu wa mazingira katika ukanda huo.

Akizungumza mara baada ya kuhudhuria mkutano wa wataalamu wa maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii kwa nchi za SADC, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Raisi,Kemilembe Mutasa amesema kuwa katika mkutano huo wa wataalamu kutoka nchi za SADC wamekua wakizishawishi nchi mwanachama kuridhia itifaki ya hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku matumizi ya SADC.

“Tunatumia fursa ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa SADC kushawishi nchi mwanachama kuhimiza agenda ya marufuku ya mifuko ya plastiki iweze kutolewa kwa nchi zote ikiwa ni mkakati wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ,Cletus Shengena amesema kuwa wataalamu wa mazingira kutoka nchi za SADC wamekua na mikutano ya kuweka mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiko ya tabia ya nchi ambayo ni changamoto kubwa inayokabili nchi wanachama Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo.

Shengena amesema kuwa mkakati huo utawasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na athari ambazo zilizoanza kujitokeza ikiwemo mafuriko na upepo mkali na vimbunga katika nchi mwanachama.

Afisa Mazingira Mkuu wa Ofisi hiyo, Emelda Teikwa Adam amesema kuwa wameangazia fursa za kukuza uchumi wa nchi za SADC kwa kutumia uchumi wa bluu unaojulikana kama uchumi wa bahari unaotumika kwa njia ya usafirishaji, uvuvi na kutoa nishati kwa maana ya uchimbaji wa mafuta na gesi kama njia za kukuza uchumi wa nchi za SADC.

Emelda anasema kuwa ili uchumi huo uwe endelevu mazingira yanapaswa kutunza na kulindwa ili wananchi waweze kunufaika na fursa za uchumi wa bluu ambao ukitumika vizuri unaweza kupunguza umasikini.

Ends.


,
IMG-20191024-WA0010.jpeg
 
Hongera Magufuli
Mafanikio yako toka uchaguliwe kuwa kiongozi wa sadic yanaonekana sasa
 
Back
Top Bottom