Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,574
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kuwa na vibali halali. Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka.

Japo vifaranga hivyo havijathibitika kuwa na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source: ITV
 
Taarifa ya Habari ya ITV ya leo imeonesha mfanyabiasha wa Ukonga aliyeingiza vifaranga vyenye thamani ya milioni 40 kutoka Kenya bila kufuata utaratibu.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kulingana na sheria ni kubinafsisha mali na kuteketeza vifaranga wote kwa mujibu wa sheria.

Je, kipi bora kumuita mfanyabiasha ukampiga faini pia akalipia gharama za kuhakiki usalama wa vifaranga(kwa afya ya binadamu) alafu umrudishie vifaranga? Au ukateketeza mtaji au fedha milioni 40?
 
Unyama Unyama Unyama.

Unaanzaje kuchoma kiumbe kisa mambo ya vibali tuu! Tukae kwa kutulia, haya maisha tuu kuna kupanda na kushuka

Mbona lile Gari la Jamaa alokamatwa yeye na Mkewe kwa kesi ya Madawa ya kulevya, Limetaifishwa na kutumiwa na Serikali basi nalo wangelichoma moto kama hiyo ndio fundisho.

Haya mambo ya kuchoma Moto ilihali wananchi wanakufa njaa, wananchi masikini tena hawana hata pakuzugazuga wakajiingizia kipato rasmi ... mimi siliafiki ata 0%

Watunga Sheria Wayatizame upya haya.. Wasiyajue Matumbo yao tu.
 
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Kwa nini magari yanayoingia bila vibali kwa nini hawachomi moto?

Pia walishakamata ngombe toka Kenya walitaifisha na sio kuchoma moto?

Kwa nini vifaranga ndo wachome koto?
 
Back
Top Bottom