Tanzania Kunufaika na Dola Milioni 750 za Marekani Kupitia TradeMark East Africa.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,463
113,518
28/03/2016 Tanzania Kunufaika na Sehemu ya Dola Milioni 750, Kuboresha Biashara

Tanzania itafaidika na mchango wa Dola la Kimarekani Milioni 750, zilizochangwa na Taasisi ya TradeMark East Africa kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa nchi za Afrika ya Mashariki, ambapo sehemu ya maboresho hayo, ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya bandari za Dar es Salaam na Mombasa, ujenzi wa vituo vya pamoja vya forodha katika mipaka ya nchi za Afika Mashariki, na kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki, likiwemo kundi muhimu la wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Trade Mark East Africa, Ali Mfuruki, katika mohojiano maalum na mwandishi wa habai hizi, yaliyofuatia uzinduzi wa Ripoti ya Mwaka ya Taasisi ya Trade Mark East Africa iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mfuruki amesema TradeMark East Africa imefanikiwa kukusanya takiban dola za Marekani $ milioni 750 kutoka kwa nchi washirika wake wa maendeleo ambapo imezitumia fedha hizo katika kuboresha mazingira na miundombinu ya ufanyaji biasharra kwa nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki, ukiwemo ujenzi wa vituo 8 vya ushuru wa pamoja ambapo tayari kituo kimoja na Holili/Taveta kimeishazinduliwa hivyo kuahisisha kuvusha biashara mipakani.
Bw. Mfuruki amesema anafarijika sana kwa jinsi, juhudi za Trade Mark East Africa zinavyoanza kuzaa matunda na kutolea mfano maboresho ya bandari za Mombasa na Dar es Salaam ambapo sasa , inachukua muda wa siku 4 tuu kusafirisha bidhaa kutoka bandari ya Mombasa hadi Kampala wakati zamani ilichukua wiki mbili. Maboesha ya Bandari ya Dar es Salaam yakikamilika, pia itachukua muda mfupi kusafirisha mizigo kupitia bandarri ya Dar es Salaam.
Hata hivyo Mfuruki alisema, kila kwenye mafanikio hapakosi changamoto, ambapo changamoto kubwa ni hali ya kiusalama kwa nchi za Burundi na Sudani ya Kusini, kunapunguza kasi ya kurahisasha biashara katika eneo lote la Afrika Mashariki.
Wakati wa uzinduzi wa Ripoti hiyo ya Mwaka ya TMEA, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, aliyekuwa mgeni rasmi, alisema Serikali ya Tanzania, imedhamiria kupitia upya vikwazo vyote vya kibiashara na tozo zote, ili kuwarahisishia Watanzania, kufanya biashara kwa urahisi zaidi kwa kuchangamkia fursa za soko Nchi za Afrika Mashariki.


Prof. Mkenda, amesema ni jambo la kushangaza sana, kukuta Watanzania wanavutiwa kuuza mazao yao nchi za jirani na kupata bei nzuri zaidi kuliko kuuza kwenye soko la ndani kutokana vikwazo vingi vya kibiashara na mlolongo wa tozo, hivyo lengo la serikali kupitia upya vikwavyo hivyo na tozo, ni ili kurahisisha zaidi kufanya biashara kwa nci za Afrika Mashariki ili kuongeza biashara, mapato, uwekezaji, ajira, na hivyo kuleta maendeleo.
Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Afrika kwa Tanzania, Dr. Josephat Kweka amesema, Trade Mark East Afrika, inajisikia faraja sana, kuwafungulia fursa za kufanyabiashara kwa urais zaidi, wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TradeMark East Africa, Frank Matsaert, ameipongeza Taasisi yake ya TMEA kwa kuwa ni Taasisi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki, nay a pili barani Afrika, kupata cheti cha utambuzi wa kimataifa cha ubora wa huduma za manunuzi, kutoka taasisi ya kimataifa ya Chartered Institute of Procurement & Supply. Matsaert amezishukuru nchi wahisani kuiaminia TMEA na kuifadhili. Nchi hizo ni pamoja na Ubelgiji, Canada, Denmark, Sweden, Finland, Uholanzi, Uingereza na Marekani.
TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani.
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www.www.trademarkea.com












 
Ni hatua nzuri,maana hata mwezi uliopita Kuna Jumuiya Ya Wafanyabishara wa Marekani walikuwa Zanzibar kwa ajili ya Masuala ya Biashara baina ya nchi Mbili.
Watu wa Siasa wameuchuna,maana wanafikiria kila kitu ni MCC tu.

Maisha yataendelea tu kama kawaida.
 
Back
Top Bottom