Tanzania Kosa La Kulawiti, Adhabu Yake Ni Jela miaka 30 na Viboko 24! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Kosa La Kulawiti, Adhabu Yake Ni Jela miaka 30 na Viboko 24!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Jun 10, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tanzania Kosa La Kulawiti, Adhabu Yake Ni Jela miaka 30 na Viboko 24!

  Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 24, Polikalipo Mwisua (35) kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wa umri wa miaka 12.

  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rosaria Mugissa alisema ameridhishwa pasipo shaka ya aina yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kuwa mshitakiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Tamasenga wilayani Sumbawanga, alitenda kosa hilo kinyume cha sheria na hivyo Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela na viboko 24 ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

  Awali Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Elija Matiku alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktaba 10, mwaka jana saa 2:30 usiku. Akadai usiku huo wa tukio kijijini Tamasenga, Polikalipo alimshawishi mtoto huyo ambaye ni jirani yake kuingia nyumbani kwake, na alipofanikiwa, ndipo alipomnajisi.

  Upande wa Mashitaka uliomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kutokana na kuongezeka kwa matukio ya kunajisi kunakofanywa na watu wazima wilayani humo. Hata hivyo wakati hukumu hiyo ikisomwa, juzi mshitakiwa hakuwepo Mahakamani hapo. Kutokana na kosa hilo, Hakimu Mgissa alitoa hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo ili atumikie adhabu hiyo, kuchapwa viboko 12 siku anaingia gerezani na vingine 12 siku anamaliza kifungo chake.  habarileo
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  X-PASTER umenisikitisha sana kufunga kila topic kwenye Jukwaa letu zuri la Dini! Sorry kwa kupost mada ambayo sio relevant hapa lakini ujumbe nafikiri ni sent and delivered!
   
 3. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  kuchapwa viboko 12 siku anaingia jela,hii si against fundamental human rights-so barbaric
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Mkuu nimekutumia PM wewe na wadau wengine na nimekuomba utoe mapendekezo yako kuhusiana na jukwaa la dini na imani. Lakini kwa sababu ambazo unazijuwa wewe, mpaka leo hii umenyamaza kimya, hali ukijuwa kuwa wewe ni mmoja wapo wa wachangiaji wakubwa kwenye lile jukwaa.

  Wengi niliowatumia PM, wameniletea mapendekezo yao, ila wewe na baadhi ya wachache amjapendekeza chochote zaidi ya kupost lawama.
   
 5. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  kwani hujui sheria haina haki?dunia hii ya wanadamu, wangeyafuata Mafundisho ya YESU na kuyaishi, Dunia ingekuwa mahali pazuri kama sardaus. Nikupe mfano mdogo wa fundisho la UPENDO; "Mpende mwenzio kama unavyo jipenda wewe" ukiiishi fundisho hilo hakika hutafanya baya lolote. kutakuwa hakuna ufisadi, ubakaji, ulawiti, kuvaa hijab, nk nk. Sababu tumemvaa YESU!Nawaalika wote Wenye mwili mje kwa YESU muone raha ndani ya YESU.
   
 6. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  unaelewa umepost nini kwa nani?
  nadhani kwako kufikiri kunakuja baada ya kutenda,
  ama hakuji kabisa, vinginevyo ungeidelete pumba hii
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mapendekezo: 1. Usitake watu watoe maoni kwa PM, hiyo itakuwa ni divide n' rule. 2. Fungua hilo jukwaa huku ukiendelea kupokea mapendekezo kwa uwazi ili ijulikane nani kasema nini! 3. Hili Jukwaa usilibinafsishe kwa faida ya imani yako, haitakusaidia lolote, unachohofia ni kipi hasa? Kwani Jukwaa la Dini linakupunguzia imani yako? Na kama ni hivyo achana nalo badala ya kuminya uhuru wa kutoa maoni!
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Si lazima uniPm kama unaona hakuna umuhimu, kuna jukwaa la Complaints, Congrats, Advice, unaweza kulitumia pia kufikisha malalamiko yako, lakini si kubaka kila thread.
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimekupata mkuu X-Paster
   
Loading...