Tanzania kuhamasisha kiswahili iwe lugha ya SADC

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1565690123113.png

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali na kwenye mwaka mmoja ujao Tanzania itafanya jitihada kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC na ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja. Profesa Kabudi amewaeleza waandishi wa habari kuwa, katika mwaka mmoja ujao, SADC pia itaendeleza harakati za kuitaka jumuiya ya kimataifa ishinikize Zimbabwe iondolewe vikwazo vya kiuchumi.

"Zimbabwe imewekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda na tunadhani vikwazo hivyo havina sababu ya kuendelea kwa sababu Zimbabwe imekwishafanya uchaguzi, Rais amechaguliwa na maendeleo wananchi wanaendelea vizuri sasa ni wakati wa vikwazo vya kiuchumi kuondolewa kwa Zimbabwe ili Zimbabwe iendelee" amesema Waziri Kabudi.

Profesa Kabudi anaongoza mawaziri SADC akichukua jukumu hilo kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Namibia Netumbo NandiNdaitwah. “Kwa nchi zetu kubadilisha uchumi wetu ni lazima tuendeleze sekta yetu ya viwanda ili kuongeza nafasi za ajira, na kupunguza umaskini na suala hili lazima lifanywe kwa utengamano.” amesema Waziri Kabudi baada ya kukabidhiwa jukumu hilo. Amesema, kwa sasa biashara baina ya nchi wanachama SADC ni chini ya asilimia 20, hivyo kuna kazi kubwa ya kubadili hali hiyo ili kuongeza biashara ndani ya SADC kwa kutengeneza mazingira wezeshi.
 
Tanzania yenyewe haijawahi kukirasmisha kiswahili kwa vitendo leo anataka SADC ikirasmishe.

Kabudi anapwaya sana arudi jalalani akaendelee na kazi yake ya kudanganya watoto wa watu.
 
View attachment 1180195

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema katika Mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi na Serikali na kwenye mwaka mmoja ujao Tanzania itafanya jitihada kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC na ataifanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja. Profesa Kabudi amewaeleza waandishi wa habari kuwa, katika mwaka mmoja ujao, SADC pia itaendeleza harakati za kuitaka jumuiya ya kimataifa ishinikize Zimbabwe iondolewe vikwazo vya kiuchumi.

"Zimbabwe imewekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda na tunadhani vikwazo hivyo havina sababu ya kuendelea kwa sababu Zimbabwe imekwishafanya uchaguzi, Rais amechaguliwa na maendeleo wananchi wanaendelea vizuri sasa ni wakati wa vikwazo vya kiuchumi kuondolewa kwa Zimbabwe ili Zimbabwe iendelee" amesema Waziri Kabudi.

Profesa Kabudi anaongoza mawaziri SADC akichukua jukumu hilo kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Namibia Netumbo NandiNdaitwah. “Kwa nchi zetu kubadilisha uchumi wetu ni lazima tuendeleze sekta yetu ya viwanda ili kuongeza nafasi za ajira, na kupunguza umaskini na suala hili lazima lifanywe kwa utengamano.” amesema Waziri Kabudi baada ya kukabidhiwa jukumu hilo. Amesema, kwa sasa biashara baina ya nchi wanachama SADC ni chini ya asilimia 20, hivyo kuna kazi kubwa ya kubadili hali hiyo ili kuongeza biashara ndani ya SADC kwa kutengeneza mazingira wezeshi.

Poa lakini tuhamasishe viwanda vya mazao yetu hapo ndipo tutafaidika na watu waanze kulima badala ya kukaa vijiweni na kusubiri kuiba iba tu yaani pamoja na Morogoro kuwa na mashaba watu wanakufa wakiiba mafuta!
 
Wasisahau kutoa offer za uraia kuoa na kuolewa.Kila mwaka idadi fulani tutachangamana haraka mbali ya lugha ya kiswahili.
 
Tunajua kwanini mnataka kiswahili😂😂😂😂😂jiwe ulimi wa kugonga yai Kama wenzake aliumeza😂😂duuuh!!. PhD.....!!!!
 
Sababu iko wazi mkuu nyuma ya pazia lugha gongana lazima uombe poo na mzimbabwe alete kishona,mzambia na mmalawi kote kusini waje na za kwao,Ajabu ilioje lugha unayojifunzia masomo hadi vyuo vikuu imekuwa mwiba kwetu hadi tunapanga mikakati kuikimbia AIBU.
 
Acheni porojo. Wananchi hali ngumu mitaani. Nani atakitaka kiswahili wakati anaona wenye kiswahili ni mafukara?

Kivutio kikubwa cha bidhaa ya lugha ni uchumi. Kama uchumi mbovu hakuna atakayeipenda lugha yako..
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Too ambitious to be true!!
Lakini kabla ya hizi jitihada; hatua zipi zimechukuliwa kuweza uhuru wa habari/kujieleza, demokrasia na haki za binadamu?
Je, wale waliokuwa "disappeared and died" uchunguzi wao umefikia wali?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Poa lakini tuhamasishe viwanda vya mazao yetu hapo ndipo tutafaidika na watu waanze kulima badala ya kukaa vijiweni na kusubiri kuiba iba tu yaani pamoja na Morogoro kuwa na mashaba watu wanakufa wakiiba mafuta!
🤣
 
Ni sahihi kiswahili kiwe "working language" ya SADC ili katika vikao wajumbe kutoka republic of Zamunda wasiojua kiingereza wajidai; vinginevyo kiswahili hakina tija. Mwalimu alisema Kiingereza ndio kiswahili cha dunia sio vice versa!
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Petty issues like this not fair to be presented as national agenda to SADC. Kwani hizo nchi nyingine hazina lugha zao za taifa? Mbona hawazileti kama agenda? Tujihoji kama Taifa.
 
..tangu tukipeleke Kiswahili UN na AU tumepata faida gani?

Ndio maana huyu alikuwa anatwanga hivyo hivyo afanyeje sasa? Taabu ya lugha nipale unapotaka kujiona mahiri kumbe hujui lolote pamoja na kuikalia madarasani zaidi miaka 15 ukiitumia na kufaulu halafu huijui.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom