Tanzania kinara katika udahili wa wanafunzi elimu ya awali barani Afrika

kiwenini

Member
Nov 25, 2018
73
43
Awali 1.jpg

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni.

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali.

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu.

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.
 
Ni mwazo mzuri ila bado tunafanyia mchezo sana suala la elimu katika nchi yetu.
Tuboreshe elimu yetu kuanzia;
1. Mazingira rafiki ya shule.
2. Vyumba bora vya madarasa, Maktaba, Maabara & Vitabu.
3. Walimu bora na wkutosha.
4. Mitaala bora inayoendana na maendeleo ya dunia n.k.

Quality is better than quantity
 
Kinara!? Sasa unakuta mtoto ana miaka miwili ati yupo shule ya awali hiyo ni elimu au uvivu wa kulea?
 
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni kinara katika suala la udahili wa wanafunzi katika elimu ya awali barani Afrika na hivyo kuifanya kupiga kubwa katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu(SDGs).

Mafanikio hayo yanatokana na serikali kutoa elimu bure bila malipo ambao umechangia kuongeza udahili wa watoto wengi kupata fursa ya kupata elimu.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Viti maalum FATUMA TOUFIQ ambaye ni pia champion wa masuala ya SDGs bungeni wakati akitoa mrejesho kwa waandishi wa habari kuhusu mkutano aliohudhuriwa wa ‘High level political forum’ uliofanyika Umoja wa Mataifa(UN) hivi karibuni.

Amesema katika mkutano huo waliwasilisha malengo 6 ya SDGs ambayo kwa ujumla wake Tanzania imefanya vizuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu na kutoa wito kwa serikali.

TOUFIQ ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika linalojishughulisha na wanawake na watoto(Wowap), amesema katika mkutano huo alipelekwa kwa ufadhili kutoka Shirika la Equal Measure 2030 la nchini Marekani linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo hayo ili kuhakikisha kunakuwa kuna usawa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo elimu.

Mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya utoaji taarifa jinsi nchi ilivyofanya katika utekelezaji wa SDGs na Tanzania ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kutoa ripoti yake iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dk.Philipo Mpango.
 
Hivi kampeni za kujenga madarasa na kutengeneza madawati bado zipo?

Kimsingi kiwango cha elimu inayotolewa kwa watoto wa Kitanzania ni duni:

1. Sehemu zingine za nchi watoto bado wanarundikana madarasani. Wapo pia wanaosomea chini ya miti!
2. Baadhi ya wanafunzi waliobahatika kuingia madarasani, madarasa yao ni ya tope na hayakusakafiwa,
3. Vifaa vya kufundishiwa na kujifunzia ama ni duni au havitoshelezi,
4. Walimu hawatoshelezi na maxingira yao ya kszi na ya kuishi ni duni, na
5. Walimu wanakosa hamasa ya kufanya kazi (unmotivated).
 
Tunarudisha literacy rate kipindi cha Nyerere.

Tatizo letu siyo UDAHILI bali UBORA/VIWANGO vya elimu inayotolewa.

Wengine wanafika level ya PhD hawawezi kujieleza kwa ufasaha ktk lugha za Kiswahili na Kiingereza.
 
..tatizo letu siyo UDAHILI bali UBORA/VIWANGO vya elimu inayotolewa.

Wafaransa wanasema, petit a petit l'oiseau fait son nid, yaani kidogo kodogo ndege hujenga kiota.
..wengine wanafika level ya PhD hawawezi kujieleza kwa ufasaha ktk lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Waliosababisha hao wenye PhD leo wasioweza kujieleza visuri kiingereza/kiswahilii sio hao waliomadarakani sasa.
 
..mtihani wa kuandikisha watoto shule tulishafaulu.

..tena kuna maeneo hapa Tz yalikuwa na sifa hizo tangu wakati tukiwa chini ya Mkoloni Muingereza.

..ziko wilaya fulani mbili, sitazitaja, zilipewa lengo la kuandikisha watoto nadhani ilikuwa asilimia 40% wazazi wakaweka juhudi wakaandikisha mpaka asilimia 85%.

..mambo ambayo tulikuwa na uwezo nayo hata kabla ya kupata uhuru siyo ya kujisifia miaka 57+ tangu tuanze kujitawala.

..sasa hivi, tulitakiwa tujizatiti katika kuboresha VIWANGO vya elimu tunayoitoa.

..Tuangalie WAHITIMU wanaotokana na mfumo wetu wa elimu wana viwango gani.
 
Ndiyo maana nikasema, mambo ni ngazi kwa ngazi.

Hapo juzi kati watu walikuwa hata hawajali kiasi cha watoto wanaojiunga shule za awali, Sasa angalau wale masikini wasio na fedha wanahamasishwa.

Hapo nyuma watu waliharibu mitaala ili shule za serikali zife. Walitaka kutengeneza matabaka ili familia zilizokuwa kwenye mfumo ziendelee kuneemeka. Sasa taratibu tutaanza kuongeza viwango lakini hili siyo jambo la mwaka mmoja kwa kuwa ilituchukua miaka zaidi ya 20 kufika hapa tulipo.
 
..tatizo letu tangu wakati wa Mwalimu Nyerere lilikuwa kuruhusu siasa ziingie ktk uendeshaji wa sekta ya elimu.

..walioharibu mitaala ni wanasiasa. Lakini mimi siamini kama walifanya hivyo kwa nia mahsusi ya kuua shule za serekali.

..makosa yaliyotokea yalisababishwa na watu wasio na uelewa wa masuala ya elimu kuwa na sauti zaidi ktk maamuzi yaliyokuwa yakifanyika ktk sekta hiyo.
 
..tatizo letu siyo UDAHILI bali UBORA/VIWANGO vya elimu inayotolewa.

..wengine wanafika level ya PhD hawawezi kujieleza kwa ufasaha ktk lugha za Kiswahili na Kiingereza.
Kula tano mkuu hapo hapo kote tutazunguka lakini tutarudi kwenye point uliyoisema hapo elimu ipi hii yakinafiki ya kujifunza ujinga na kujipendekeza.
 
Back
Top Bottom