TANZANIA KUNA MAMBO: DPP amkana Hoseah asema hajapata jalada la Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZANIA KUNA MAMBO: DPP amkana Hoseah asema hajapata jalada la Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jul 23, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dk Edward Hoseah, kusema kwamba ofisi yake imekamilisha uchunguzi wa madai ya kumiliki Dola za Marekani 1.2 milioni katika Kisiwa cha Jersey, Uingereza yanayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na kwamba imekabidhi faili lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, kiongozi wake, Eliezer Feleshi amejitokeza na kusema kwamba hawahi kuliona jalada hilo.

  "Niko safarini subiri hadi wiki ijayo… kwanza ashtakiwe kwa kosa gani? Acheni siasa nyie,” alisema DPP alipotakiwa kuthibitisha kama jalada hilo limefika mezani kwake na lini Mwanasheria huyo Mkuu wa zamani wa Serikali atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili... “Aseme ni tarehe gani alileta jalada hilo kwangu?”

  Kutokana na majibu hayo ya DPP, Mwananchi lilimtafuta Dk Hoseah kupata ukweli juu ya kauli yake hiyo aliyoitoa juzi huko Arusha na kusisitiza kuwa jalada hilo limepelekwa katika Ofisi ya DPP na kumtaka mkuu huyo wa Mashitaka nchini asiharakishe kusema hajaliona, kwani siyo lazima kila kitu akabidhiwe mikononi... “Kwani kila kitu kinachopelekwa kwake lazima akione? Ameangalia registry (masjala)?. Suala hili nimeshaliongea nanyi vya kutosha hivyo muulizeni zaidi DPP

  Chanzo. Mwananchi
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Wote wamoja hao DPP, Chenge, Hoseah, Ngereja, na wale waliokuwa wana metetea Ngereja hapa juzi, nilitakusema walionwa na Kampuni ya Execitive Solutions lakini baada ya kugunduwa ni ndugu nikajuwa walisukumwa na ndamu nzito kuliko maji.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Anasema waache siasa ama yeye na Hoseah ndo waache siasa?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,546
  Trophy Points: 280
  Hao ndio watendaji wetu kila mmoja anakurupuka na kutoa kauli yake bila ya kuwa na mawasiliano ya ndani kabla ya kutoa kauli ambazo zinashabihiana. Ndio watendaji ambao hawana maadili katika utendaji wao kila mtu anakurupuka kivyake vyake, wa kulaumiwa hapa si mwingine ila ni bosi wao ambaye kama angekuwa ni mtu makini hizi kauli zinazopingana zisingekuwepo kabisa.

  DPP amkana Hoseah
   
 5. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  DPP wa Tanzania(Director of Public Procurement).
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha ahahaha ahahaha!!!!!!! I knew it!!!!!!!!!!
   
 7. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi ipo.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Procurement au Prosecution???
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Watu mna kazi kweli.. hivi si imewahi kusemwa kuna undugu kati ya Feleshi na Chenge? which automatically should disqualify Feleshi kuona, na kufuatilia hili..
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  This is a clear conflict of interests, and Feleshi should not only see the file but also be consulted for any action against his relative. Chenge alitakiwa kushitakiwa the moment kashfa ilipojitokeza, kujiuzulu pekee hakukutosha. Ila hii yote ni mazala ya kuwa na katiba inayompatia mtu mmoja umungu mtu wa nchi, na Tanzania ya sasa unaweza sema inaongozwa waoga, Kuanzia Mkuu wa nchi mpaka wateule wake.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,076
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]DPP amkana Hoseah
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 22 July 2011 20:27 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  ASEMA HAJAPATA JALADA LA CHENGE, AAMBIWA AKAANGALIE MASJAJA
  Nora Damian
  SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, kusema kwamba ofisi yake imekamilisha uchunguzi wa madai ya kumiliki Dola za Marekani 1.2 milioni katika Kisiwa cha Jersey, Uingereza yanayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na kwamba imekabidhi faili lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, kiongozi wake, Eliezer Feleshi amejitokeza na kusema kwamba hawahi kuliona jalada hilo.

  "Niko safarini subiri hadi wiki ijayo… kwanza ashtakiwe kwa kosa gani? Acheni siasa nyie,” alisema DPP alipotakiwa kuthibitisha kama jalada hilo limefika mezani kwake na lini Mwanasheria huyo Mkuu wa zamani wa Serikali atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili... “Aseme ni tarehe gani alileta jalada hilo kwangu?”

  Kutokana na majibu hayo ya DPP, Mwananchi lilimtafuta Dk Hoseah kupata ukweli juu ya kauli yake hiyo aliyoitoa juzi huko Arusha na kusisitiza kuwa jalada hilo limepelekwa katika Ofisi ya DPP na kumtaka mkuu huyo wa Mashitaka nchini asiharakishe kusema hajaliona, kwani siyo lazima kila kitu akabidhiwe mikononi... “Kwani kila kitu kinachopelekwa kwake lazima akione? Ameangalia registry (masjala)?. Suala hili nimeshaliongea nanyi vya kutosha hivyo muulizeni zaidi DPP.”

  Juzi, Dk Hoseah alisema taasisi yake imekamilisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Chenge na kwamba jalada lake limepelekwa kwa DPP kwa hatua zaidi. Alisema Chenge atashtakiwa chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akiwa na mali ambazo hazilingani na kipato chake alichokipata akiwa madarakani au baada ya kuondoka ni kosa kisheria.

  Chenge anadaiwa kukutwa na kiasi hicho cha fedha mwaka 2008 baada ya uchunguzi wa kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO). Tuhuma hizo ndizo zilizomfanya alazimike kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu mwaka huo.

  Malumbano kati ya Dk Hoseah na Feleshi siyo ya kwanza. Mwaka jana waliwahi kulumbana baada ya mkuu huyo wa Takukuru kusema kuna majalada takriban 50 ya kesi za rushwa ambayo yamekaliwa na DPP.

  Pia Dk Hoseah aliwahi kumshutumu DPP mbele ya wabunge wakati wa semina elekezi mapema mwaka huu akidai kwamba amekuwa kikwazo cha kesi kubwa za ufisadi kupelekwa mahakamani kwa kukwamisha majalada.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,076
  Trophy Points: 280

  kiburi cha DPP kinatoka kwa yule aliyemteua.................................JK.........................ndiye kamweka pale alinde mafisadi.........................na ndiyo maana wanapokabiliwa na kesi za ufisadi DPP hukimbilia kusema ni siasa............................we really need constitutional reforms where the House will have a final say on presidential appointments........................
   
 13. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  DPP before alikuwa mwanasheria Kanda ya Ziwa, Chenge akampigia debe kwa jk pia ni ndugu ,hamna kitu hapo .
   
 14. m

  mhondo JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Na DPP akisema hakuna ushahidi ndiyo kesi imekwisha hakuna kwa kukata rufaa au kupeleka malalamiko tena.
   
 15. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Haya sasa hii ndio Tanzania bhana.Tz inaleta BP mimi binafsi nataka kuihama kwani nikiendelea kuishi hapa nitakuja kuua mtu.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi huyu DPP anapokurupuka kuwa "Chenge ashtakiwe kwa kosa gani, acheni siasa," hata kabla ya kuliona Jalada husika, mbona ananipa wasiwasi sana kuhusu kutenda haki? Ingekuwa heri akasema tu kwamba bado hajaona Jalada na akiliona ataamua! Anyway, ngoja tuangalie movie hii ambayo ndio kwanza ipo kwenye trela!
   
 17. K

  Kaseko Senior Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hosea mwenyewe mtu wa bariadi itakuwa ngumu sana.
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hoseah si wa Bariadi, ni Maswa!
   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Uh! Watu mnajua kufuatilia. Hapo kwenye red; the four guys have at least three things in common:

  (i) They are all SUKUMAS
  (ii) They are all LAWYERS
  (iii) They are all SENIOR OFFICERS
  (iv) They are all CHRISTIANS
  (v) They are all MALES

  Kwa dini yenu, hebu mwogopeni Mungu na muache kuliaibisha Jina la BWANA kwa malumbano na utendaji usio na tija kwa taifa. Mnamwaibisha Mh. Rais aliyewateua na hata kuziaibisha taaluma zenu - SHERIA. Mnaaibisha wafanyakazi wa Serikali na hata wanaume mnawatia aibu.
   
 20. zeus

  zeus JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hii movie itakuwa ya ajabu na based on true story......si umeona trela inavyosisismua??? beliieve me kutakuwa na viini macho!!! the good thing ni kwamba katika hili hakuna neutrality ni kusuka au kunyoa, kushtaki au la na historia itawahukumu.
   
Loading...