Tanzania kuanza kuuza masafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada mwakani

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Tanzania itaanza kuuza masafa ya mawasiliano kwa njia ya mnada kuanzia mwakani.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hayo jana baada ya kumaliza mkutano wake na Mtendaji Mkuu wa Nchi wanachama wa Mawasiliano katika Jumuiya ya Madola, Dk Shola Taylor.

“Kuanzia mwakani mnada wa masafa utaanza, zoezi hilo ni jipya hatuwezi kufanya makosa, nina imani tutapata fedha za kutosha, ” alisema.

Waziri Mbarawa alisema masafa hayo yalipatikana baada ya Tanzania kutoka analojia kwenda digitali ambapo masafa 700- 816 yako wazi.

Alisema baadhi ya nchi barani Afrika zimeanza kuuza masafa kwa njia ya mnada na sasa Tanzania itaanza mwakani na kuongeza kuwa nchi za Ghana na Nigeria zimefanikiwa katika hilo na Tanzania inataka kufanya kitu kutokana na mafanikio hayo.

Alisema watakaonunua masafa watatakiwa kuyatumia, vinginevyo wanaweza kunyang’anywa masafa hayo na kuwa wanataka kujipanga vizuri ili sekta hiyo ipate fedha na anaamini Tanzania itafanikiwa katika hilo.

Alisema pia Jumuiya hiyo imekuwa na mikakati mizuri ya ushirikiano kwenye masuala ya kukabiliana na uhalifu wa kimtandao na jinsi ya kushirikiana.

Alisema nchi nyingi zimeweka mikonga ya taifa na kama serikali watapeleka huduma kwenye hospitali na maeneo mbalimbali ya nchi, pamoja na kutengeneza maudhui, kwani katika nchi hakuna maudhui ya kutosha na kutakuwa na mkakati wa kutosha wa kuweza kutayarisha maudhui kwa njia ya kiswahili ili watu wengi wanaufaike na elimu inayotolewa.

Naye Dk Taylor aliipoongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika sekta ya mawasiliano na kuongeza kuwa nchi za Afrika zimeanza kuuza masafa kwa njia ya mnada na katika hilo anaamini Tanzania itafanikiwa kutokana na kupiga hatua katika nyanja ya mawasiliano.
 
Kama wameyanunua ili kuyauza wasipopata Wateja inakuwaje!?
 
Kama wameyanunua ili kuyauza wasipopata Wateja inakuwaje!?
Masafa ni maliasili ya nchi hayanunuliwi, yapo bure Kama haki ya nchi! Ila watumiaji hugharamia kupata haki ya kuyatumia.
 
Kama wameyanunua ili kuyauza wasipopata Wateja inakuwaje!?
Masafa ni non-tangible resource, ni sawa na kuwaambia wasanii ukitaka kuimba sauti fulani inabidi ulipie, it doesn't mean the government owns your voice, ila kwa sababu wanatumia sauti kupata pesa, inabidi walipe
 
Masafa ni maliasili ya nchi hayanunuliwi, yapo bure Kama haki ya nchi! Ila watumiaji hugharamia kupata haki ya kuyatumia.
Hilo naelewa . Kama mtu amenunua masafa ili kuuza kwa wengine inakuwaje asipopata wa kuwauzia!?
 
Hilo naelewa . Kama mtu amenunua masafa ili kuuza kwa wengine inakuwaje asipopata wa kuwauzia!?
Kununua masafa kama middleman sidhani Kama inaruhusiwa. Unanunua masafa kwa matumizi yako na sidhani Kama reselling inaruhusiwa. Muuzaji au mpiga mnada ni mmoja tu, yaani serikali ambaye ndio mmilki, wakati watumiaji ni wapangaji tu (tenants). Hiyo issue ya mnada ilianzia marekani baada ya kuwa na demand kubwa ya masafa kutokana na kuongezeka sana kwa matumizi katika baadhi ya bandwidth hasa masafa ya juu. Hii inatokana na ukweli kuwa pamoja na masafa kuwa mengi katika mgawanyo wake, ni kiasi kidogo tu ndio hutumika kwa ufanisi kimawasiliano wakati watumiaji wanaongezeka kila siku ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa matumizi mapya. Yaani katika bandwidth moja utakuta ni baadhi tu ndio inakuwa na characteristics nzuri au zisizo na matatizo kwa mawasiliano au matumizi. Hivyo watumiaji wakubwa wa masafa kama radio/television (broadcasters), mobile telephone, satellite, na navigation hukimbilia hayo masafa. Hivyo kukatokea uhaba mkubwa kwani demand ilikuwa kubwa wakati masafa hayaongezeki (finitive). Nia sio mtu anunue ili auze bali anunue kwa kuthamini umuhimu wa masafa katika biashara yake kama kitu adimu-scarce resource. Hivyo ni kutoka kwenye mgawanyo wa kawaida Kama ilivyo sasa, ambapo unaomba na kuwa na haki ya umilki hata Kama hutumii,kwenda kwenye ushindani. Hata hivyo kunaweza kuwa na ulanguzi kama Tcra hawatakuwa na mfumo mzuri wa usimamizi, yaani mpangaji anaweza kumpangisha mtu mwingine kitu ambacho ndio unakizungumzia (kununua ili kuuza).
 
Back
Top Bottom