Tanzania Kumepambazuka: Kikwete Kwaheri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Kumepambazuka: Kikwete Kwaheri!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by RMA, Oct 26, 2010.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :rain:Karibu Rais wetu Dr Slaa! [​IMG]:director:


  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!:rain:


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..:loco:


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? :director::wink2:


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious! :alien::director: :hat:


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?:rain::spider:


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :wink2: :bolt:


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.


  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..:bolt::loco:

  [FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]​
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kimsingi kumekucha, atoke, turekebishe nchi yetu.:israel:
   
 3. M

  Mikomangwa Senior Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania amkeni kumekucha, jua limechomoza kuashiria siku mpya, maisha mapya, matumaini mapya? Maskini watanzania, mbona mnaogopa mabadiliko?
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakika Mungu anawapenda watu wake. Hatimaye nchi inaondoka kwenye minyororo ya ufisadi wa kutisha. Kweli Mungu mkubwa.
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Tatizo langu kubwa ni kuwa siwaamini kabisa CCM................!!!
   
 6. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Too late, tarehe 4 kikwete anaapishwa tena,sorry


  Kila la kheri;Maki-lafi
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo, umenena...umesema kila ambalo CCM hawataki kulisikia popote linasemwa....

  Tunarudia tena maneno ya busara ya Dr Slaa..."Watanzania Kuichagua tena CCM ni Maafa"

  Wote tuseme SASA BASI, TUMECHOKA, MABADILIKO LAZIMA; RAIS TOKA CHAMA MAKINI NDIO JIBU!
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hofu yangu wakituibia kura. Jamani tuzidishe maombi.
   
 9. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mimi nitasikitika saana kama CCM watachukua tena nchi hii.

  Naamini kama itakuwa hivyo basi watakuwa aidha wamechakachua kura Watanzania tulio wengi ni mbumbumbu wa Siasa na hawajui nani hasa anaweza kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo na ufanisi wa maisha yao.

  Kama kweli JK huyu huyu mwongo ambaye Kampeni zenyewe anafanyiwa na Mkewe Salma na mwanae Ridhiwani atarudi Ikulu basi Watanzania hatujui maana ya DEMOKRASIA,UONGOZI BORA NA SIASA SAFI.

  Kwa kifupi itakuwa ni kuitakia nchi hii LAANA YA KARNE YA 21.

  KURA YANGU NAMPA MBOWE kama RAIS, MBUNGE wa CHADEMA, na DIWANI WA CHADEMA.
  Sidanganyiki nasema.
   
 10. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  4 days remain for jk trial version, database are not available n access denied
   
 11. L

  Limbwata Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hee! Hivi leo ni tarehe ngapi???

  Kura zimeshapigwa jamani??? Mama yangu weee mi nilikuwa wapi???

  Slaa kashinda uchaguzi????

  Mh ndoto hii isipotimia, sijui nyuso zitafichwa wapi kwa kweli!!!!
   
 12. T

  The King JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn:
  :violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin:
  :horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn::horn:
  :violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin::violin:
  :peace::peace::peace::peace::peace::peace::peace::peace::peace::peace:

  Karibu Rais wetu Mtarajiwa Dr Slaa utuongoze Watanzania
   
 13. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kabla ya pambazuko jipya unaposema nisichague chama bali mtu wakati wa kupiga kura ina maana gani. Kwamba nimchague Kikwete na nisichague CCM? au nimchague Slaa au Mnyika na sio chadema. Kuna kura zinataka kupotea kwa namna hii.
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,462
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  ''I will miss the Gulfstream G55....and per diems'' says JK
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,462
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 16. General

  General Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mbowe hagombei Urais
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwaheri CCM karibu CHADEMA
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Hapa umefunga kazi kabisaaaaaaaaaaaaa.........................na asiyesikia la mkuu huvunjika guu...........................
   
 19. K

  King kingo JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanini watuibie???? TUSIKUBALI KUIBIWA
   
Loading...