Tanzania kukopa trilioni 2.1 kutekeleza bajeti ya 2016/17

dos santos

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
252
250
Serikali ya Tanzania iko kwenye mazungumzo na taasisi za kifedha ambazo zinakopesha ili iweze kuikopesha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema hali hiyo inatokana na kuwepo kwa masharti magumu yanayowekwa na taasisi za kifedha za nje pamoja na nchi wahisani ambazo zimekuwa zinaikopesha serikali katika kutekeleza bajeti yake yake katika miezi mitano ya kuanza kutumika kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Pia Serikali imesema kwamba ina matumaini kwamba hivi karibuni itakamilisha mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa lengo la kupata mkopo wenye masharti nafuu.

Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo ya kibiashara ya Sh trilioni 2.1 kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, lakini kutokana na masharti magumu ikiwemo riba kubwa haikuweza kufanya hivyo.

Dk Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Kuwait, Abu Dhabi na Jumuiya ya nchi zinazouza mafuta kwa wingi (Opec).

source:shirika la habari la china Tanzania: Serikali ya Tanzania yapanga kukopa Sh trilioni 2.1 - china radio international
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,468
2,000
Ukishangaa ya Nyati utayaona ya Faru John!!!

Pale tuliposema hii nchi bado sana kwahiyo mikopo na misaada haikwepeki; tulikejeliwa na kuelezwa ni jinsi gani serikali ya sasa ilivyo na uwezo wa kujiendesha yenyewe!!!

Hata tuliposema kwa hapa tulipo, mosi hatuna hata ubavu wa kukusanya hata Trillion 1.5 kwa mwezi at least for the next 3 years LAKINI hata kama tutakuwa na ubavu wa kukusanya Trillion 2 kwa mwezi; bado misaada na mikopo haikwepeki... wale wanaoishi kwenye dunia ya kufikirika; waliendelea kukejeli!!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,458
2,000
Hivi kipi bora; kukataa zile hela za bure za MCC na wafadhili wengine au kwenda kukopa? Labda mimi sielewi! Kwa mtindo huu si deni la taifa litapaa kwa kasi ya mwanga wajameni?

======= UPDATES ======

ukweli utabaki kuwa ukweli kwamba Serikali imekosea sana kwenye swala la kuweka kodi za VAT kwenye bandari uku wenzetu kwenye nchi za kenya na mozambique kutoweka tozo hiyo. ....
Hii issue ya VAT isipoangaliwa itaua uchumi. Nilikuwa nawaza, kwa mfano kwa mlaji aliyeko huko pembezoni mwa nchi na ambaye ili bidhaa imfikie itapitia kwa wafanyabiashara watatu at minimum; yaani mwagizaji kutoka nje (mfanyabiashara 1 - MB1), whole seller jirani na alipo mlaji (MB2), muuza rejareja kwa mlaji (MB3). Hapo katikati pia kuna m/wasafirishaji au transporters angalau wawili - kutoka bandarini/DAR hadi kwenda kwa MB2 (T1); kutoka MB2 kwenda MB3 (T2); kutoka MB3 kwenda kwa mlaji (T3).

Kama thamani ya mzigo kutoka nje ni TZS/USD X kwa mfano, ina maana VAT, bila kuhusisha VAT kwenye usafiri wa ndani (assume hauna VAT to minimize computation complications) inakokotelewa hivi (I think):

1. On entry (bandarini): 0.18X
2. From MB1 to MB2: 0.18 (X + 0.18X)
3. From MB2 to MB3: 0.18 (X + (0.18(X + 0.18X)))
4. From MB3 to Mlaji: 0.18 (X + 0.18 (X + (0.18(X + 0.18X))))

Hii ina maana mlaji wa mwisho VAT atakayolipa bila usafiri ni: 0.18X + 0.18 (X + 0.18X) + 0.18 (X + (0.18(X + 0.18X))) + 0.18 (X + 0.18 (X + (0.18(X + 0.18X))))

Dah! Ha ha ha! hii ni "cascading" ya hatari! Kazi ipo.
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,555
2,000
Serikali ya Tanzania iko kwenye mazungumzo na taasisi za kifedha ambazo zinakopesha ili iweze kuikopesha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema hali hiyo inatokana na kuwepo kwa masharti magumu yanayowekwa na taasisi za kifedha za nje pamoja na nchi wahisani ambazo zimekuwa zinaikopesha serikali katika kutekeleza bajeti yake yake katika miezi mitano ya kuanza kutumika kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Pia Serikali imesema kwamba ina matumaini kwamba hivi karibuni itakamilisha mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa lengo la kupata mkopo wenye masharti nafuu.

Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo ya kibiashara ya Sh trilioni 2.1 kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, lakini kutokana na masharti magumu ikiwemo riba kubwa haikuweza kufanya hivyo.

Dk Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Kuwait, Abu Dhabi na Jumuiya ya nchi zinazouza mafuta kwa wingi (Opec).

source:shirika la habari la china Tanzania: Serikali ya Tanzania yapanga kukopa Sh trilioni 2.1 - china radio international
Unapopewa Masharti magumu na wakopeshaji ina maana kuwa hukopesheki
 
Ongata

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
525
1,000
Ccm watueleze vizuri kwanini wanataka kukopa wakati walituambia wamepata serikali inayokusanya kodi,imedhibiti watumishi hewa,uzembe kazini,wamepunguza safari za nje,wamejenga viwanda,wamepunguza kuwapa mkopo wanafunzi wa vyuo vikuu,.....hivi kuna barabara inajengwa kweli Kama uyoga Kama enzi za Kikwete na Mkapa au ni maneno tu,sisi wengine tuko vijijini mtujulishe
 
Ukback255

Senior Member
Aug 31, 2016
175
500
Nchi imefirisika kodi hakuna,watalii hakuna kwa sababu ya kuingia mkenge wa VAT .
Mpaka sasa Serikali imeshakopa zaidi ya trion 17 ndani ya mwaka mmoja
Sasa inataka tena kukopa tri 2

Nilikuwa na Google map view ya bandari ya Dar ni kichekesho hakuna hata meli

Naomba tu Mungu saidia wasikope kununua ndege
 
mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,381
2,000
Madhara ya kujifanya tynaweza wakati bado! Jpm alidhani nchi inaongozwa kwa matamko na mihemko! Eti hatuhitaji misaada, kiko wapi sasa? Kutumbua kote huko bado hali ni mbaya kuliko hata ilivyokuwa serikali iliyopita! Sad!
 
Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Nahitaji kufahamu hiyo mikopo inatumika kununulia nn au ndege kubwa zaidi. ?..Ama kweli anainyoosha nchi. ..
 
NAKEMBETWA

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
3,523
2,000
Hii serikale si Mdaiwa Sugu ?

Lile deni la Taifa limefikia Trillion ngapi vile?
 
e nkwasi

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
384
500
Walikua wanatoa matamshi ya kukurupuka tu 'nchi hii ni tajiri sana sio ya kutegemea misaada na kukopa kopa'. Sasa wanakula matapishi yao, ni ulaghai mtupu. Tunakoenda ndio kubaya zaidi coz hata pato la ndani (GDP) litazidi kupungua kwa sababu ya kuzorota kwa shughuli za kiuchumi. Serikali iache 'kiburi' , iridishe pesa kwenye mzunguko through Investment and
Commercial banks under certain conditions.
 
RockSpider

JF-Expert Member
Feb 16, 2014
6,866
1,500
Serikali haifanyi biashara ila inakopa mkopo wa Kibiashara ...
Serikali ya Tanzania iko kwenye mazungumzo na taasisi za kifedha ambazo zinakopesha ili iweze kuikopesha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema hali hiyo inatokana na kuwepo kwa masharti magumu yanayowekwa na taasisi za kifedha za nje pamoja na nchi wahisani ambazo zimekuwa zinaikopesha serikali katika kutekeleza bajeti yake yake katika miezi mitano ya kuanza kutumika kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha.

Pia Serikali imesema kwamba ina matumaini kwamba hivi karibuni itakamilisha mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa lengo la kupata mkopo wenye masharti nafuu.

Alisema Serikali ilitarajia kukopa mikopo ya kibiashara ya Sh trilioni 2.1 kutoka kwa taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali, lakini kutokana na masharti magumu ikiwemo riba kubwa haikuweza kufanya hivyo.

Dk Mpango aliongeza kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Kuwait, Abu Dhabi na Jumuiya ya nchi zinazouza mafuta kwa wingi (Opec).

source:shirika la habari la china Tanzania: Serikali ya Tanzania yapanga kukopa Sh trilioni 2.1 - china radio international
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom