Tanzania kuanza kuuza umeme Kenya ndani ya miaka miwili

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
  • Mradi huu unakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) utakamilika ndani ya mwaka 2018.
  • Zaidi ya MegaWatt 2,000 kuuzwa nchini Kenya katika mradi utakaogharimu Tshs Billioni 600.
  • Pia kuna mradi mwingine wa zaidi ya Tshs Trillioni 1 utakaouza umeme nchini Zambia na nchi nyingine za SADC.
Naanza kuziona faida za gesi yetu.

==================

Powerlines2.jpg

Tanzania is planning a $300 million energy project that will see it export electricity to Kenya within the next two years. The project is being financed by the African Development Bank (AfDB).

Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) deputy managing director Deckian Mhaiki told The EastAfrican that part of the project will involve a 2,000MW supply line to Kenya, to be in place by 2018.

Mr Mhaiki said that Tanesco is in the final stage of floating a tender for the design and construction of the line to a border town in Kenya.

He added that Kenya had indicated to Tanesco that it needed about 1,000MW through a double traffic line/ an extension of 1,600km-long backbone electricity transmission line running from the Tanzanian town of Iringa to Shinyanga through the towns of Dodoma and Singida.

Mr Mhaiki, however, said that the construction of the 680km line between Iringa and Shinyanga that had been slated for completion in June, has been delayed for another three months.

The line is also meant to provide mining companies in the Lake Victoria area in Tanzania with reliable electricity.

The Tanesco official said a feasibility study on a $500 million worth project to connect the Tanzanian supply line with that of the Zambia has started as part of a project to link East African and the Southern African electricity pools.

Tanzania, which now depends on gas for 60 per cent of its domestic power consumption, is also eyeing markets in drought-prone Southern African countries.

Currently, Tanzania exports only 1MW of power through cross-border connection to Lungalunga town in Kenya, but imports 5MW from both Kenya and Zambia and 9MW from neighbouring Uganda, to the Kagera region in northwestern Tanzania.


Tanzania to export electricity to Kenya
 
TANESCO endeleeni na uwajibikaji huo huo watanzania tuna imani kubwa sana na hii TANESCO ya Mramba Muhongo na Magufuli
 
MK254 Leo kaamka na Kenya kutuuzia umeme sisi

Wewe Tanzania kui uzia Kenya !
Inamaana Tumuelewe nani
 
MK254 Leo kaamka na Kenya kutuuzia umeme sisi

Wewe Tanzania kui uzia Kenya !
Inamaana Tumuelewe nani
Kuna yule jamaa lisema juzi kati kuwa hakuna shirika la Tanzania hata moja lenye ubavu wa kufanya biashara za kimataifa.

Sasa leo tumebisha hodi mlangoni kwao
 
Mnapanga kuuza nje huku kwenu hamjitoshelezi.... Nchi gani inawaza kununua umeme unaokatika zaidi ya unavyotumika
Hapo bwana ndio shida
Yaani Tanesco
Huniboa sana
Wakijisikia kukata umeme nikugusa
Wao umeme ukishinda kutwa nzima bila kukata wanakonda kwa kweli
 
Tanesco endeleeni na uwajibikaji Huo Huo watanzania tuna Imani kubwa sana na hii Tanesco ya Mramba Muhongo na Magufuli
Hapa nchini penyewe umeme kwanza hautoshelezi na sio wa kuaminika ni ahadi na uongo mwingi tu kila siku, ije kuwa miaka miwili na katika nchi mbili jirani?Haya na tuji aminishe katika nguvu za miujiza.
 
Hv tunampango wa kuuza umeme Kenya na vilevile tunampango wa kununu umeme Ethiopia..ah ah ah Tz haishiwi vituko..tunanunua nguzo South Africa na wakenya wananunua nguzo kwetu.....viongozi wetu wamerogwa sio buree...
 
Ninachoweza kusema tujitosheleze kwanza kwa umeme maana Wenyewe unazingua kila mara giza,Kulaza nje na ubovu wetu wa kuharakishia tatizo tutashindwa. tujitambue kwanza
 
p { margin-bottom: 0.1in; line-height: 120%; }

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa sekta ya nishati nchini shirika letu hili la tanesco idara ya uzalishaji linafanya vizuri zaidi kuliko idara zingine zote kwa mfano niliona takwimu za juzi jioni zilizotolewa tanesco inazalisha umeme wa megawat 1540 lakini matumizi au mahitaji ya watanzania ktka gridi ni kwa wakati ule yalikuwa ni 1100mw



Kwahiyo hapo utaona kuna Megawati 440 nzima zimebaki hazina mtumiaji kwa muda ule tena muda ambao ni peak demand time. Kwahiyo kwa hapo tuwapongeze sana tu TANESCO kwa kweli sema waendelee kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji katika sehemu ambazo mahitaji yameongezeka kwa kasi na kupelekea uhaba wa umeme kama Arusha, Moshi na Tanga na Kanda ya Ziwa.

Penye pongezi toa pongezi pabovu kosoa ndugu sio kulaumu tu.
 
Kenya wanajua kulalamika watatusaidia na sisi watanzania kuwapigia kelele katakata ya umeme
 
KAMA WEWE NI MFUATILIAJI MZURI WA SEKTA YA NISHATI NCHINI SHIRIKA LETU HILI LA TANESCO IDARA YA UZALISHAJI LINAFANYA VIZURI ZAIDI KULIKO IDARA ZINGINE ZOTE KWA MFANO NILIONA TAKWIMU ZA JUZI JIONI ZILIZOTOLEWA TANESCO INAZALISHA UMEME WA MEGAWAT 1540 LAKINI MATUMIZI AU MAHITAJI YA WATANZANIA KTKA GRIDI NI KWA WAKATI ULE YALIKUWA NI 1100MW

KWAHIYO HAPO UTAONA KUNA MEGAWATI 440 NZIMA ZIMEBAKI HAZINA MTUMIAJI KWA MUDA ULE TENA MUDA AMBAO NI PEAK DEMAND TIME. KWAHIYO KWA HAPO TUWAPONGEZE SANA TU TANESCO KWA KWELI SEMA WAENDELEE KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI KATIKA SEHEMU AMBAZO MAHITAJI YAMEONGEZEKA KWA KASI NA KUPELEKEA UHABA WA UMEME KAMA ARUSHA MOSHI NA TANGA NA KANDA YA ZIWA.

PENYE PONGEZI TOA PONGEZI PABOVU KOSOA NDUGU SIO KULAUMU TU.
Sina uhakika kama nimekuelewa unacho maanisha...Kwa nini kuna shortage?
 
Sina uhakika kama nimekuelewa unacho maanisha...Kwa nini kuna shortage?
kwanza kiujumla nchi nzima hakuna shortage kuna excess ya 440MW Kwa maana nyingine asilimia 30 nzima ya umeme unaozalishwa unabaki kwa kukosa watumiaji mpaka sasa na ni 70% tu ndio unaotumika kwa mujibu wa takwimu nilizopitia juzi. shortage inatokea pale mifumo ya usafirishaji na usambazaji umeme inapozidiwa uwezo na ongezeko kubwa la gafla la mahitaji ya wateja. mifumo hiyo una uwezo tofauti tofauti wa kusafirisha umeme, kuna yenye ukubwa wa 400kv,220kv na 120kv. kinachotokea kwa mfano njia iliyokuwa inapeleka umeme mji A kutokea Dar es salaam Ilikuwa na uwezo wa 120kv ikibeba karibu robo ya umeme unaoweza kubebwa na hii njia kubwa ya 400kv, sasa matumizi katika huu mji A yameongezeka kwa karibu mara tatu hapo umeme unaofika pale kamwe hautatosha mpaka line hii ipanuliwe ama ijengwe nyingine yenye uwezo mkubwa zaidi wa aidha 400kv au na zaidi mambo ambayo ndi Tanesco inayafanyia kazi sana muda huu naona.

hope angalau tumeelewana hapo mkuu
 
Tangu nikiwa mtoto nasikia tunauza dhahabu williamson diamond mines mwadui. Mpaka na uwanja wa ndege ulibomolewa kuchimba dhahabu. Imetusaidia nini? Eti mrahaba. Kwa umeme mrahaba utasikia ni asilimia moja!
 
KAMA WEWE NI MFUATILIAJI MZURI WA SEKTA YA NISHATI NCHINI SHIRIKA LETU HILI LA TANESCO IDARA YA UZALISHAJI LINAFANYA VIZURI ZAIDI KULIKO IDARA ZINGINE ZOTE KWA MFANO NILIONA TAKWIMU ZA JUZI JIONI ZILIZOTOLEWA TANESCO INAZALISHA UMEME WA MEGAWAT 1540 LAKINI MATUMIZI AU MAHITAJI YA WATANZANIA KTKA GRIDI NI KWA WAKATI ULE YALIKUWA NI 1100MW

KWAHIYO HAPO UTAONA KUNA MEGAWATI 440 NZIMA ZIMEBAKI HAZINA MTUMIAJI KWA MUDA ULE TENA MUDA AMBAO NI PEAK DEMAND TIME. KWAHIYO KWA HAPO TUWAPONGEZE SANA TU TANESCO KWA KWELI SEMA WAENDELEE KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA USAFIRISHAJI NA USAMBAZAJI KATIKA SEHEMU AMBAZO MAHITAJI YAMEONGEZEKA KWA KASI NA KUPELEKEA UHABA WA UMEME KAMA ARUSHA MOSHI NA TANGA NA KANDA YA ZIWA.

PENYE PONGEZI TOA PONGEZI PABOVU KOSOA NDUGU SIO KULAUMU TU.
NITA PONGEZA ITAKAPO FIKIA HATUA YA KUPONGEZA SITA PONGEZA KWA TAKWIMU ZA KWENYE MAKARATASI NA BAHATI NZURI UMEME NI BIDHAA UNAYO IPATA MOJA KWA MOJA NA ISIYO HITAJI SABABU NYINGI NISIZO STAHILI KUZIJUA KAMA NIKI KULIPA IN ADVANCE(LUKU) TAYARI NI MKATABA NI WAJIBU WAKO UNILETEE UMEME SABABU NYINGINE YOYOTE NA TAKWIMU HAINA NAFASI VINGINEVYO INGEKUWA NCHI ZA WENZETU UNA SHTAKI SHIRIKA HAYA MAMBO YETU YA YANI,YANI NA ACTUALLY NDIO YANAYO TU DUMAZA MIAKA YOTE TUNATAKA UMEME UWE STABLE KWA WAKATI WOTE, I WISH KATIKA HIZO TAKWIMU ZAKO UNAJUA NI KIASI GANI KINAPOTEA KWA SAA MOJA YA KUKOSEKANA UMEME DSM,HAPA NINA KUJIBU UMEME ULI KATIKA KWA DAKIKA KUMI HUKU MBEZI BEACH,PENGINE HATU FANANI MIMI SI SIFU TU ILI MRADI,NINA SIFU KWA UBORA WA HUDUMA NA HUDUMA NZURI NA MUDA UKIFIKA NITAFANYA HIVYO WEWE UNATOSHA SANA KUWASIFU KWA SASA.
 
porojo za kila siku hizi. umeme tu majumbani wa kawaida kabisa shida...
 
hii nchi imelogwa si bure sisi wenyewe atujitoshelezi alafu leo muuze nje hiyo ni akili kweli?
 
Back
Top Bottom