Tanzania kiwanda cha wanasiasa uchwara

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Toka Tanzania ipate uhuru mpaka sasa ni takribani miaka 60 tuna kimbilia robo tatu Karne,tukishuhudia mabadiliko ya kimfumo na siasa zinazo zalisha wanasiasa UCHWARA.

Wanasiasa Giants wenye kuheshimika wameendelea kupoteza dira na mwelekeo wa kisiasa kwa kutokujua lengo na matakwa yao kisiasa nini hasa.

Tumeshuhudia zama za ujima na mifumo ya kina Mangungo wa Msovero zikirudi kwa Kasi na kupoteza malengo ya milinea katika sayansi ya siasa kwa wanasiasa wengi nchini.

Kujipendekeza,uongo,uchimvi na uzandiki vimekuwa ni aina ya siasa mpya ndani ya Karne ya 21 Hali inayopoteza postive Impact kwa wanasiasa waganga njaa wengi kwenye Taifa hili maskini wa ubunifu. Hali hii haina tija kwa Taifa zaidi ya kukuza unafiki na utengano kwa Taifa.

Wanasiasa wengi hawatazami nini kinacho wafanya kuwa wanasiasa, wamesimamia uchumia tumbo na ubinafsi kuliko kulifikiria Taifa na nchi yao.

Robert Kennedy aliyewahi kuwa rais wa Marekani aliwahi kusema usifikirie nini Marekani inakufanyia fikiria wewe umeifanyia nini Marekani pia. Kwa aina hii ya wanasiasa UCHWARA tusitegeme Tanzania kufanyiwa chochote na wao zaidi ya wao kuwa oppoturnist.

Kwa tabia ya wanasiasa hawa watu wa Kilimanjaro huwaita kuwa wana ndomo mbili, huku yuko kule yupo.

Double standard hii inawafanya kushindwa kujua katiba ni nini,kwao katiba ni mihemuko,kwao madaraka ni fursa binafsi kwao Tanzania ni Mali ya watu wachache walio noa tumbo wanakula bila kushiba.

Tukiwajua kwa tabia zao hakika tutakaa mbali kwa kuwa wamekuwa sehemu ya chanzo cha matatizo ya Taifa.

Quran tukufu imetaja sifa za wanafiki kuwa zipo tatu,wakiaminiwa hawaaminiki,wakisema husema uongo na ni wepesi kusahau.

Tanzania ya leo si ya wavimba macho kuwa hawaoni. Ni waoga wakusema lakini ni wepesi wa kulalamika ikiwa wameweza kulalamika ujue wame pave way to action.

Tuendelee kuwapuuza na ukatwaji wenu mikia ila ipo siku time will tell.
 
Ukielewa maana halisi ya siasa ni kujipatia ushawishi na kuungwa mkono (no matter by what means, for the end always justifies the means), KAMWE HATA KIDOGO HUTATAABIKA.

Ndiyo maana wazalendo na wapenda-nchi yao kama akina JPM walisema waziwazi ^MIMI SI MWANASIASA.^ Tukumbuke pia alisema: ^Mtanikumbuka kwa mazuri, na wala si mabaya!^
 
Ukielewa maana halisi ya siasa ni kujipatia ushawishi na kuungwa mkono (no matter by what means, for the end always justifies the means), KAMWE HATA KIDOGO HUTATAABIKA. Ndiyo maana wazalendo na wapenda-nchi yao kama akina JPM walisema waziwazi ^MIMI SI MWANASIASA.^ Tukumbuke pia alisema: ^Mtanikumbuka kwa mazuri, na wala si mabaya!^
Yeye ndiye aliyeasisi ukanjanja huu
 
Hao wakufunzi wa hiko Chuo wapo kwenye vyama gani ili tuwatambue?
Nalog off
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom