TANZANIA kuanza kuchimba TUNGSEN na COBALT.

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Kampuni ya Serikali ya Korea inayoitwa Korea Resources Corporation imeishauri Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuanza kuchimba madini ya TUNGSEN (Business Worth USD 600M per annum) pamoja na COBALT.

Hivi karibuni Wizara ilikamilisha uandaaji wa Ripoti ya Aina za madini yaliyopo katika Ardhi ya Tanzania ambapo COBALT na TUNGSEN ni miongoni mwa madini ya thamani yaliyopo nchini, Kampuni mbalimbali za Korea tayari zimeweka nia ya kuanza uchimbaji wa madini hayo nchini, STAMICO imetakiwa kujiandaa kupokea makampuni hayo makubwa kutoka Korea na kufanya nao mazungumzo ya namna ya kushirikiana baina ya Kampuni hizo na STAMICO.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini Imeanzisha kamati maalum ya kuratibu na kusimamia ushirikiano wa nchi mbili hizo, kamati hiyo yenye jina TANZANIA and SOUTH KOREA INTER-MINISTERIAL COMMITTEE ON ENERGY AND MINERALS itahusisha maafisa kutoka wizara inayosimamia nishati na madini ya hapa nchini na ile ya Korea. Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo kamati hiyo imeyazingatia na kuanza nayo ni kuratibu na kudhamini Kampuni hasa za Tanzania kupata mtaji na mikopo kutoka AFRICA Fund for ENERGY.

Mipango hii ya Wizara ya Nishati na Madini inalenga kujenga ustawi kwa makampuni ya wazawa ya Tanzania ili kupata mitaji na mikopo ya kuendesha miradi mbalimbali mikubwa na hivyo kunufaika na maliasili za hapa nchini.

Juhudi hizi za Prof Sospeter Muhongo chini ya Wizara yake ya Nishati na Madini zinabatilisha madai ya uzushi na tuhuma ambazo anashutumiwa kuwa anapingana na sera ya Uzawa na kwamba anapendelea makampuni ya nje katika uwekezaji na kunufaika kutokana na rasilimali za Tanzania.

Profesa Muhongo yuko safarini nchini Algeria kwa mwaliko rasmi kutoka kwa Waziri wa Nishati alioutoa October mwaka huu, katika safari yake hiyo tayari kampuni mbalimbali zimeshaingia makubaliano na kampuni za Tanzania kuja kuwekeza katika usambazaji wa gesi ya matumizi ya ndani, kampuni hizo ni pamoja na NAFTAL. Pia nafasi mbalimbali zimepatikana katika vyuo vya mafuta na gesi nchini Algeria na Serikali inategemea kupeleka wanafunzi nchini Algeria mwanzoni mwakani.
 
Macho yangu Yana hitaji maombi kwakweli maana kila siku nashindwa kusoma neno TANZANIA badala yake nasoma as TANZIA....
 
Wachache ndio watafaidika masikini,sisi wadanganyika,hospital tunalala chini,wakubwa wakiugua wanapelekwa nje kwa kodi ya mvuja jasho,watoto wetu wanakaa chini madarasani,madaktari wanachinjwa wakidai haki zao,wabunge wanalipwa $12,000 na wanadai hazitoshi,weekend njema wadanganyika!
 
Kwanini mara nyingi watu wanakuwa so negative when it comes about the Gov operations..,fanya maomboi haraka maana hali hiyo katika lugha tunaitafsiri kama kukata tamaa, na hakuna kitu kibaya kwa binadamu aliye hai kama kukata tamaa.

Simama fanya maombi nami nitakusaidia.
 
Suala la kufaidika wachache sio sahihi.,kwa maana kutokana na kodi na mrejesho wa miradi hii mikubwa ya uwekezaji nchini, watanzania watatimiza ndoto ya maisha bora ambayo wameendelea kuiota. Ni kwa sababu return ya maliasili hizi ndizo zitasaidia watoto wasikae chini darasani, itatuwezesha kulipa mishahara na stahiki za juu kwa madaktari wetu na kuzalisha wataalamu zaidi pamoja na kuongeza ustawi katika maisha ya watu wetu.
 
watu wanaendelea kukaa chini na migodi ya dhahabu inakauka chini ya hawa wezi ccm sahau
 
kuna topic nyingine ambazo kuzisoma unatakiwa uwe na moyo wa jiwe. Roho inauma sana .
 
