Tanzania kuadhimisha miaka 100 ya Julius Kambarage Nyerere

automata

usisepe urudi uendeleze stori na babu yako

1990 alikua London tayari mwezetu sijui ulikua wapi au ulikua unazuga kwenye kaptura ya dingiyako au lakwanza ...njooo usisepe
Kina...
Hiyo Cairo 1988.

1647888328234.png
 
Kina...
Nyinyi hapa ni wanangu.
Mimi siwezi kuwa babu yenu.

Watoto wenu sasa mimi ndiyo babu yao.

Akiwa mwanamme akija nyumbani mke wangu ananiweka roho juu kwa kumpiga mabusu.
Mara kampa juice, mara kampa ice cream.

Akija mtoto wa kike zamu yangu.
Hizi ndizo mila zetu.
Akija Khalid huna amani shakra huyo niwako rahasana
 
Mzee Mohamed .
.naomba kufahamu kwa nia njema tu.

Kipi kilichokufanya uwe unatembea sehemu zote hizo ulimwenguni na katika sekta ya elimu hasa ?

Nitafurahi ukinijuza juu ya hilo.

Maana nilitoka kibaha hadi Kariakoo kwenye duka la vitabu kwenda kununua kitabu chako cha Maisha na Nyakati ya Abdulwahid Sykes .

Basi kuna Mzee mmoja naye ni muislamu nami mkristo alikipenda kitabu basi nikampa kama zawadi .
 
Unahangaika aisee

Usipokuwa makini utakufa kwa msongo wa mawazo
Huku ukiacha familia yako masikini

Achana na hizi mambo, umri wako ushaenda sasa
Huyu ni mwana mikakati, anatumia nyuma ya pazia kusukuma Agenda na kuuza vitabu vyake.

Utawasikia Uamsho, Sheikh Ponda, Sheikh Ilunga Hussein huwa wanakuwa front lakini anayechora ramani na kusukuma Agenda Ni huyu mzee.

Ukisikia Agenda za kutaka kwenye Dodoso la Sensa kuwe na kipengele cha dini, ujue Hawa ndio Wana mikakati.

Mfano, Wakishajua waislamu wako wangapi. Kama ni pungufu maana yake wataanzisha kampeni ya kuzaliana kea fujo na kuoa wake zaidi ( kumbuka Hawa watu Hawaamini kwenye uzazi wa mpango ).

Wakishakulipa wengi wanaanza kuutumia huo wingi KISIASA. Kulazimisha kila wanachotaka na kuweka madarakani watu wao wote KIDINI na hapo nchi lazima itavurugika.

Ukitaka kujua zaidi Hawa watu wasome, soma mpaka Azimio La Abuja.
 
TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 100 YA MWALIMU NYERERE

WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na wadau imeandaa na kuzindua programu ya Maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kusherehekea urithi wa maisha yake, itakayotumika kama zao jipya la utalii wa utamaduni.

Programu hiyo inayojulikana kama Mwl. Nyerere@100 ni sehemu ya mpango wa miaka 10 wa kuenzi na kusherehekea urithi wa maisha ya Mwalimu Nyerere ambao unalenga kuwashirikisha wadau ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere kitaifa na kimataifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amesema programu hiyo pia kutangaza, kumuenzi Mwalimu Nyerere na umuhimu wa kukusanya, kuendeleza, kuhifadhia na kutangaza rasilimali za urith wa Mwalimu Nyerere kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho ili kukuza na kuendeleza utalii.

" Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Aprili 13 mwaka huu, Butiama mkoani Mara siku ambayo kama angekuwa hai angetimiza miaka 100, lengo likiwa ni kuenzi na kucherehekea mchango maridhawa wa Mwalimu Nyerere katika nyanja mbalimbali kitaifa na kimataifa."

Dkt. Ndumbaro amesema matukio yatakayofanyika wakati wa maadhimisho hayo kuanzia mwezi huu hadi kilele ni mikutano ya wadau, mashindano ya baiskeli, matembezi ya hiyari, ngoma za asili, Mwl Nyerere marathon, usiku wa Mwalimu Nyerere, Kalamu ya Mwalimu itakayohusiana na vitabu alivyoandika , maonesho, kughani mashairi na shindano maalumu ya kutengeneza nemba ya Mwalimu@100.

Akifafanua zaidi kuhusu mpango huo amesema Wizara yenye dhamana ya uhifadhi wa Malikale na matumizi yake ya Kiutalii imedhamiria kushirikisha wadau katika kuhifadhia na kutumia kiuendelevu urithi unaotokana na maisha ya Mwalimu Nyerere.

Amesema endapo Mpango huu utaweza kusimamia ipasavyo na kutekelezwa unategemea kuwezesha kutangaza nchi kwa kazi zikizofanywa chini ya Mwalimu Nyerere na pia viongozi wengine waliokuwa naye bega kwa bega.

Ameongeza kuwa kutakuwa na Makumbusho ya wapigania Uhuru ya kwanza Afrika ambayo itaitangaza Tanzania kwani kuna vioneshwa vya kutosha na urithi wa Mwalimu Nyerere utatambulika, kuhifadhiwa, kusherehekewa na kujulikana kwa watanzania wengi hasa vijana.

"Pia maeneo yenye historia ya Mwalimu Nyerere yatatangazwa, yatahifadhiwa kisheria lakini yatafunguliwa kwa ajili ya utalii na itakuwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi."
Thanks for this.
P
 
Thanks for this.
P
eo April 13, ni siku ya kumbukumbu ya miaka 100 ya kuzaliwa Kwa muasisi wa Taifa Letu, Tanzania.

Najiunga na Watanzania wenzangu kuadhimisha siku hii kwa kutembelea mabandiko mbalimbali ya kujikumbusha kuhusu shujaa huyu na Baba wa Taifa Letu.

Wengine wanakuenzi Kwa mawazo, Kwa kuikubali falsafa yako.

Wengine wanakuenzi Kwa maneno Kwa kuzungumzia Kwa mazuri yako.

Na tuko sisi tunaokuenzi Kwa vitendo Kwa kuitekeleza Dira na Dhima yako ya Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea, hivyo niligombea kuomba kuteuliwa kugombea nafasi fulani bila kutoa hata senti moja, na matokeo yake ni niliambulia patupu.

Pamoja na kutoka kapa Kwa kukuunga mkono Kwa vitendo, bado tutaendelea kukuenzi Kwa mawazo, maneno na vitendo kupitia kwenye kalamu yangu.

Nimalize Kwa swali hili, jee viongozi wetu wa kisiasa, wanamuenzi Mwalimu Nyerere kiukweli ukweli kabisa au wanazuga tuu?.

Happy Birthday Mwalimu Nyerere.
Pascal Mayalla Snr
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom