Tanzania, Kenya kama mataifa huru ya kongole kwenu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Kenya na Tanzania ni mataifa mawili ambayo ni distinct sovereign states. Jambo la heri kabisa katika mstakabala wa kuishi kwa utengamano na kufahamiana.

Kama taifa kila moja lina haki zote katika nchi yake.

Kwa hakika ni ujinga uliopitiliza kwa uamuzi wowote ndani ya nchi moja kuwa hoja ya majadiliano haswa, yenye kubeza kutokea nchi nyingine. Angalau bora ingekuwa majadiliano yenye kupongeza.

Kila mtu na apambane na hali yake. Yote kheri.

"Kwamba Kenya kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Tanzania likihusisha watu wenye akili zao?

"Kwamba Tanzania kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Kenya likihusisha watu wenye akili zao?

Kwamba wanaoyashadadia maamuzi ya Kenya hapa kwetu hawayajui haya? Thubutu? Tunayo yaona hapa kuhusiana na huu ugonjwa, mwungwana mmoja aliandika:

IMG_20200801_100446_674.jpg

Wanayajua vyema bali hii ni janja ya nyani tu, kujaribu ku deviate attention kutoka kwenye matatizo halisi yaliyopo hapa nyumbani. Yaani:

1. Poor handling ya huu ugonjwa.

2. Hali halisi ya sasa kuelekea October 2020.

Ifahamike kuwa ukakasi uliopo katika mawili hayo, kwa hakika si chamtoto tena.

Kenya hata ikisitisha ndege zote duniani kwenda kwake kwa sababu zozote zile, sisi inatuhusu nini?

Ni vizuri wakafahamu kuwa tunawaona na hatudanganyiki!
 
Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
462
500
Unapoficha ukweli kwa watu wako wa ndani na nje (hasa kwa ugonjwa wa hatari) lazima uogopwe kama ukoma. Kenya wameshtuka. hawana uhakika na kinachoendelea. Kwa nini unapokuwa na matatizo usisemwe. Ukisemwa una-react. lazima watu wajadiri
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Sikuwahi kulisemea hili mahala leo naomba nieleze kidogo tu ya kwamba Kihistoria Wakenya ni Majirani zetu ila Mioyoni mwao Wanatuchukia sana.
Generalization za namna hii hazina tofauti na zilizowahi kuwapo hapa kwetu. Mifano ni mingi:

1. Kabila fulani ni wezi
2. Kabila fulani ni Malaya
3. Kabila fulani ni waongo
4. Nk, nk.

Generalization za namna hii wanaziita cliché.

Walikutana wapi watu milion 40 kutuchukia sisi wote tulio idadi kama hiyo, na kwa nini? Labda kama ni wenda wazimu.

Hata kama ni uwenda wazimu wao basi, sisi unatuhusu nini? Hatuwezi kuwalazimisha au kuwashawishi kutupenda wala hatuna haja hiyo.

Wanafanya yao tunafanya yetu. Suala la ugonjwa huu ni local kwenye nchi husika na watu wake.

"Kwamba Kenya kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Tanzania likihusisha watu wenye akili zao?

Makelele tunayoyasikia ni janja janja tu.

Ila kwa hakika, ya kongole yote yaweendee Kenya na Tanzania wameonyesha ni sovereign states na kwa vitendo.

Kila mtu apambane na hali yake.

Ila ya hapa kwetu hatudanganyiki!
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,734

Huna IQ ya kunielewa na kamwe hutokuja kuwa nayo na tafadhali acha Kunipotezea muda sawa? Nilichokiandika wenye IQ Kukuzidi wamenielewa.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Unapoficha ukweli kwa watu wako wa ndani na nje (hasa kwa ugonjwa wa hatari) lazima uogopwe kama ukoma. Kenya wameshtuka. hawana uhakika na kinachoendelea. Kwa nini unapokuwa na matatizo usisemwe. Ukisemwa una-react. lazima watu wajadiri
Kenya ana haki ya kuwahami raia wake kama anavyoona inafaa.