dah naona shavu linazidi tu kutuangukia wenye fani wizara husika...

ajira zetu hizo...

sasa wengine mnahoji mtafaidika vipi??mnataka pesa ije mikononi mwenu??, ajira nyingi ni moja ya faida tunazopata sie geologist jaman...
 
wenzenu walipogundua madini hawakuanza kuchimba bali waliandaa wataalamu wao ili wachimbe na baadae kama nchi inufaike norway walifanya hivyo leo hii norway wamefaidika sana gesi sisi tumekimbilia kuchimba dhahabu leo hii migodi inafungwa hakuna tulichofaidika zaidi ya watu wachache kufaidika kila siku tunasikia gesi imegunduliwa lakini hakuna mipango yoyte endelevu nchi kama korea kusini leo hii ina nguvu kiuchumi pamoja na nchi za asia kwa sababu baada ya kugundua hazina rasilimali waliwekeza kwenye elimu kwanini korea kusini watushauri kuchimba hayo madini kikubwa wanataka kupata malighafi za viwanda vyao lakini kama tungesomesha watu wetu tungefungua viwanda kama vya kutengeneza simu,computer ambazo malighafi zake ni hayo madini na sisi tukawa tunauza bidhaa zetu kwa bei nafuu
 
Kwanini mara nyingi watu wanakuwa so negative when it comes about the Gov operations..,fanya maomboi haraka maana hali hiyo katika lugha tunaitafsiri kama kukata tamaa, na hakuna kitu kibaya kwa binadamu aliye hai kama kukata tamaa.

Simama fanya maombi nami nitakusaidia.
kwa sababu wanachimba na kutu achia mashimo.Kwakweli hatupati kitu.Naona wenyewe wakubwa wanatajirika.wewe kwakua gamba huwezi kuona.Maana ukiwa gamba unatakiwa uwe zuzu vinginevyo maisha ya kigamba huta ya weza
 
Kampuni ya Serikali ya Korea inayoitwa Korea Resources Corporation imeishauri Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini kuanza kuchimba madini ya TUNGSEN (Business Worth USD 600M per annum) pamoja na COBALT.

Hivi karibuni Wizara ilikamilisha uandaaji wa Ripoti ya Aina za madini yaliyopo katika Ardhi ya Tanzania ambapo COBALT na TUNGSEN ni miongoni mwa madini ya thamani yaliyopo nchini, Kampuni mbalimbali za Korea tayari zimeweka nia ya kuanza uchimbaji wa madini hayo nchini, STAMICO imetakiwa kujiandaa kupokea makampuni hayo makubwa kutoka Korea na kufanya nao mazungumzo ya namna ya kushirikiana baina ya Kampuni hizo na STAMICO.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini Imeanzisha kamati maalum ya kuratibu na kusimamia ushirikiano wa nchi mbili hizo, kamati hiyo yenye jina TANZANIA and SOUTH KOREA INTER-MINISTERIAL COMMITTEE ON ENERGY AND MINERALS itahusisha maafisa kutoka wizara inayosimamia nishati na madini ya hapa nchini na ile ya Korea. Miongoni mwa mambo ya msingi ambayo kamati hiyo imeyazingatia na kuanza nayo ni kuratibu na kudhamini Kampuni hasa za Tanzania kupata mtaji na mikopo kutoka AFRICA Fund for ENERGY.

Mipango hii ya Wizara ya Nishati na Madini inalenga kujenga ustawi kwa makampuni ya wazawa ya Tanzania ili kupata mitaji na mikopo ya kuendesha miradi mbalimbali mikubwa na hivyo kunufaika na maliasili za hapa nchini.

Juhudi hizi za Prof Sospeter Muhongo chini ya Wizara yake ya Nishati na Madini zinabatilisha madai ya uzushi na tuhuma ambazo anashutumiwa kuwa anapingana na sera ya Uzawa na kwamba anapendelea makampuni ya nje katika uwekezaji na kunufaika kutokana na rasilimali za Tanzania.

Profesa Muhongo yuko safarini nchini Algeria kwa mwaliko rasmi kutoka kwa Waziri wa Nishati alioutoa October mwaka huu, katika safari yake hiyo tayari kampuni mbalimbali zimeshaingia makubaliano na kampuni za Tanzania kuja kuwekeza katika usambazaji wa gesi ya matumizi ya ndani, kampuni hizo ni pamoja na NAFTAL. Pia nafasi mbalimbali zimepatikana katika vyuo vya mafuta na gesi nchini Algeria na Serikali inategemea kupeleka wanafunzi nchini Algeria mwanzoni mwakani.

Multiple utilization of our resources will cost our future generation. The question is the ministry of mineral will be able to monitor/control all these underway projects eg Gas-Lindi/Mtwara, Coal and Iron ore-Ludewa, nickel -Ngara, Uranium-Namtumbo, Tanzanite-Arusha, Gold -Geita/Mara/Kahama, etcccccccccccc
 
Hiyo yote ni kwa manufaa ya wageni na watawala.Chukua mifano ya nchi kama Brazil,China na zile zote zinazojita zimeendele kiuchumi,wanaofaidika ni Wenye nacho!Tembea uone mambo.
 
wenzenu walipogundua madini hawakuanza kuchimba bali waliandaa wataalamu wao ili wachimbe na baadae kama nchi inufaike norway walifanya hivyo leo hii norway wamefaidika sana gesi sisi tumekimbilia kuchimba dhahabu leo hii migodi inafungwa hakuna tulichofaidika zaidi ya watu wachache kufaidika kila siku tunasikia gesi imegunduliwa lakini hakuna mipango yoyte endelevu nchi kama korea kusini leo hii ina nguvu kiuchumi pamoja na nchi za asia kwa sababu baada ya kugundua hazina rasilimali waliwekeza kwenye elimu kwanini korea kusini watushauri kuchimba hayo madini kikubwa wanataka kupata malighafi za viwanda vyao lakini kama tungesomesha watu wetu tungefungua viwanda kama vya kutengeneza simu,computer ambazo malighafi zake ni hayo madini na sisi tukawa tunauza bidhaa zetu kwa bei nafuu
sasa mkuu TZ kuna mtu anaye jisumbua kufikiri?Mtz hapo atawaza apate hela za chapuchapu tu.Liccm ndiyo hilo halina shida na maendeleo.Lakini ukili uliza kushinda uchaguzi linaamuka usingizini na kupanga kuiba kura basi
 
Kama vile tumelaaniwa hivi.Madini yamesha kuwepo miaka yote lakini wana faidi wageni tuna achiwa mashimo
 
Suala la kufaidika wachache sio sahihi.,kwa maana kutokana na kodi na mrejesho wa miradi hii mikubwa ya uwekezaji nchini, watanzania watatimiza ndoto ya maisha bora ambayo wameendelea kuiota. Ni kwa sababu return ya maliasili hizi ndizo zitasaidia watoto wasikae chini darasani, itatuwezesha kulipa mishahara na stahiki za juu kwa madaktari wetu na kuzalisha wataalamu zaidi pamoja na kuongeza ustawi katika maisha ya watu wetu.
Mkuu wewe uko wapi?Kama uko Ulaya basi sawa.Watambiwa wacimbe miaka 12 warudishe gharama zao.Zikisha rudi na madini yameisha .Ndiyo wanavyo fanya kwa madini yote
 
dah naona shavu linazidi tu kutuangukia wenye fani wizara husika...

ajira zetu hizo...

sasa wengine mnahoji mtafaidika vipi??mnataka pesa ije mikononi mwenu??, ajira nyingi ni moja ya faida tunazopata sie geologist jaman...
Wewe ndiyo mjinga Waziri mwenyewe anasema mikataba wanayoingia mibovu.halafu wewe kapuku unabwabwaja hivyo
 
Hiyo yote ni kwa manufaa ya wageni na watawala.Chukua mifano ya nchi kama Brazil,China na zile zote zinazojita zimeendele kiuchumi,wanaofaidika ni Wenye nacho!Tembea uone mambo.
Nikweli mkuu wanafaidika wegeni.Viongozi wanahongwa wasaini mikataba,baadaye tunaachiwa mashimo.Ndiyo yalivyo maccm hayana uchungu wowote
 
Kwanini mara nyingi watu wanakuwa so negative when it comes about the Gov operations..,fanya maomboi haraka maana hali hiyo katika lugha tunaitafsiri kama kukata tamaa, na hakuna kitu kibaya kwa binadamu aliye hai kama kukata tamaa.

Simama fanya maombi nami nitakusaidia.

Maombi bila imani ni makelele tuu afu akiomba ndio atapata mgawo wa hayo madini au atakuwa na hisa Nayo.. au Ndo atafukuzwa maeneo husika ili yeye afanye biashara za juice ama??
 
Back
Top Bottom