Tanzania ktk mgogoro: Mwadui wakana kuhusishwa uchunguzi wa Almasi. Wasitisha uzalishaji, wadai wizara inajua kila kitu

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Mgodi wa Almasi wa mwadui umesema haujahusishwa katika hatua zozote za kuipima Almasi yake hapo uwanja wa ndege kama ilivyodaiwa na prof Mruma,badala yake na wao walikuwa wanaona tu ripoti zikitoka katika vyombo vya habari

Wamesema wao huwa hawahusiki kuipima almasi hiyo,bali wapimaji ni maafisa wa wizara ya nishati na Madini(TANSORT)


Mgodi huo umesitisha shughuli zote za uzalishaji katika mgodi huo isipokuwa shughuli za ulinzi maji na umeme

Je serikali hii haina njia za kutatua mgogoro na wawekezaji zaidi ya "kusutana" kila kukicha?

Bwana Mruma,ni kweli hukuwataarifu watu wa mgodi na kuwashirikisha?mbona kwenye TV ulisema uliiwashirikisha? Je umekuwa "hijacked" professionally?

Mgogoro huu utaigharimu Tanzania trilioni ngapi wakati Acacia tu wanadai trilioni 5,samaki na meli trilioni 1.2,bombadia bilioni 89,kampuni kadhaa za umeme zinadai matrilioni,kwa nini ndani ya muda mfupi deni la taifa linalotokana na kesi linakaribia kuzidi trilioni kumi?

Je tuko makini kiasi gani?tunajua kwamba Sera za utaifishaji zilishafutwa na utaifishaji lazima ufate due process za kimahakama,je kale ka drama ka kwenye TV ndio due process ya kutaifisha almasi ya bilioni 14? kwa nini tunataifisha mali za watu ambao wanasema hawakusikilizwa wala kuhusishwa? Kama hawakuhusishwa,nani huyu aliyejipa jukumu la kudanganya watanzania? Anapata faida gani?

IMG-20170910-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom