Tanzania kuadhiriwa na sera za Donald Trump

client

JF-Expert Member
Dec 13, 2015
661
847
8fad76871adcf0e3f1f42d5eed263b50.jpg

TANZANIA imetajwa kuwa miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zinaweza kuathirika kutokana na kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani.

Hayo yalisemwa juzi Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wahasibu katika nchi za Uingereza na Wales (ICEAW) Kanda ya Kati, Afrika na Asia ya Kusini, Michael Armstrong, wakati akizindua ripoti ya utafiti mpya uliofanyika ili kuangalia sera za kiongozi huyo zinavyoweza kuzisaidia ama kuziathiri nchi za Afrika.

Akizindua ripoti hiyo iliyopewa jina la Economic Insight: Africa Q4 2016, alisema dalili zinaonyesha kuwa hali hiyo itatokana na sera ya upanuaji wa matumizi ya fedha chini ya utawala wa Trump, pamoja na kupunguzwa kwa matumizi ili kukidhi ongezeko la miundombinu nchini Marekani.

“Misaada ni mojawapo ya vitu ambavyo vinaweza kuiathiri Afrika, kutokana na mabadiliko katika sera za Marekani chini ya uongozi wa rais mpya.

“Watunga sera na wafanyabiashara wana hamu kuona mipango ya sera za maendeleo za Rais mteule Trump atakapoingia ofisini,” alisema.

Alisema utafiti huo ulifanywa na ICAEW wakishirikiana na taasisi ya uchumi ya Oxford (Oxford Economics) ili kutoa maelezo ya utendaji wa uchumi wa kanda, hasa nchi za Afrika.

Alizitaja nchi nyingine ambazo zinaweza kukumbana na janga hilo kuwa ni Kenya, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Ivory Coast, Afrika Kusini na Angola.

Kwa mujibu wa Shirika la Kiuchumi, Ushirikiano na Maendeleo (OECD), Marekani ndiyo mfadhili mkuu wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Imekuwa ikitoa Dola bilioni tisa kila mwaka kwa kila kanda.
 
Bull shit!!!!!!! Wanatoa dola bilioni 9 huku wanachota rasilimali za dola bilion 900!!!!! Let them go to hell with their senseless predatory aid!
 
Trump anaweza kuwa sawa kwasera zake na kweli kama Tanzania kwa asilimia themanini mpaka tisini katika sekta ya afya tunategemea msaada kutoka marekani,imagine Tanzania inaenda kuomba msaada wa tirioni marekani wakati kuna mwanasiasa wa kibongo anayo hiyo tena kimagumashi kwenye account huko uswiss
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom