singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SERIKALI imekubali kununua asilimia nane ya hisa za kiwanda cha kusafishia mafuta, kitakachojengwa Uganda kwa Dola za Marekani milioni 150, sawa na karibu Sh trilioni tatu. Aidha, inaangalia endapo fedha hizo zitatoka serikalini moja kwa moja au katika sekta binafsi au kwa kushirikiana na sekta hizo ili kununua hisa hizo.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, baada ya kufungua kikao cha kwanza cha majadiliano ya utekelezaji wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga, kilichofanyika Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni, Profesa Muhongo alisema, asilimia 40 ya hisa za kiwanda hicho zitauzwa kwa nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo kila nchi itanunua asilimia nane ya hisa za kampuni hizo.
Alisema ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu Dola za Marekani bil 4.7. Akizungumzia kikao chao, Profesa Muhongo alisema, kilihusisha wataalamu mbalimbali wa nchi hizo mbili ili kuangalia jinsi utekelezaji wa ujenzi wa bomba hilo utakavyofanyika.
“Nimepewa maagizo na Rais, lakini pia mwenzangu amepewa maagizo na Rais wa Uganda kwamba hii kazi ianze haraka na ikiwezekana ikamilike kabla ya wakati uliopangwa,” alisema Profesa Muhongo.
Aidha, alisema kikao cha pili kitafanyika Mei 26, mwaka huu nchini Uganda ili kuhakikisha ujenzi wa bomba hilo unakamilika haraka iwezekanavyo. Naye Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini, Muloni alisema, mradi huo uliogharimu Dola za Marekani bilioni 3.5 una manufaa makubwa kwa watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema wanatambua Tanzania kuna rasilimali nyingine ikiwemo mafuta na gesi, hivyo ni mwanzo mzuri kwani na wao wanaweza kuja kununua gesi kutoka nchini.