MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Mapambano ya Tanzania na Kenya kiuchumi yamepamba moto huku Rwanda na Uganda zikichochea moto.
Makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda yaliipokonya Kenya ajira na pesa kwa sababu awali serikali za Uganda na Kenya zilikubaliana kupitisha bomba hilo katika ardhi ya Kenya.
Tanzania kukataa kuweka saini makubaliano yanayoitwa EAC-EU Economic Partnership Agreements(EPA) kwa upande mwingine yanaifanya Kenya kuanza kulipa kodi kati ya asilimia 8 mpaka asilimia 12 kwenye uuzaji bidhaa zake kwenye masoko ya EU(Export).
Makubaliano ya EAC-EU Economic Partnership Agreements(EPA) ili yakubalike yanahitaji ridhaa ya nchi zote za EAC. Utiaji wa saini ulikuwa ufanyike wiki ya kwanza ya mwezi August 2016.
Ikumbukwe Kenya kwa sasa inapata zaidi ya €25 billion (KSh3 trillion) kwa mwaka kutokana na mauzo ya bidhaa katika soko la EU. Kujiondoa kwa Tanzania kutaifanya Kenya kulipa kodi inayokadiriwa kuwa zaidi ya Ksh 8 billion kwa mwaka.
Mbaya zaidi kuanzia tarehe 1, Januari 2017, Kenya itaondolewa katika kundi la nchi zilizo kwenye mpango unaitwa EU’s Generalised Scheme of Preferences (GSPs) ambao unahusu bidhaa za floriculture na live plants na hivyo kutakiwa kulipa kodi zaidi za bidhaa hizo.
Chini ya protokali za kibiashara katika soko la Umoja wa Ulaya, kundi la Nchi Masikini Zaidi Duniani (The Least Developed Countries - LCD) hazitozwi kodi kwa kuingiza bidhaa zake katika soko la Umoja wa Ulaya. Tanzania ni mojawapo ya Nchi Masikini Zaidi Duniani wakati Kenya haipo katika kundi la Nchi Masikini Zaidi Duniani.
Kwa maana nyingine, Tanzania haina faida yoyote ya kuweka saini kwenye makubaliano ya EPA kwa sasa wakati kilichoko kwenye makubalino hayo kwa sasa inakipata kupitia kundi la Nchi Masikini Zaidi Duniani wakati huo huo inakuwa na uhuru kisheria wa kuweka kodi za Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import) ili kulinda bidhaa zake za ndani.
Nini mwisho wa mapambano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya ambayo yanachagizwa na mazingira.