Tanzania kuna kabila linaitwa Waarusha au ni Wamasai mmeamua kujiita hivyo?

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,549
6,097
Wakuu nipo sehemu fulani hapa kuna vijana wanajaza fomu fulani hivi mimi nikiwa kama msimamizi wa hili zoezi kuna jambo linanitatiza hapa kidogo.

Katikati hizo fomu kuna kipengele cha kujaza kabila lako sasa vijana wengi kutoka Mkoa wa Arusha katika hiki kipengele wanajaza kabila lao MUARUSHA.

Hapa nabaki najiuliza mbona hili Kabila sijawahi kulisikia na hata katika ile list yetu ya mkeka wa makabila zaidi ya 120 sijawahi kuona hili kabila?

Pembeni yangu kuna vijana wameniambia hilo kabira ila nawasikia wanaongea KIMASAI. Najiuliza au ndugu zetu WAMASAI mmeamua ku edit jina la kabila lenu kutoka MAASAI na kuwa WAARUSHA?

Kama ni hivyo kwani nyie ndugu zetu hamuijui LEGACY ambayo kila Siku MATAGA wanaihubiri humu ndani? Naomba tusipoteze LEGACY.
 
Ni makabila mawili tofauti, tena mahasimu kweli kweli.

Hawapendani hata kidogo. Hata kuoana hawaoani

Makabila Mengi ya kaskazini yanafanana mambo mengi sana, kuna tofauti ndogo ndogo sana.
 
Waarusha na Masai ni makabila mawili tofauti, waarusha ni wenyeji wa Arusha mjini, wao ndio wameuza maeneo yao ya maboma kwa wengine (wahamiaji) waliopo Arusha, ila nao wakati mwingine hujifunika mashuka kama wamasai.
Waarusha ni kabila linaloshabihiana na wamasai Wana asili ya upareni na walikuwa vijakazi wa wamasai ila Waka adopt lugha na tanaduni za kimasai wanakaa Arusha mjini.
N. B hii story nilisimuliwa na Babu wa kimasai.
Ni makabila mawili tofauti, tena mahasimu kweli kweli.

Hawapendani hata kidogo. Hata kuoana hawaoani

Makabila Mengi ya kaskazini yanafanana mambo mengi sana, kuna tofauti ndogo ndogo sana.
Ni kabila tofauti ambao ni ndio watu wa Arusha asilia kabla ya jiji lao kuporwa na wachagga.
Mbona katika list ya makabila 121 yanayo patikana Tanzania hili kabila halipo wakuu?

Na mbona wanaongea kimasai tu au na wenyewe wana lugha yao ya kiarusha?
 
Back
Top Bottom