Tanzania kuna amani au ni msemo tu uliozoeleka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania kuna amani au ni msemo tu uliozoeleka?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Somi, Sep 30, 2010.

 1. S

  Somi JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kutafakari matukio ya ujambazi yanayotokea kila kukicha na kujiuliza hivi kweli tanzania kuna amani au ni wanasiasa wetu wamezoea kutumia huo msemo kuzidi kujipatia kila wanachotaka.
  Ukienda mwanza na basi lazima upewe eskoti ya polisi hali kadhalika hivyo hivyo na kigoma na kagera.
  Arusha nako ndio hivyo tena kila siku risasi zinalia, ukija daessalaam napo hapako nyuma kwa matukio ya ujambazi kila kukicha kwenye mabenki, mabaa, majumbani n.k.

  Juzi juzi tena nikasikia majambazi yameteka magari yote yanayotumia bara bara ya iringa maeneo ya kati kati ya morogoro na mikumi bila woga na kupora watu mali zao.

  Tunduma nasikia watu wakijua una mali basi ndio umekwisha kama huna ulinzi wa kutosha
  juzi nikasoma kwenye gazeti la uwazi majambazi walivamia kanisani kwa mchungaji anthony lusekelo ubungo wakaiba ela ingawa sijadhibitisha kama hii habari ni ya kweli au uongo

  kwa ujumla nchi nzima haipo salama kwa matukio ya ujambazi
  hali yote hii inasababishwa na hali ya umasikini kuzidi huku watu wachache wakizidi kuwa matajiri katika nchi hii masikini na hii kupelekea matabaka ya walionacho na wasio nacho inayosababishwa na wizi na ufisadi unaofanywa na mafisadi vidagaa mpaka mapapa

  kuhitimisha kama hii hali ya uchumi haitarekebishwa tanzania inaweza kuwa kama nigeria au south africa
   
Loading...