Tanzania kuanza Utengenezaji wa Chanjo ya Corona

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,166
Baada ya kuhutubia wafanyabiashara na wawekezaji wa jukwaa la MEDEF nchini Ufaransa, Leo hii historia imeandikwa tena kwa Rais Samia Suluhu kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya Bw.Charles Michael juu ya ushirikiano kati ya Tanzania na EU.

Rais Samia ameeleza adhma ya serikali kujenga miundombinu ya kuzalisha chanjo mbalimbali nchini ikiwemo chanjo ya Covid19, Lengo likiwa kukidhi mahitaji si tu ya Tanzania bali Afrika mashariki na nchi za kusini mwa Afrika (SADC).

Ziara ya Rais Samia mjini Brussels ni matokeo ya wito wa Rais Charles Michael unaothibitisha uhusiano imara kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya. Tangu kuanzishwa uhusiano huu Tanzania imepata msaada wa takribani Trilioni 5.98 kutoka EU.

Mambo mengine yaliyojitokeza katika ziara hii ya Rais Samia barani Ulaya ni pamoja na;

1. Kuhutubia shirikisho la biashara la Ufaransa (MEDEF), MEDEF yenye washirika zaidi ya 750,000 ni vinara wa ushawishi na mipango ya biashara, karata hii inafungua ukurasa mpya kwa Tanzania.

2. Utiaji saini wa mikataba sita ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ufaransa, nchi hii iliyopo magharibi mwa Bara la Ulaya inakadiriwa kuwa na pato ghafi(GDP) ya zaidi ya USD Trilioni 2.6 hivyo mikataba hii itafungua fursa kubwa ya biashara na uwekezaji.

3. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 178 kwaajili ya UJENZI WA MRADI WA MWENDOKASI (BRT) AWAMU YA TANO.

4. Kufanikisha upatikanaji wa fedha kiasi cha takribani Euro milioni 80 kwaajili ya kuimarisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

5. Makubaliano ya Tanzania na Ufaransa kushirikiana katika uchumi wa buluu na usalama wa bahari.

6. Kutembelea na kufanya mazungumzo na waendeshaji wa kituo cha wabunifu na wafanyabiashara wa Startup F facility kilichosheni fursa mbalimbali.

Mwenye macho haambiwi ona. Watanzania tunajionea wenyewe uwezo mkubwa unaoonyeshwa na Rais wetu, shime tumpe ushirikiano aweze kufanya makubwa zaidi.
IMG-20220215-WA0074.jpg


Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom