kirengased
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 5,987
- 6,646
Ingefaa waziri aweke 'komitimenti' kwamba utalii ukishuka naye cheo kinashuka mpaka kuwa 'tuwagaidi' maana vivutio vyenyewe havitangazwi vizuri kiiivyo mpaka tuwaongezee gharama nao waridhie
Wewe ndiyo aidha hujui cho chote kuhusu kodi za serikali au umeamua kupotosha kwa masilahi yako binafsi.Hujui unachoongea/unachoandika.
VAT is an indirect tax which was exempted, unlike Corporate tax.
Mtalii halipi kodi. Mtalii analipa tour company kwa package anayotaka kupitia wakala au directly.
Tour operator analipa TANAPA na NCAA (hayo ni mapato kwa serikali) kwa kila mtalii anayeingia katika mbuga na analipa kodi kutokana na faida kampuni inayopata.
Kwa hiyo kusema watalii hawalipi kodi ni kusema uongo au kuongea usichokijua.
Tour operator anauza package kwa mtalii, hapa ameuza bila VAT. Let's assume ameshauza $100 VAT excl. Sasa Gvt inasema VAT will be charged. $18 extra ambayo mtalii halipi maana ameshakulipa na kuingia mkataba na wewe. Tour company itapata loss ya hiyo $18. Fanya kwa watalii wote wanaokuja Tanzania kuanzia 01 July ambao most of them walishafanya bookings miezi na miaka nyuma.
Kampuni hizi zimeajiri Watanzania. Kampuni zinanunua vyakula kutoka kwa Watanzania. Zikipata hasara multiplier effect ni kubwa.
Wewe ndiyo aidha hujui cho chote kuhusu kodi za serikali au umeamua kupotosha kwa masilahi yako binafsi.
Kwa hiyo huo utaratibu uliokuwa unatumika kama ulivyouelezea unauona ni sahihi.
Yaani mbuga ni za taifa kwa manufaa ya taifa. Halafu tunamuachia kampuni binafsi jukumu la kupokea fedha zote toka kwa watalii halafu baadaye eti akailipe TANAPA.
Yaani hiyo kampuni binafsi ndiyo imekuwa mmliki wa hizo mbuga?
Yaani TANAPA na TRA wamekaa tu inactively kumsubiri tour operator awaletee alichopata, wao hata data hawana.
Hili haliwezi kuendelea. VAT na kodi zingine kama coperate tax lazima zote zilipwe na hawa operators na lazima wawe na mashine za EFDs.
TANAPA, TRA na mamlaka mengine ya serikali kama immigration lazima sasa ziwe active ku track watalii hawa nia ya serikali kupata malipo yake stahiki.
Kisingizio eti cha multiplier effect, eti tunatoa ajira is just nonsense kwani nani ambaye hafsnyi ajira au hiyo multiplier effect? Kwanza ni vyema TANAPA yenyewe ikafanya shughuli zote zinazoendeshwa na hizo kampuni za tour operators.
Lakini mkuu The Boss hii 18% VAT itaiingizia serikali tshs bilioni 7.
Hivyo TRA wamegundua hiyo "loophole".
Idadi ya watalii wataongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 2.
Serikali nyingi sasa zinazuia biashara haramu ya nyara za serikali kupitia uwindaji haramu, hivyo utalii kwa njia hii unapungua.
Asilimia 18 ya VAT inayokatwa ni ndogo sana kwenye huduma kama ya kukodisha turubai la kulala porini kwa siku saba au huduma ya wabeba mizigo.
Asilimia 18 haitakatwa kwenye package nzima ya mtalii akija bongo kiasi cha kumfanya huyo mtalii asitishe safari yake.
Mtalii anapofika Arusha na anaanza kutumia huduma za hapo si ndipo anapoambiwa kuwa gharama ya kukodisha turubai imepanda kidogo?
Kwahio kwa mfano mkodishaji turubai ambae ni mlipa kodi kihalali anapaswa kuwa na stakabadhi ya malipo na mashine ya kufanyia malipo ili aweke hesabu zake sawa.
Bila hii kodi serikali inakuwa inakosa pato la bilioni 7.
Hivyo hiyo ndio njia dhahiri ya kukusanya kodi hiyo.