Kinachoendelea hapa Tanzania si cha kawaida. Tunaweza tukajiliwaza kwamba tuko kwenye mpito kutoka uzembe na ufisadi ULIOPITILIZA KUELEKEA KWENYE MABADILIKO KAMA WATAWALA WANAVYOTAKA TUAMINI lakini nje ya duara hilo kuna masuali hayana majibu.
Kisiasa hali hairidhishi, ni kama nchi ina ombwe fulani. Na ubaya hapatafutwi dawa mujarabu chuki na vitendo vya kuumbuana na maneno yasio staha yametamalaki. Kumejitokeza matendo ya kurudisha nyuma mustawa wa siasa. Kwa kiasi licha ya kukosa maendeleo mengine kama uchumi imara siasa ilijitahidi na kuvumiliana kulikuwa kukubwa jambo lililoendeleza umoja na mshikamano kama taifa licha ya itikadi tofauti za kisiasa. Kwa sasa hali ni mbaya na siasa imerejeshwa na watawala wenyewe kwa kutumia mkakati wa kuinyima demokrasia ya siasa kufanya kazi. Uhai wa vyama vya siasa ni kufanya siasa na hoja za kisiasa hujibiwa na wanasiasa sio kuziba midomo.(ya bungeni ni mfano.
Kiuchumi hali hairidhishi. Unafuu haujapatikana na maisha yamezidi kuwa ghali sana. Licha ya jitihada za watawala za ahadi na kutaka kupewa muda dalili hazionekani. Watu wa uchumi wana kazi ya ziada kuwafahamisha wananchi wanaoelekea kukata tamaa.
Kijamii, watu wanaanza kufarakana kunakosababishwa na hayo hapo juu ya mifarakano ya siasa na kiuchumi. Nchi inaanza kwa taratibu kuingia katika mifarakano kwa wanajamii. Kipindi hiki cha utawala yote hayo yamekuja kwa kasi mno.
ZANZIBAR.
Ikiwa Tanzania kuna au hakuna Ombwe la Uogozi hilo litajulikana baadae, lakini Zanzibar ni wazi kuna taharuki. Ni taharuki ya kisiasa kutokana na uchaguzi wa 2015 kwa mnasaba wa kile kinachoendelea. Kususiana, kutishana, kupigwa watu na kuvamiwa, kuteswa na kunyanganyana mali ndio mfumo halisi wa maisha ya Zanzibar kwa sasa.
Vyombo vya ulinzi vinaendelea na kutoa majibu yasiotosheleza kila pale panapotokea hujuma.
Hakuna kiongozi anaeguswa kwa udhati ni lini hali itarudi kama awali. Hilo suali halipo na hakuna anaeguswa.
Hii ni taharuki ya wazi. Ni taharuki kwa kuwa haijulikani Zanzibar inakwenda wapi na suluhu ya karibu haionekani. Ni taharuki kwa kuwa viongozi wakuu wa kisiasa wa vyama wamesusiana na kutengana kwa muda sasa, Hakuna Ajenda ya kitaifa kwa sasa ni vijembe na kutupiana mpira kila mmoja akimshutumu mwenzake.
Ni taharuki kwa kuwa hata viongozi wa kijamii na kidini wametofautiana na hawana msimamo wa pamoja kuhusu kinachoendelea Zanzibar kwa sasa.
Tanzania kama nchi inahitaji tujitafakari, Tunakoelekea siko.
Nauliza tu, Tanzania kuna ombwe la Uongozi?