Tanzania itapata maendeleo makubwa iwapo fedha nyingi zitawekezwa kwenye tafiti na miradi ya uzalishaji na sio kwenye siasa

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,238
16,678
Wakuu!

Tumechelewa Sana kupata maendeleo ya kweli nchini tangu tupate uhuru kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye siasa kuliko miradi ya uzalishaji.

Nchi yetu iliamua kuwa kupiga domo kwenye siasa NDIO kulipe Sana kuliko utafiti wa mbegu Mpya za kilimo na ufugaji pale SUA.

Miradi ya uzalishaji kama kilimo na mifugo na wadau wake sio kitu chenye tija KWA nchi yetu wala fungu lake la pesa ni dogo ukilinganisha na mishahara ya kuwalipa wabunge na mawaziri na wafanyakazi ndani ya vyama vya siasa!

Uchawa,upiga domo kwenye vyombo VYA habari unalipa zaidi kuliko utafiti wa kiprofesa unaohusu uzalishaji na vitengo vyake katika nchi yetu!Mfumo huu tulio ikea toka uhuru umezalisha kundi kubwa Sana la wazalendo wa kwenye maiki kuliko wazalendo wachapakazi na kudumaa kea maendeleo yetu.

KAZI za kitaaluma zinabezwa na wasomi wenyewe na kukimbilia siasa zinazo lipa sana hapa nchini. Kuna haja KWA WENYE nchi na MAMLAKA yao kuja na sera Mpya za uwekezaji kwenye uzalishaji kuwe na tija na malipo makubwa Sana kuliko siasa na kuzifanya siasa kuwa KAZI ya KAWAIDA Sana kiasi KWAMBA watanzania hawatokua na ndoto za kupigania siasa bali ndoto za uzalishaji.

Kama Taifa tumetengeneza vita kubwa ya kusaka madaraka ya kisiasa tena KWA baadhi ya Koo zenye historia ya kisiasa na uongozi kuliko vita vya ushindani vya uzalishaji KWA kuwekeza mapesa meengi kwenye malipo ya kisiasa kuliko uzalishaji na tafiti za kisayansi kuhusu uchumi na maendeleo.

Leo kuna wazee wanawaza kupigana kufa na kupona Ili watoto WAO wawe Wana siasa wakubwa nchini kuliko kuwahimiza wafanye KAZI kubwa ya uzalishaji na tafiti kea KUTUMIA elimu zao!!!Kundi la wanasiasa ni la WACHACHE Sana na hawapaswi kulipwa mamilioni mengi ya pesa kuliko wadau wa uchumi na uzalishaji waliopo kila sehemu ya nchi yetu!

Tupate wapi kijana mzalendo atakaeingia ikulu na kubadili mfumo huu mbovu uliopo!!? Yaani atakaeshusha mishahara ya wanasiasa KWA asilimia 75% Ili fedha zote zielekezwe kwenye miradi ya uzalishaji na wadau wa uzalishaji kuliko Sasa!!?

Ni jambo la kushangaza eti vyama vya siasa vilivyopo nchini kwa zaidi ya miaka 20 havina hata kiwanda cha mafuta ya kula,nguo na n.k Hadi sasa vimebaki kupiga domo tu kuliko kushiriki KAZI za uzalishaji Ili vipate uungwaji mkono WENYE tija kwa wananchi!!!

Nadhani kuna haja WENYE MAMLAKA kufanya jambo kwenye hili!!Ili tupate wazalendo wa kweli na sio Hawa wazalendo wa kwenye maiki!!!
 
Tafiti za hawa maproffesor wetu?
Tafiti tuwaachie NGO tu tena zile ziko funded by Donors ambazo ha itaki upuuzi
 
@ Rais Ajaye you have a very valid argument but the origin of the problem is fundamental to solving this and that is to do away with ancient politics and start fresh horizons. We can't bring reform with the existing platform who for almost six decades have failed to realize the fundamentals of development.
 
