Tanzania kupeleka majeshi Zimbabwe

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,004
2,000
Wakati mkiendelea kutafakari uamuzi wa Tanzania kupeleka majeshi nchini Comoro, Setikali imetangaza kuwa iwapo itaombwa, ipo tayari kupeleka majeshi yake nchini Zimbabwe ili kumng'oa kiongozi ambaye atang'angania madaraka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Hayo hayajasemwa na mwingine bali waziri Mkuu, Mizengi peter Pinda, wakati alipozingua utaratibu wa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge leo asubuhi.
Alitoa jibu hilo kutokana na swali lililoulizwa na Zitto kabwe aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusiana na hatua ya Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuchelewa kutangaza matokeo na serikali inafikiria kuchukua hatua gani ili kuhakikisha nchi hiyo haitumbukii katika mgogogor wa umwagaji damu?
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,852
0

Alitoa jibu hilo kutokana na swali lililoulizwa na Zitto kabwe aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusiana na hatua ya Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuchelewa kutangaza matokeo na serikali inafikiria kuchukua hatua gani ili kuhakikisha nchi hiyo haitumbukii katika mgogogor wa umwagaji damu?Jamani Mheshimiwa P, mbona anaanza kuzingua tena, unakumbuka misemo ya kibanzi na boriti?
 
S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,141
1,195
Wakati mkiendelea kutafakari uamuzi wa Tanzania kupeleka majeshi nchini Comoro, Setikali imetangaza kuwa iwapo itaombwa, ipo tayari kupeleka majeshi yake nchini Zimbabwe ili kumng'oa kiongozi ambaye atang'angania madaraka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Hayo hayajasemwa na mwingine bali waziri Mkuu, Mizengi peter Pinda, wakati alipozingua utaratibu wa kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge leo asubuhi.
Alitoa jibu hilo kutokana na swali lililoulizwa na Zitto kabwe aliyetaka kujua msimamo wa serikali kuhusiana na hatua ya Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuchelewa kutangaza matokeo na serikali inafikiria kuchukua hatua gani ili kuhakikisha nchi hiyo haitumbukii katika mgogogor wa umwagaji damu?

Naanza kuona kuna watu wanatafuta LEGACY za chap chap.
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
Kumbe yalikuwa kwenye maswali ya chapchap?

Hilo wala halipo, Zimbabwe haijafikia hapo kwani hakuna aliyekatalia madaraka na Tsvangirai anakataa kuingia duru ya pili.

Labda upatanishi kama ule wa Kenya, Mzee Mkapa anaweza kwenda kusuluhisha.
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,004
2,000
Acheni kukopy na kupaste tuuuuuuuuuuuuu, tafuta habari adimu ili magazeti yacopy hapa please, naona JF imekuwa ni kwa ajili ya copy and paste News from papers!!!

Sawa Mkuu, lakini hii imekopiwa kutoka katika gazeti gani?
Na (hata kama ingekuwa imekopiwa kwenye gazeti) kuna ubaya gani kujadili yanayoandikwa kwenye magazeti yetu?
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,437
2,000
Tanzania wanataka kuonyesha nchi za jirani kwamba jeshi letu ni imara na Tanzania inatakiwa kuheshimiwa.
 
Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,852
0
Tanzania wanataka kuonyesha nchi za jirani kwamba jeshi letu ni imara na Tanzania inatakiwa kuheshimiwa.

Kuwa na jeshi imara ilhali wananchi wako wanapata mlo mmoja kwa siku haimake sense. Serikali yetu ingejitahidi kutumia pesa kuimarisha uchumi badala ya kuimarisha majeshi
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,176
2,000
..viongozi wetu wajivunze kusema " I do not have all the facts right now..."

..sasa Waziri Mkuu Pinda anadai wako tayari kupeleka majeshi ikiwa wataombwa. Sasa wakiombwa na nani? Kwa malengo gani?
 
Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Source please,
Huyu Pinda anapakaziwa au ni mtupu kabisa?

How can Pinda say that without first establishing the results? Unajua hilo liko diplomatically explosive? Vipi kama Mugabe atashinda na Morgan akaomba majeshi ya Tanzania yaende, tutatumia kigezo gani kuingia?

Why didn't this make headlines? Is today April the first still or are our journalists kaput?

I shouldn't even ask any question until a verbatim quote is produce citing credible sources.
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
..viongozi wetu wajivunze kusema " I do not have all the facts right now..."

..sasa Waziri Mkuu Pinda anadai wako tayari kupeleka majeshi ikiwa wataombwa. Sasa wakiombwa na nani? Kwa malengo gani?

Acha hizo! Mheshimiwa P kazi yenyewe ndio bado anajaribu kuizoea kisha interview ya kwanza tu unahitimisha.

Mpe muda kidogo tuone; maswali yatakuwepo kila Alhamisi na bila shaka akina "Lunyungu" watajaribu kumharibia.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,896
2,000
hahaha maswali ya pao kwa papo ni balaa sana maana unaweza ukaja tofautiana na mkulu wa bangoi itakuwa balaa..bure kupeleka majeshi...mmm msala wajua..vipi kama wakiombaa..waende somalia na sudan?wataendaa?kwa gharama ya nani?bajeti je??
 
Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Acha hizo! Mheshimiwa P kazi yenyewe ndio bado anajaribu kuizoea kisha interview ya kwanza tu unahitimisha.

Mpe muda kidogo tuone; maswali yatakuwepo kila Alhamisi na bila shaka akina "Lunyungu" watajaribu kumharibia.

Kama kweli alisema hili, tuna kiongozi wa ajabu sana kuliko nilivyokuwa naamini. Tena ni utoto kujitetea kwamba lilikuwa swali la chapchapa au ilikuwa siku yake ya kwanza. Ni vizuri pia ukatafakari kidogo implications zake kwa nchi yetu katika mahusiano ya kimataifa na kidiplomasia.

Maswali ya chapchap ndiyo yanatoa picha ya uwezo wa kiongozi na hapa tumeshathibitisha yale tuliyokuwa tunayajua kuhusu uwezo wa kiongozi wetu huyu. My only hope ni kwamba hakusema hili ambalo limeletwa hapa, kama alisema basi tuna hali mbaya sana ya uongozi katika nchi yetu!
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,875
2,000
Kitila unasema ? Maana sijakuelewa hapa mkuu .Maswali jamaa anasema alishitukizwa ama ?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,176
2,000
kakalende said:
Acha hizo! Mheshimiwa P kazi yenyewe ndio bado anajaribu kuizoea kisha interview ya kwanza tu unahitimisha.

Mpe muda kidogo tuone; maswali yatakuwepo kila Alhamisi na bila shaka akina "Lunyungu" watajaribu kumharibia.

kakalende,

..Waziri Mkuu Pinda siyo kijana aliyetoka chuoni majuzi kwamba anajifunza kazi.

..Waziri Mkuu Pinda alikuwa msaidizi wa Raisi kwa muda mrefu tu. baada ya hapo ame-serve ktk serikali ya Mkapa na sasa ya Kikwete.

..tatizo ni viongozi wetu kujidai wana majibu ya kila swali wanaloulizwa.
 
Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,252
2,000
Kama kweli alisema hili, tuna kiongozi wa ajabu sana kuliko nilivyokuwa naamini. ...

Maswali ya chapchap ndiyo yanatoa picha ya uwezo wa kiongozi na hapa tumeshathibitisha yale tuliyokuwa tunayajua kuhusu uwezo wa kiongozi wetu huyu.

Kitila hapa umesema kweli, kuna kiongozi mmoja alinukuliwa akiwataka watanzania waachane na amani na utulivu.
 
think BIG

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
236
195
..tatizo ni viongozi wetu kujidai wana majibu ya kila swali wanaloulizwa.

Tatizo ni kuwa ni wavivu wa kuelewa na kupambanua! Hii kauri kama ni ya kweli kutoka kwa Mh. Pinda, basi atakuwa amenishangaza mara 2 kwa siku 2 mfululizo

La kwanza, ni jana na suala la EPA/, sitaki kulizungumzia hapa.

La pili ni ili la nchi mjumbe wa SADC, anasema wakiombwa msaada wa kijeshi, ... hivi msaada wa kijeshi kwa mapinduzi gani yaliyofanyika nchini Zimbabwe mpaka sasa? Hivi hilo jeshi la Zimbabwe ambalo linatakiwa kisheria kumtii Kiongozi wa nchi kwa sasa linamtii nani? Mpaka sasa nani ni kiongozi halali wa Zimbabwe?

Mh Pinda anafahamu kuna mkutano wa dharura umeitishwa nchini Zambia kwa wajumbe wa SADC ili kuzungumzia suala la Zimbabwe. ...Sasa yeye (Mh. Pinda) anatoka wapi na suala la jeshi. Hivi mjumbe wetu (TZ) atakwenda kwenye huu mkutano kuzungumzia suala la kupeleka jeshi?

Tatizo si jeshi kuvamia wala nini ... Tatizo ni Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) kutangaza matokeo. Leo hii ukiwaambia Wazimbabwe SADC inampango wa kupeleka jeshi kila mmoja atashangaa, haijafikia hatua ya kupeleka jeshi.

Hatua ya kwanza ZEC itangaze matokeo either halali au batili! Sio suala la jeshi .. wapi na wapi. Katika hili Mh. Pinda amepinda.
 
Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,555
0
Source please,
Huyu Pinda anapakaziwa au ni mtupu kabisa?

How can Pinda say that without first establishing the results? Unajua hilo liko diplomatically explosive? Vipi kama Mugabe atashinda na Morgan akaomba majeshi ya Tanzania yaende, tutatumia kigezo gani kuingia?

Why didn't this make headlines? Is today April the first still or are our journalists kaput?

I shouldn't even ask any question until a verbatim quote is produce citing credible sources.

Unskilled? Lacking any meaningful qualifications? Don't worry, your country needs you.Now guess who we got?

PINDA

I have to say that I am disgusted by the bit of human garbage known as " Prime Minister " and I thought it would be good to see highlighted in print a reference to the fact that whilst Garbage is on yet another freebie and grinning from ear to ear, the supported JK in sending our boys to Comoro on his personal "see how great I am"

Its only about time ukawona PRO WAR brigade (Mwanakijiji et al)wakianza kutable motions kwa nini tusiiunge mkono serikali ya CCM kupeleka majeshi Zimbabwe..lakini hawa hawa hawaishi kulalama kuhusu ufisadi left and right na hakuna aliyetaka kuuliza hard questions kuhusu gharama ya vita kule Comoro
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom