Mdakuzi mkuu
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 212
- 719
Ninapojaribu kuwaza na kutathmini kwa kina juu ya mwelekeo hasi wa vyama vya upinzani hapa nchini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kujiimarisha zaidi.
Nguvu ya upinzani iliyokuwepo kuanzia mwaka 1992 mpaka 2015 haitakaa ijirudie tena. Wapinzani wanapwaya sana, hawana makali kama huko nyuma. Makada wengi wa upinzani wanazidi kupotea kimya kimya.
Mbaya zaidi, Mh Rais Dk John Pombe Magufuli "mzee wa hapa kazi tu" ameonekana kufanya mambo mazuri na ya kihistoria ambayo kwa miaka nenda rudi, wapinzani wamekuwa wakiimba nayo kila kukicha. Sasa watasema lipi tena? Maana kama kubanwa, tumebanwa wote kiasi kwamba hata hao wapinzani wanaomba "elegeze koki".
Na wapinzani wawashukuru sana akina Lowasa, Sumaye kwa kuamsha-amsha huko mikoani. Bila hivyo sasaiv wangekuwa kimya kama panya kabanwa na mlango. Mbowe ameacha siasa, amegeukia kilimo huko jimboni kwake.
Watu wenye kelele wote hoi. CCM itaendela kupeta kwa kuwa wanayafanyia kazi malalamiko mengi ya upinzani na wananchi kwa ujumla.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM