Tanzania kuingia Uchumi wa Kati maana yake nini?

kama hivi ni vigezo basi litakua ni timba LA karne
Mkuu watu wanashangilia wanahusisha na Maisha yao binafsi wakidhani pesa ipo mifukoni mwao. Hili jambo hasa hii miradi mikubwa italeta mrejesho baada ya miaka kadhaa. Hapo ndipo mabadiliko kidogo yataonekana kwa watu.
 
Watanzania wengi wanashangilia hasa wanasiasa sidhani kama wanaelewa maana halisi ya uchumi wa kati kwa hivi vipimo vya GNI vya Benki ya Dunia na IMF
Hapa ndipo kama tungekuwa na vyama vya upinzani vyenye viongozi komavu na uelewa mzuri wa haya mambo, wangeyaelezea vizuri na kwa lugha rahisi ili wananchi waelewe maana yake.

Lipumba ni mpinzani, tena mchumi. Ni lini umemsikia akizungumzia haya mambo kwa wananchi waelewe!

CCM watatumia nafasi ya ombwe hilo kujisifu na kuhadaa wananchi.

Nilipokuwa nikisoma uliyoweka hapo kwenye mada yako hii, nikawa nawaza Rais Magufuli na maburungutu yake anayogawa huko mitaani mara kwa mara. Nikatafuta ni wapi tunaweza kupachika hayo kuwa sehemu ya ongezeko la pato. Sikupaona! Eeeeenh Heee!

Mkuu 'GUSSIE' umefanya kazi nzuri hapa. Hii ni aina ya michango ambayo wakuu wa JF wanatakiwa wawe wanaipa 'utambuzi' maalum kwa sabau inaongeza thamani ya jukwaa.

Hongera sana.
 
Mambo ni race mnoo...yaani tumeingia kwenye uchumi wa Kati wenyewe kitaa Hatuna habari mpaka tumekumbushwa....
 
Kuhusu Tanzania Kuingia Uchumi wa Kati, Prof Ngowi Mchumi amefafanua vizuri Sana hata mm layman wa Uchumi nimeweza kuelewa. Mambo ya Msingi hapa Ni kwamba:

1. Tunaposema tumeingia Uchumi wa Kati tunachukua Pato la WATANZANIA wote tunatafuta wastani. Maana yake Pato langu linajumlishwa na la kina Mo au Pato la msukuma toroli pale soko la Tandale linajumlishwa na Pato la kina Bakharesa halafu wanatafuta wastani. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo wastani wa Pato la kila mtanzania kwa Sasa linaanzia milioni mbili Hadi milioni nne.

2. Ukiingia Uchumi wa Kati maana yake unaanza kuachana na Misaada mfano tuna miradi mingi Sana tunayofadhiliwa Kama nchi kwenye Afya, Elimu nk hii tuanze kufikiria muda si mrefu haitafadhikiwa tena, Bajeti yako ya ndani kwa asilimia kubwa inatakiwa ibebwe na Pato la ndani, Mahali ambapo ulikuwa ukikopa wanakupa kwa riba ndogo Sasa riba itakuwa kubwa nk. Kwa maana ya Prof Ngowi ni kuwa mtoto kakua anapaswa kujitegemea Mwenyewe.

3. Wananchi waelimishwe wajiandae na mazingira ya Kuingia Uchumi wa Kati kuwa Ni kuzidisha kufanya kazi kwa bidii sio kupumzika, wengi wanaoshangilia wanadhani Ni muda wa kula Bata kumbe Ni kinyume chake kuwa ni wakati wa kupambana haswa kuelekea kujitegemea.

4. Kuna wanaosema World Bank imetutega kutuongoza Uchumi wa Kati ili wapate kutubagaza kwa kutunyima mikopo ya masharti nafuu na kukosa misaada kwa maana ya kutakiwa kujitegemea. Wenye nadharia hii wanadai kuwa nchi kama nchi ilikuwa haijafikia kuingia kwenye Uchumi wa Kati Bali ni Janja ya Mabeberu kutubagaza. Hili wewe unalionaje?

