Tanzania: Kipi kianze, Elimu bure au matibabu bure?

augustino ameri

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
267
170
Watu wanapoteza maisha kwa kukosa dawa na matibabu lakini pia tuna shule zenye wanafunzi wengi,maabara hakuna wala vitabu na walimu waliochoka kati ya hizi huduma mbil ni mtaj wa kisiasa je kipi kitolewe bure?
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
Mkuu augustino ameri, Elimu bado ni priority...magonjwa mengi hasa huku Afrika(Tropical diseases)na ndiyo yenye kuua sana yanaweza kuepukwa kwa kujikinga...mf.mzuri tembea JF Doctor kule magonjwa mengi ni kutokana na Usafi, Mitindo ya maisha, kupuuzwa, kuendeleza mila n k..dont get me wrong, kuwa napuuza Afya lakini iwapo hata kama matibabu yatakuwa bure na bado elimu(hasa ya kujikinga, kutunza mazingira,n.k) haipo basi hatutakuwa tumefanya jambo lolote, and the Vicious cycle will yet stand.
 
Last edited by a moderator:

augustino ameri

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
267
170
Bw.hipp... Tupo pamoja lakin fahamu kuwa mwanafunzi anaweza kulipa ada kwa awamu tsh 10,000/ kila mhula, lakin ugonjwa hauna taarifa wala kulipa kidogo kidogo.tunaongeza yatima nan atawanunulia sare za shule,na mengineyo.
 
hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
AUGUSTINO, ni kweli mkuu ugonjwa hauna taarifa lakibi magonjwa mengi yanayotupata tunaweza kuyaepuka...mf.Malaria, Kipindupindu, Kichocho, Utapiamlo, magonjwa ya zinaa n.k..utaona kuna shida katika elimu(yaani elimu ni njia ndefu hadi kuja kutoa matunda/matokeo) lakini ni matokeo bora...jiulize wangapi wanakwenda shule kusoma(sio kama mazoea/routine, na wanaelimuka kweli)?..na kisha jiulize kwa mwaka unatumia kiasi gani cha pesa ukiwa ni wewe/wewe na familia yako kwa kugharamia matibabu ya malaria, tumbo, n.k huku unaweza kujikinga...hapo ndipo utagundua nini kianze, mkuu.
 
Last edited by a moderator:

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,028
1,500
Watu wanapoteza maisha kwa kukosa dawa na matibabu lakini pia tuna shule zenye wanafunzi wengi,maabara hakuna wala vitabu na walimu waliochoka kati ya hizi huduma mbil ni mtaj wa kisiasa je kipi kitolewe bure?
Mkuu naona haoa cha muhimu ni kuangalia kwanza kama kuna uwezekano wa kuleta shule zenye maabara nzuri, walimu wazuri mazingira mazuri na kufanya watoto wetu wawe na elimu ya maana. Hata kama zitakuwa za kulipia.

Hata hospitali zinatakiwa kuwa nzuri na zenye matibabu ya maana, hata kama malipo yake yatakuwa mkaubwa.

Lakini tatizo lililopo ni kwamba watu wanazaa ovyo. Utaweza kuona mtu ana watoto wanne lakini hana uwezo wa kumsomesha hata mmoja. Ukiangalia wa pwani wanasema kila mtoto anakuja na bahati yake, lakini matokeo yake utaona hakuna anayesoma, na akiumwa anapelekwa kwa mganga wa kienyeji.

La muhimu ni kuwa na watoto tunaweza kuwamudu, hilo ni la kwanza tukifanya hilo hayo mawili itakuwa rahisi kuyashughulikia.
 
Sunshow

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,130
1,500
Elimu kwanza maana yake ni kwamba elimu ni ufunguo wa maisha bora. Mtu akiwa na maisha bora ataweza kupata hela ya matibabu kwa ajili yake na familia yake sehemu yoyote. Tukibadili mwenendo wa maisha yetu tunaweza kujiepusha na magonjwa mengi bila kutumia gharama kubwa kama wachangiaji wengine walivyosema hapo juu.
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,881
2,000
Nawaza ! kwanini bure? ukisha waza kupata huduma yoyote bure unawaza kuhusu huduma duni.imeandikwa asiye fanyakazi na asile.maana yake ni kwama hufanyikazi hakuna kula wala huduma yoyote.vya bure ni aghali, kwa maana vinakosa kiwango.binafsi sipendi kabisa kusikia kitu cha bure.chochote unacho pata bure kuna mtu kalipia.na ndio maana viongozi wa afrika wanahangaika kupita huko na huko kuomba ili wawape wananchi wao vitu na huduma za bure,ndivyo walivyo wajenga na kuwaahidi wakati wa kampeni.
Tujifunze kutoka kwa wazungu, toka niwe na akili zangu sijawahi kumsikia kiongozi yeyote wa huko anakwenda nje ya nchi yake kwenda kuomba ili arudi kuwapa watu wake huduma fulani bure.kuzaliwa masikini si kosa lakini kufa masikini ni kujitakia.chapa kazi kataa umasikini,kataa vitu na huduma za bure.
 
Mkuu, serikali kuwapatia wananchi wake huduma fulani bure wala siyo tatizo. Kumbuka serikali ni sawa na baba kwenye familia na imepewa mamlaka ya kukusanya mapato na raslimali zote za nchi ziko chini yake, kwa nini isitoe huduma bure? Kwa serikali makini popote duniani lazima iangalie ni jinsi gani inaweza kuwapunguzia ugumu wa maisha wananchi wake kwa kuwapatia baadhi ya huduma bure.
 
Mzee wa fund

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
517
0

Umeanzisha siku yangu vyema.
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,119

niko na wewe mkuu !kwa nini bure?kilema apewe bure na mzuma naye?
Fikra za bure ziondoke kabisa!

Tukijizoesha kulipia huduma hizi ndipo tutakapoweza kuzidai ziwe bora.
Wananchi wahamasishwe kujiunga na NHIF na CHF.

Huwa nashangaa kuona mama mja mzito hanunui hata pair moja ya gloves lakini mama huyohuyo anajiaandaa kwa kununua vitenge vya kongo na pia inaandaliwa sherehe kubwa ya kumpongeza kwa kupata mtoto,tatizo lililopo hapa ni attitude.

Tusitarajie huduma bora kwenye afya wakati tunanga'ngania bure,imagine underfives,wajawazito,magonjwa sugu,wazee,wenye ukimwi wooote hawa ni bure huku kitaalamu hawa ndio asilimia kubwa ya wahudhuriaji wa hospitali.
 
JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
2,881
2,000
Mkuu, serikali kuwapatia wananchi wake huduma fulani bure wala siyo tatizo. Kumbuka serikali ni sawa na baba kwenye familia na imepewa mamlaka ya kukusanya mapato na raslimali zote za nchi ziko chini yake, kwa nini isitoe huduma bure? Kwa serikali makini popote duniani lazima iangalie ni jinsi gani inaweza kuwapunguzia ugumu wa maisha wananchi wake kwa kuwapatia baadhi ya huduma bure.
Huduma za bure ziwe kwa makundi fulani ya watu katika jamii kwa mfano masikini sana na wenye ulemavu wa kuzidi.lakini yeyote mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea lazima ajitegemee kwa kila jambo ili aishi labda kama bado yupo masomoni. serikali ibaki na jukumu la kuhudumia wanajeshi,kujenga miundombinu kama barabara, mabwawa ya umwagiliaji, viwanja vya ndege, bandari, majosho,kugharamia utafiti katika nyanja mbalimbali,kugharamia sensa and the like.huduma nyingi ziwe za kulipia na zibinafsishwe.
Angalia hospitali za serikali zilivyo,shule za serikali zilivyo,public toilets zisizo za kulipia zinasikitisha.kama tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tujenge mfumo unao wafanya watu wafanye kazi ili wajiingizie kipato na walipie huduma mbalimbali wao wenyewe.KUFANYA HIVYO KUNA FAIDA ZAKE,JAMII ITAAMKA KIFIKRA,KIJAMII NA KISIASA.
 
SHIP

Member
Nov 26, 2012
49
0
Ni muhimu zaidi afya kwa kuwa afya ndio uzima wenyewe utasomaje ukiwa mgonjwa?na kubwa elimu haina kikomo,utaitafuta tu.
 
filonos

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
647
225
Bw.hipp... Tupo pamoja lakin fahamu kuwa mwanafunzi anaweza kulipa ada kwa awamu tsh 10,000/ kila mhula, lakin ugonjwa hauna taarifa wala kulipa kidogo kidogo.tunaongeza yatima nan atawanunulia sare za shule,na mengineyo.
kwauzoefu tulio nao kitu chochote kitolewacho Bule hata Thamani hahkina pia hata jinsi yakukipata mtoaji atatoa kwa Style yake kwa wakati wake na kwa matakwa yake hao watoaji napia wewe mpokeaji hauna sauti ya kulalamikia huduma hiyo
 
augustino ameri

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
267
170
Kutoa huduma fulan bure ni mamna ya uwajibikaji wa serikali wa serikal kwa mambo mhimu ili mwananch aweze kutumia kipato chake kwa mambo mengine ya maendeleo,misri,libyabahrein, umeme maji,elimu,bure,vitu ving havina kod,km magari nk.
 
Top Bottom