Tanzania kuongoza kikosi cha Jeshi la Kimataifa DRC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kuongoza kikosi cha Jeshi la Kimataifa DRC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabayi, Sep 25, 2012.

 1. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tanzania imepewa jukumu la kusimamia na kuongoza kikosi cha jeshi la kimataifa la nchi za maziwa makuu lisiloegemea upande wowote litakalokuwa Mpakani mwa DRC na Rwanda.Hii ina tafsiri gani kwa jeshi letu na nchi yetu? Je ila Sifa ya JWTZ iliyojengwa na Mwalimu kipindi kile bado ipo hadi leo au haya mataifa yanaendelea kuamini hivyo wakati sio kweli? Au ni kweli Jeshi letu bado lipo makini na madhubuti hasa ukizingatia bado linashiriki katika operesheni nyingi za kulinda amani kimataifa?
   
 2. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,028
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Uhuni mtupu. Kwa mtazamo wangu wanataka tu k uujua udhaifu wetu toka vifaa tulivyonavyo hadi wa mafunzo ili hao Watutsi waweze kuandaa hiyo HIMA EMPIRE kwa uzuri zaidi. Hii ni kwa vile kwa sasa jeshi letu ni dhaifu katika nyanja hizo mbili (vifaa -vifaavita na vya msaada na mafunzo kwa askari na maafisa). Kwa upande wa maafisa zamani jeshi lilikuwa (TMA) likiwaandaa MAKAMANDA lakini siku hizi linaandaa MAAFISA.

  Kwa kweli siipendi hali hiyo.

  Bazazi ni Bazazi!
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Acha wakajinoe noe kidogo!
   
 4. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,348
  Likes Received: 6,696
  Trophy Points: 280
  hakuna mto huko!!
   
 5. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  JWTZ lilikuwa, wengi wao ni wahuni na kazi yao ni kupiga raia wema
   
 6. serio

  serio JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  haya majukumu anatoa nani??????? kila siku sisi ni wakupeewa majukumu tuu.... agrhhghrh
   
 7. i

  iseesa JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jenerali SHIMBO na mkuu wa kaya wamelifanya kuwa JCCM (jeshi la CCM) badala ya JWTZ (Jeshi la Wananchi wa Tanzania)
   
 8. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ukiangalia uhusiano wa nchi zote za maziwa makuu na mgogoro wa DRC.. tz ni lazima ipewe jukumu
   
 9. M

  Mundu JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nadhani ni zoezi zuri kwa majeshi yetu...Hili ni kama mashindano ya Challenge kwao!!
   
 10. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Waache JWTZ wakapashe huko. Huenda wakahitajika kuingia Malawi muda si mrefu ikiwa Malawi wataendelea kujifanya kichwa ngumu.
   
 11. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  tuache kuponda kila kitu.., hii ni heshima kwa jeshi letu.., kuna mijitu hata kama maskini sana unajitahd kumlisha kila siku akienda kwa jirani analalamika tunakula kuku kila siku lakn mm nakula vipapatio. wakati hivyo vipapatio hana hata sumni ya kuvinunua hana..,

  Hiyo contigent itakua ni recce part (recconaissance) kuchunguza m23 ana nguvu gani (idadi ya wapiganaji), vifaa alivyonavyo, maeneo walipo na kwa idadi gani pia hapa wataangalia landscape, accessability, supply chain ya vifaa na chakula, na kuandaa model ya kistratejia kwa ajili ya maandalizi ya deliberate attack itakapopangwa..,
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  gazeti la champion limeandika leo kwamba kuna nchi jirani mbili zinataka kuivamia bongo, na JK kashtuka.
   
 13. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  itaongozwa na jasusi la jeshi, kamanda mwakibolwa...,
   
 14. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ngoja wakapashe kidigo wamekaa muda mwingi mno makambini bila vita....ndio maana wengi wao wana vitambi siku hizi
   
 15. U

  Ukana Shilungo JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 911
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  acha kujishushia heshima ndogo uliyokuwa nayo mkuu!
   
 16. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  JW hawa ambao wakati wa uchaguzi wanatangaza wako tayari........! Sasa sijui wako tayari kwa lipi? wameshindwa kulinda mipaka ya nchi wao wanalinda wapinzani wasiingie ikulu, mnakumbuka Zanzibar JWTZ ilivyooingia mitaani eti kulinda usalama! sijui usalama upi ambao wenye jukumu lao polisi wameshindwa?
  Malawi imewatetemesha hatujawasikia kusema lolote zaidi ya kumponda Lowassa?
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  Katika posts zote, ya Nyarubongo ndiyo imesummarize kila kitu.
  Hii inaifanya post yako kuwa ya kilimbukeni.
  Kwa kuwa post yako ni ya kilimbukeni, hii inafanya wewe mwenyewe uwe limbukeni.
  Hebu nenda uani huko!!
   
 18. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizi ndizo lugha ninazo taka kuzisikia humu, mimi nasikitika sana ninapo ona/sikia Watanzania wenzetu wanaponda JESHI lao! Wengi wanao lisema vibaya jeshi wala hawajuhi linavyo fanya kazi na si ajabu hawakuwahi hata kwenda National Service. Mkuu wala hapakuwepo ulazima hata wa ku-diclose kila kitu, ni wachache sana watakuelewa. Nimependa sana ufafanuzi wako-umekwenda shule MKUU - God bless TANZANIA na jeshi LETU.
   
 19. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Chezea Watutsi wewe wajanja sana acha sie tufikiri kuwa ni sifa kumbe wanatusoma then waje kutuchakaza.Nani asiejua kuwa Rwanda ndo inayoivuruga Congo? Kwa nini wasimkamate Kagame ili suala hili liishe tu.Rais wangu Kikwete juzi alienda Uganda eti kujadili suala la vita vya DRC yamkini atakua alienda na agenda mbali mbali.Kufika pale uwanja wa Entebe naona ziliyeyuka maana Mseveni na Kagame wanajua wanachokifanya kule DRC
   
 20. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280
  Kuna ngoma mbichi inatusubiri hapo Lake Nyasa na nilazima tuicheze wenyewe against wamalawi na mabwana zao. Sijui strategists katika medani ya kiusalama na kimkakati wamezingatia hilo. Tuna vikosi Darfur na tutakuwa na vikosi DRC. Adui akiingilia kusini tumekwisha achilia mbali ukanda wa bahari - Al-Shabaab na vibaraka wao. Just for noting.
   
Loading...