Tanzania iwe mwangalifu na mikopo ya kinyonyaji. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania iwe mwangalifu na mikopo ya kinyonyaji.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by puza46b, Oct 31, 2012.

 1. p

  puza46b Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Wanajamii naomba kuleta hoja maana hizi mbio za nchi za magharibi kutoa mikopo kwa Tanzania inanitisha. Kufafanua zaidi tukumbuke mwaka 2008 kulipotokea matatizo ya uchumi duniani sababu kuu iliyotajwa ni kutoa mikopo kwa watu wasioweza kulipa na kuhakikisha wanalipa mikopo milele daima.
  Kwanini Tanzania iogope?

  1. Mtoa mkopo nia yake ni kutengeneza faida katika riba.
  Tanzania bado masiki hivyo itakwama ichague lipi kulipa deni au kujenga vitega uchumi hivyo deni litaendela kukua

  2. Mtoa mkopo aka bepari nia yake ni wewe ulipe deni milele kwani faida kupitia riba ni kubwa sana
  Hii mikopo imeongozeka ghafla na ni mikubwa.

  3. Mtoa mkopo anatumia mtaji wa mlipa deni kujijengea utajiri
  Mfano mzuri ni kwamba bank zinatumia saving account money kutoa mikopo kwa watu na hiyo mikopo ina riba kubwa zaidi. Kwa sasa IMF inashauri Tanzania ifungue sovereign fund. Ni wazo zuri lakini kama hiyo hela haitawekezwa kwenye nchi yetu faida itaenda wapi?

  4. Ukiwa unadaiwa dola 1000 na benk tatizo ni lako.. benki ikikudai $ million moja tatizo ni lao
  Tanzania ina malighafi nyingi sana madeni yatatufanya watumwa milele. Tuangalie nchi kama Greece ambavyo world bank na mabenk ya ufaranza na ujerumani yalimweka banker aiongoze nchi. kwa sababu greece inadaiwa zaidi ya asilimia 40 ya pato la taifa. Wananchi wote wamesahaulika na greece imeuzwa.

  Kila siku nayoperuzi website naona habari ikisema nchi hi imetoa hela kiasi hichi kwa Tanzania.. hivi hatuwezi ingia mikataba ya maana tuanze kujilipia gharama zetu wenyewe?

  Mwisho nakumbusha nyerere alichosema ni bora tufe tuwaachie mali watoto wetu. Kwa wasome someni kitabu cha the secrate of the economical hit man .. au kingine maarufu cha dead aid by dambisa moyo.

  akhsanteni na mubarikiwe.
   
Loading...