Hili haliwezekani kwa sababu Ili maendeleo yapatikane,lazima uwe na sera nzuri,sasa sera zinatungwa na wanasiasa wakiwatumia wataalamu,
Sasa aliyeshika mpini ni mwanasiasa,mbovu wa ccm,Hawa wataalamu watatunga sera Ili kulinda matumbo yao tu,maendeleo yatakuja kwa kubadili mfumo wa kisiasa,toa ccm,weka katiba,weka uchaguzi huru.

Atakaepatikana ataweka mazingira wezeshi Ili wananchi wajiletee maendeleo yao,hakuna maendeleo sasa hv chini ya utawala wa ccm!!,never hata Yesu akirudi,it willnt happen!!

Ili maendeleo yaje,toa ccm Madarakani,weka katiba mpya
 
Hili haliwezekani kwa sababu Ili maendeleo yapatikane,lazima uwe na sera nzuri,sasa sera zinatungwa na wanasiasa wakiwatumia wataalamu,
Sasa aliyeshika mpini ni mwanasiasa,mbovu wa ccm,Hawa wataalamu watatunga sera Ili kulinda matumbo yao tu,maendeleo yatakuja kwa kubadili mfumo wa kisiasa,toa ccm,weka katiba,weka uchaguzi huru.atakaepatikana ataweka mazingira wezeshi Ili wananchi wajiletee maendeleo yao,hakuna maendeleo sasa hv chini ya utawala wa ccm!!,never hata Yesu akirudi,it willnt happen!!
Ili maendeleo yaje,toa ccm Madarakani,weka katiba mpya,
Mkuu
Kweli mabadiliko ya kikatiba na kisheria yanapaswa yawepo!lakini kuna ule mhimili uliojichimbia sana wanauita the state unapaswa kusimamia haya na Dira ya kitaifa!yaani uwe na meno ya kusimamia malengo ya kitaifa BILA kujali CCM, CHADEMA au NCCR imeshika hatamu!!
 
@ Rais Ajaye you have a very valid argument but the origin of the problem is fundamental to solving this and that is to do away with ancient politics and start fresh horizons. We can't bring reform with the existing platform who for almost six decades have failed to realize the fundamentals of development.
Through the new Constitution we can do reform but the constitution should recognise the state as an organ to observe the objectives are fulfilled no matter who is in the throne!!
 
Tuanze kwanza kwa kuindosha CCM madarakani, mambo mengine yatakuwa ni rahisi ku ya set, kutegemea nchi hii kuwa na maendeleo chini ya utawala wa CCM ni kujidanganya na kupoteza muda mchana kweupe
 
Kuna mtu anapaswa kuingia mule Ikulu na kufanya haya nilioyaandika Ili tupate maendeleo ya kweli!!

Bado unaamini kwenye mtu? Kumbuka kuamini kwenye mtu hata mapungufu yake itakuwa sehemu ya hayo matamanio yako, awamu iliyopita ilikuwa ni mfano halisi wa hayo matamanio yako. Wangalau vyama vingekuwa vinabadilishana kukaa madarakani nguvu zingebaki kwa wananchi, lakini hii ccm kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti, usitegemee maendeleo makubwa, bali maendeleo ya kawaida yatakayo halalisha ccm kukaa madarakani bila ridhaa ya umma.
 
Angalau huyo mtu asaidie hiyo KATIBA na mfumoi ikae sawa ILI tuendeleee Naamini mtu ataweza akipata back up ya the state KWA KATIBA hii inahitaji mtu aingie alete hayo!!
 
Kwa katiba hii inayoilinda ccm sitegemei matamanio yako kutokea. Labda yatokee machafuko tuanze upya, ama jeshi lipindue kuwe na kipindi cha mpito kila chama kianze upya, na uwekwe mpango wa maendeleo ambao utakuwa lazima ufuatwe kwa chama chochote kilichopo madarakani, tofauti iwe kwenye aprroach tu. Si zaidi ya hapo.
 
Tatizo nchi hii haina watafiti. Hawa hawa wa majalalani wanaweza kuja na utafiti wa maana kweli?

Wasomi wetu mfano Kabudi, Shivji na Mwakyembe wanayakana machapisho yao kwa sababu ya matumbo yao.
 
Wakuu!

Tumechelewa Sana kupata maendeleo ya kweli nchini tangu tupate uhuru kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye siasa kuliko miradi ya uzalishaji.

Nchi yetu iliamua kuwa kupiga domo kwenye siasa NDIO kulipe Sana kuliko utafiti wa mbegu Mpya za kilimo na ufugaji pale SUA.

Miradi ya uzalishaji kama kilimo na mifugo na wadau wake sio kitu chenye tija KWA nchi yetu wala fungu lake la pesa ni dogo ukilinganisha na mishahara ya kuwalipa wabunge na mawaziri na wafanyakazi ndani ya vyama vya siasa!

Uchawa,upiga domo kwenye vyombo VYA habari unalipa zaidi kuliko utafiti wa kiprofesa unaohusu uzalishaji na vitengo vyake katika nchi yetu!Mfumo huu tulio ikea toka uhuru umezalisha kundi kubwa Sana la wazalendo wa kwenye maiki kuliko wazalendo wachapakazi na kudumaa kea maendeleo yetu.

KAZI za kitaaluma zinabezwa na wasomi wenyewe na kukimbilia siasa zinazo lipa sana hapa nchini. Kuna haja KWA WENYE nchi na MAMLAKA yao kuja na sera Mpya za uwekezaji kwenye uzalishaji kuwe na tija na malipo makubwa Sana kuliko siasa na kuzifanya siasa kuwa KAZI ya KAWAIDA Sana kiasi KWAMBA watanzania hawatokua na ndoto za kupigania siasa bali ndoto za uzalishaji.

Kama Taifa tumetengeneza vita kubwa ya kusaka madaraka ya kisiasa tena KWA baadhi ya Koo zenye historia ya kisiasa na uongozi kuliko vita vya ushindani vya uzalishaji KWA kuwekeza mapesa meengi kwenye malipo ya kisiasa kuliko uzalishaji na tafiti za kisayansi kuhusu uchumi na maendeleo.

Leo kuna wazee wanawaza kupigana kufa na kupona Ili watoto WAO wawe Wana siasa wakubwa nchini kuliko kuwahimiza wafanye KAZI kubwa ya uzalishaji na tafiti kea KUTUMIA elimu zao!!!Kundi la wanasiasa ni la WACHACHE Sana na hawapaswi kulipwa mamilioni mengi ya pesa kuliko wadau wa uchumi na uzalishaji waliopo kila sehemu ya nchi yetu!

Tupate wapi kijana mzalendo atakaeingia ikulu na kubadili mfumo huu mbovu uliopo!!? Yaani atakaeshusha mishahara ya wanasiasa KWA asilimia 75% Ili fedha zote zielekezwe kwenye miradi ya uzalishaji na wadau wa uzalishaji kuliko Sasa!!?

Ni jambo la kushangaza eti vyama vya siasa vilivyopo nchini kwa zaidi ya miaka 20 havina hata kiwanda cha mafuta ya kula,nguo na n.k Hadi sasa vimebaki kupiga domo tu kuliko kushiriki KAZI za uzalishaji Ili vipate uungwaji mkono WENYE tija kwa wananchi!!!

Nadhani kuna haja WENYE MAMLAKA kufanya jambo kwenye hili!!Ili tupate wazalendo wa kweli na sio Hawa wazalendo wa kwenye maiki!!!
Tatizo lako ni kuwa umeelezea hasa kiini cha cha matatizo yetu kama nchi, na unapofanya hivi hawa vilaza waliopora utawala hawatapenda kusikia kitu kama hiki.
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom