MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Nijuavyo mimi vyama vyovyote vya siasa duniani lengo lake kuu hasa ni kutoa viongozi watakaoweza kuiongoza ama kuiwakilisha jamaii ili kuipatia mahitaji mbali mbali muhimu hasa huduma za kijamii!
Bila vyama vya kisiasa tusingeweza kupata viongozi wa kuiwakilisha jamii na hatimaye kupata watawala! Vyama ni taasisi ambazo zimekuepo tangu enzi za mababu ispokua kinachobadilika ni mifumo ya kuviendesha kulingana na mazingira na muda.
Sasa kusema kua Tanzania kuna vyama vya hovyo hovyo inamaana hata viongozi wake ni wa hovyo hovyo pamoja na jamii wanazoziwakilisha nazo ni za hovyo hovyo! Jamii flani inapofanya maamuzi kumchagua kiongozi flani kuiwakilisha kukaa pamoja na kuafikiana kumpata kiongozi huyo na sio kwamba kuna mtu hua anaibuka tu na Kujiita kiongozi au mtawala.
Huwezi kujiita kua ni kiongozi makini unayejinasibu kuhudumia wananchi wote bila kujali vyama vya vyao huku unaita vyama vyao ni vya hovyo hovyo! Binafsi sijui maneno haya ni ya kumaanisha, utani wa kisiasa,dharau au makusudi flani lakini yana ujumbe mzito sana na ukakasi usioelezeka.
Nijuavyo mimi hapa ni kwamba chama chochote cha siasa kina uwezo wa kutoa kiongozi makini wa kuliongoza taifa hili ila tofauti ni uwezo wa kihali na mali tu pamoja na umri wa kuanzishwa chama hicho.Hawa hawa viongozi wa CCM, CUF, CHADEMA, NCCR, NLD, ACT nk walisoma shule zinazofanana, wanatoka mazingira tanayofanana japo mawazo yanaweza kutofautiana.
Si vyema sana sisi Waafrika wenye ngozi inayofanana kutupiana maneno au vijembe vya aina hii maana hata wenzetu wa ngozi tofauti na sisi nao wataendeleza dharau zao kwetu kwasababu sisi kwa sisi hatuheshimiani.