5. Kuna ambao wanafurahia kuwa nchi Sasa imepiga hatua kwa maana ya kuelekea kujitegemea. Hili wewe unalionaje? ....
Msikilize Prof Ngowi
 
Attachments

  • Thadei.mp4
    10.1 MB
Kwa jinsi tulivyopigika,mimi naungana na wanaotoa hoja namba 4, tumetegwa!! 😊 halafu tunafurahiiii wenyewe kwa raha zetu😀😀😀

NB: nashangaa kwa nini baba na mwana hata hawajatuambia tutenge hii weekend kwa kushangweka.
 
Kuhusu Tanzania Kuingia Uchumi wa Kati, Prof Ngowi Mchumi amefafanua vizuri Sana hata mm layman wa Uchumi nimeweza kuelewa. Mambo ya Msingi hapa Ni kwamba
1. Tunaposema tumeingia Uchumi wa Kati tunachukua Pato la WATANZANIA wote tunatafuta wastani. Maana yake Pato langu linajumlishwa na la kina Mo au Pato la msukuma toroli pale soko la Tandale linajumlishwa na Pato la kina Bakharesa halafu wanatafuta wastani. Kwa hiyo kwa kufanya hivyo wastani wa Pato la kila mtanzania kwa Sasa linaanzia milioni mbili Hadi milioni nne.

2. Ukiingia Uchumi wa Kati maana yake unaanza kuachana na Misaada mfano tuna miradi mingi Sana tunayofadhiliwa Kama nchi kwenye Afya, Elimu nk hii tuanze kufikiria muda si mrefu haitafadhikiwa tena, Bajeti yako ya ndani kwa asilimia kubwa inatakiwa ibebwe na Pato la ndani, Mahali ambapo ulikuwa ukikopa wanakupa kwa riba ndogo Sasa riba itakuwa kubwa nk. Kwa maana ya Prof Ngowi ni kuwa mtoto kakua anapaswa kujitegemea Mwenyewe.

3. Wananchi waelimishwe wajiandae na mazingira ya Kuingia Uchumi wa Kati kuwa Ni kuzidisha kufanya kazi kwa bidii sio kupumzika, wengi wanaoshangilia wanadhani Ni muda wa kula Bata kumbe Ni kinyume chake kuwa ni wakati wa kupambana haswa kuelekea kujitegemea.

4. Kuna wanaosema World Bank imetutega kutuongoza Uchumi wa Kati ili wapate kutubagaza kwa kutunyima mikopo ya masharti nafuu na kukosa misaada kwa maana ya kutakiwa kujitegemea. Wenye nadharia hii wanadai kuwa nchi kama nchi ilikuwa haijafikia kuingia kwenye Uchumi wa Kati Bali ni Janja ya Mabeberu kutubagaza. Hili wewe unalionaje?

5. Kuna ambao wanafurahia kuwa nchi Sasa imepiga hatua kwa maana ya kuelekea kujitegemea. Hili wewe unalionaje? ....
Msikilize Prof Ngowi
Suala kubwa ni hiyo mradi mikubwa ilio tuinua na kua na GDP kubwa, ni miradi ambaye aijakamilika pia ni yamikopo....nasidhani kama itakamalika kwa 100% kwa miaka 5 injao.....JPM hajui 'political economy' kadaganywa na akakubali, bepari hawezi kukupa promotion bila mtego mkuu kaingia mtego wao, kushine ata watambua mabepari wanauwezo gani
 
(1)Maisha ya watanzania walio wengi bado mabovu mno
(2)Watanzania wanajihisi kama hawako huru kuwakosoa viongozi wao wanaowachagua.
(3)Serikali ni kama haijali maendeleo ya watu, imewekeza zaidi kwenye vitu
(4)Uhuru/demokrasia ni tatizo
(5)Visasi imekuwa ni tishio.
(6)Viongozi kujiona wana akili nyingi
(7)Majeshi yetu kuonekana wazi kutumika kisiasa.

Punguza kusifia ili uache akili yako kuwa huru.

Sifa zingine wana ccm mnajidhalilisha.
 
Ukiwa ccm lazima akili uiweke pembeni.tatizo wakila wao wakashiba basi wanaona watu wote wameshiba kama wao.
 
Back
Top Bottom