Tanzania kuna kabila linaitwa Waarusha au ni Wamasai mmeamua kujiita hivyo?

Waarusha kiasili wanaitwa Larusa, neno la kimasai ikiwa na maana ya watu wanaoishi Rusa ambayo waswahili wakaita Arusha
Olarusai mwanaume wa kiarusha
Engarusai ni mwanamke wa kiarusha
 
Nijuavyo mimi, waarusha ni mazezeta wasiopenda kazi, wao hawalimi, si wafugaji, hawana issue yeyote ila wapo wapo tu. Mambo yakiwa magumu kwao wanauza viwanja vyao kwa wageni na kwenda kuishi maporini.
 
Waarusha ni wamasai, ila wao wamepunguza ukali wa Mila za Kimasai.

Unaweza sema ni wamasai walioachana na Mila zao na kuchukua mambo ya mjini. Makazi Yao ni Arusha Mjini. (Manispaa ya Arusha)
Na ndio ipo hivyo mkuu
 
Waarusha na Masai ni makabila mawili tofauti, waarusha ni wenyeji wa Arusha mjini, wao ndio wameuza maeneo yao ya maboma kwa wengine (wahamiaji) waliopo Arusha, ila nao wakati mwingine hujifunika mashuka kama wamasai.
Nitajie tofauti tatu Kati ya wamasai dhidi ya waarusha,nje ya geographical location.
 
Mm mwenyewe Ni muarusha ingawa nikibanwa snaa najita mmasai ingawa wazazi wangu wote Ni waarusha mam na Bab na babu na bib ..nazungumza kilugha Cha kiarusha na CYO kimasai pure ingawa nazungumza lugha zote ila kimasai sikipati chote chote ..ila naweza kuimba na kwa kilugha nyimbo za dini hususan kitabu maarufu Cha mwimbieni bwana au kwa kilugha sinkoloitini le ngai
 
Waarusha ni wamasai, ila wao wamepunguza ukali wa Mila za Kimasai.

Unaweza sema ni wamasai walioachana na Mila zao na kuchukua mambo ya mjini. Makazi Yao ni Arusha Mjini. (Manispaa ya Arusha)
Manispaa ya Arusha ni ile west Meru, Arusha mjini ni Halmashauri ya Jiji la Arusha more than 7 years ago
 
Acha uongo ndg
mimi ni Mwarusha
Kabila la kiarusha ni kabila dogo lililomeguka kutoka kwa wamasai sio kabisa, wala halikumevuka kiuhasama
tumetofautishwa na wamasai kwenye mambo machache sana
kwanza ni occupation, wamasai ni wafugaji 100% wakati waarusha ni wakulima na wachache wao wanafuga na kulima
Pili wamasai na waarusha tunatofautiana kwenye jando na baadhi ya mila zile za ndani sana
Tunafanana kwenye lugha, rika, koo nk
Kwa jinsi tunavyoushi ni kabila mbili ndani ya moja ndio maana watu wengine wanashindwa kutofautisha. Hakina uhasama wowote kati ya wamasai na waarusha. Infact wakati wa tohara na mambo mengi ya kimila malaiguanani wa pande zote mbili hukaa pamoja hadi wale wa Kenya na sehemu mbalim ali Tanzania kwenye mlima mmoja uko maeneo ya west Kilimanjaro nafikiri maeneo ya Hai au jirani kupitisha maamuzi ya pamoja. mfano tohara ianze lini na rika hilo liitweje. nk
Kabila hili linasadikika kutokea au kumeguka kutoka kabila mama la wamasai miaka ya mwanzoni mwa 1900 au mwishoni mwa 1800
Wamasai waliokuwa wanauza madawa na kufanua biashara ya minada walikuwa wakipita arusha na kifanya kiwa ni kituo cha kupumzikia. kwa sababu ilikuwa ni paradiso ya kweli muda ulivyosonga kidogokidogo wakaamua kusetle na kufanya makazi ya kudumu wakaanza kuzaliana na kufanya shighuli za ufugani na kilimo ndipo kabila la Waarusha au Larusa likatokea
tupo pamoja tena sana. hivyo ndg acha kupotosha mambo usiyoyajua
nlikuja Arusha vijana wengi kule walinishauri nisioe wake wa Kiarusha ...hii ni kwa sababu gani?
 
nlikuja Arusha vijana wengi kule walinishauri nisioe wake wa Kiarusha ...hii ni kwa sababu gani?
Walikushauri vibaya, kwa dunia ya leo mtu anayezungumzia makabila na ukabila amepungukiwa na vitu vingi muhimu. Uzuri wa mke au ubovu wake hauko kwenye kabila kwani kiukweli hata makabila yenyewe hayaexists kwa dunia ya leo hasa mijini, labda vijijini
  1. Malezi
  2. Company
  3. Exposure
  4. Akili ya mtu mwenyewe na
  5. Mungu au shetani anayemuongoza
 
Mambo mengine mnamsingizia tu shetani.
What you make of your life is up to you. You have all the tools and resources you need. Your answer lie inside of you
 
Mambo mengine mnamsingizia tu shetani.
What you make of your life is up to you. You have all the tools and resources you need. Your answer lie inside of you
Wewe nawe mgumu kuelewa lugha za wakubwa. Hata kama huna dini, kila mtu ana Mungu na Shetani wake anayemuongoza. Kama huelewi acha hivyo hivyo
 
Hakuna kabila la waarusha, Hawa ni wamasai walioasi kwa kuona aibu ya kuitwa Masai. Waliona aibu kutoboa masikio na Mila zingine za kimasai wakajiita Masai wa Arusha baaadae wajiita waarusha.

Wanaugomvi mkubwa Sana na wamasai kwa sababu wao wanafanya kila kitu sawa na wamasai isipokuwa kutoboa masikio.

Mwingiliano mkubwa na wameru imefanya lafudhi zao kubadilika kidogo
Inaelekea Historia imewapiga watu chenga.

Mbona kwenye Maandiko ya Wamisionari wa Kizungu kabila la Waarusha limetajwa?

Wazungu walipofika Arusha kwa mara ya kwanza, waliyakuta hayo makabila Arusha: Wamasai, Waarusha, Wameru.

Arusha imetokana na uwepo wa kabila la Waarusha. Ni kama vile baadhi ya mitaa ya Dar Es Salaam kama kwa Msuguri, Kwa Azizi Ally, n.k., au baadhi ya mitaa ya Arusha kama vile Kwa Ngulelo, Kwa Mrefu, n.k.
 
Hakuna kabila la Waarusha, these Molles's ni wamasai wa mjini.
Arusha ni Wameru wanaokaa ardhi ya Rutuba na wamasai.
 
Back
Top Bottom