Kujaribu kujifariji, kuuficha, kuukimbia huu ugonjwa haisaidii. Hakuna asiyeujua ukweli huo. Kilichopo hapa chini kutuhusu sisi ni sahihi:

IMG_20200801_100446_674.jpg

Tuna matatizo ya ndani:

1. Poor handling ya ugonjwa
2. Siasa kuelekea October 2020

Zingine ni jitihada za kuhamisha magoli.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Huna IQ ya kunielewa na kamwe hutokuja kuwa nayo na tafadhali acha Kunipotezea muda sawa? Nilichokiandika wenye IQ Kukuzidi wamenielewa.
IQ yako hupimwa na wengine. Ukiweza kupima ya kwako "nyani ataona kundule."

Nikupotezee muda, nimekuita kwenye huu uzi?

Eti IQ kubwa, huna lolote!
 
babu na mjukuu

JF-Expert Member
Jun 23, 2016
2,588
2,000
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Kenya na Tanzania ni mataifa mawili ambayo ni distinct sovereign states. Jambo la heri kabisa katika mstakabala wa kuishi kwa utengamano na kuafahamiana.

Kama taifa kila moja lina haki zote katika nchi yake.

Kwa hakika ni ujinga uliopitiliza kwa uamuzi wowote ndani ya nchi moja kuwa hoja ya majadiliano haswa, yenye kubeza kutokea nchi nyingine. Angalau bora ingekuwa majadiliano yenye kupongeza.

Kila mtu na apambane na hali yake. Yote kheri.

"Kwamba Kenya kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Tanzania likihusisha watu wenye akili zao?

"Kwamba Tanzania kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Kenya likihusisha watu wenye akili zao?

Kwamba wanaoyashadadia maamuzi ya Kenya hapa kwetu hawayajui haya? Thubutu? Tunayo yaona hapa kuhusiana na huu ugonjwa, mwungwana mmoja aliandika:

View attachment 1523468

Wanayajua vyema bali hii ni janja ya nyani tu, kujaribu ku deviate attention kutoka kwenye matatizo halisi yaliyopo hapa nyumbani. Yaani:

1. Poor handling ya huu ugonjwa.

2. Hali halisi ya sasa kuelekea October 2020.

Ifahamike kuwa ukakasi uliopo katika mawili hayo, kwa hakika si chamtoto tena.

Kenya hata ikisitisha ndege zote duniani kwenda kwake kwa sababu zozote zile, sisi inatuhusu nini?

Ni vizuri wakafahamu kuwa tunawaona na hatudanganyiki!
Utakuwa mkenya wewe
 
LUKAMA

JF-Expert Member
May 28, 2017
539
500
Kenya ana haki ya kuwahami raia wake kama anavyoona inafaa.

Kujaribu kujifariji, kuuficha, kuukimbia huu ugonjwa haisaidii. Hakuna asiyeujua ukweli huo. Kilichopo hapa chini ni sahihi:

View attachment 1523518

Tuna matatizo ya ndani:

1. Poor handling ya ugonjwa
2. Siasa kuelekea October 2020

Zingine ni jitihada za kuhamisha magoli.
Sorry boss kuna mtu yoyote ndugu yako amekufa na corona
Tanzania sisi hakuna ugonjwa au unataka tungeweka lockdown ilitufe njaa, nampongeza magu kama baba wa familia anaye jua kuisimamia familia yake vyema haigi maisha ya jila zake.
Nahisi jilani yako kama anawalisha mahindi ya kuchoma watoto wake asubuhi na wewe unaanza kuwalisha
Kila mtu aisimamie familia yake kama anavyo jua kama unaona magu ajui kuongoza hama nchi nenda kenya
 
Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
2,031

Hakuna aliyemzuia Kenya kufanya atakavyo. Halikadhalika Tanzania ana haki hiyo hiyo. Na wanafanya hivyo kimya kimya.

Tatizo la sisi watazamaji wa hiyo movie
tunajaribu kuweka maneno kwa kufuata hisia zetu.
 
Hauko mbali na ukweli mkuu. Ila tatizo la msingi ni kutaka kulikuza suala lenyewe ili kuyafunika matatizo yetu ya ndani.

Kenya kama Kenya kwa hakika haihitaji ndege yetu kwao kama tusivyohitaji yao kwetu.

Kwa hali kama hiyo jiulize tatizo liko wapi hadi mtu anayejiita mtazamaji apandishe mzuka ki hivyo?

Kupandishwa mashetani huku, hasira, kejeli na matusi haya, ni kweli kuwa kisa Kenya kuzuia ndege zetu tu?

Fumbo wawafumbie wajinga.
 
Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
2,031
2,000
Nimesoma uzi wako vizuri na nimeuelewa vyema.
Ila hayo matatizo uliyoainisha hapo bila maelezo ya kina hayaonekani kama tatizo kwa Tanzania.

Ndio maana nikasema sisi watazamaji tunaweka hisia zetu kwenye haya yanayoendelea baina ya Tz na Ky
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Sorry boss kuna mtu yoyote ndugu yako amekufa na corona
Tanzania sisi hakuna ugonjwa au unataka tungeweka lockdown ilitufe njaa, nampongeza magu kama baba wa familia anaye jua kuisimamia familia yake vyema haigi maisha ya jila zake.
Nahisi jilani yako kama anawalisha mahindi ya kuchoma watoto wake asubuhi na wewe unaanza kuwalisha
Kila mtu aisimamie familia yake kama anavyo jua kama unaona magu ajui kuongoza hama nchi nenda kenya
Kwamba ndugu aliyekufa kwa Corona? Jibu ni "ndiyo" achilia mbali list ya waliokufa kwa Corona iliyowahi kuwapo hapa jamvini na si mara moja:

Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

Msitubeze tulioatharika kwa kuwa tu hayajawakuta nyie.

Wahanga hawa wana ndugu zao na wana jamaa zao wa karibu pia.

Njaa zenu na ubinafsi wenu usio na kuthamini maisha ya watu wala msidhani kuwa tuna maslahi nao.

Kwamba hamjui kuwa ugonjwa upo? Si unafiki tu?

IMG_20200801_100446_674.jpg
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,524
2,000
Nimesoma uzi wako vizuri na nimeuelewa vyema.
Ila hayo matatizo uliyoainisha hapo bila maelezo ya kina hayaonekani kama tatizo kwa Tanzania.

Ndio maana nikasema sisi watazamaji tunaweka hisia zetu kwenye haya yanayoendelea baina ya Tz na Ky

Pana vionjo vya hasira na kupandisha mzuka.

Tanzania kaamua lolote. Au Kenya kaamua lolote.

Tatizo liko wapi tuanze kuitana majina?

Ndiyo maana nikaandika "ya kongole" yaani yote "ya kheri" kwao.

Hata hivyo mimi kama mtanzania nitahoji hapa kwetu nisiyoridhika nayo (ya kwetu). Sitayahojia Kenya.
 
Kamukhm

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
1,496
2,000
Generalization za namna hii hazina tofauti na zilizowahi kuwapo hapa kwetu. Mifano ni mingi:

1. Kabila fulani ni wezi
2. Kabila fulani ni Malaya
3. Kabila fulani ni waongo
4. Nk, nk.

Generalization za namna hii wanaziita cliché.

Walikutana wapi watu milion 40 kutuchukia sisi wote tulio idadi kama hiyo, na kwa nini? Labda kama ni wenda wazimu.

Hata kama ni uwenda wazimu wao basi, sisi unatuhusu nini? Hatuwezi kuwalazimisha au kuwashawishi kutupenda wala hatuna haja hiyo.

Wanafanya yao tunafanya yetu. Suala la ugonjwa huu ni local kwenye nchi husika na watu wake.

"Kwamba Kenya kama nchi ina vigezo vyake vya kuwahami au kutowahami raia wake (au kwa kujifariji tu) dhidi ya ugonjwa mbaya wenye kuambukiza na hata kuuwa." Kwanini hilo liwe subject of any discussion in Tanzania likihusisha watu wenye akili zao?

Makelele tunayoyasikia ni janja janja tu.

Ila kwa hakika, ya kongole yote yaweendee Kenya na Tanzania wameonyesha ni sovereign states na kwa vitendo.

Kila mtu apambane na hali yake.

Ila ya hapa kwetu hatudanganyiki!
Kenya sio mtu mmoja.. Kenya Ni
Taifa...na linapimwa na kuhukumiwa kwa sera na UTENDAJI wake. Mtu akisema wanatuchukia anaweza kumaanisha namna wao Kama Taifa wanahandle issues related to us. Nadhani hapo ndipo chuki ya chini chini, kijicho, husda na wivu wa Kenya huwa dhahir.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom