Tanzania isitishe uhuiano wake na Syria kupinga mauaji ya raia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania isitishe uhuiano wake na Syria kupinga mauaji ya raia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 13, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Mapema mwaka huu wakati suala la Libya limeanza nilitoa pendekezo la serikali yetu kusitisha uhusiano wake na Libya kwa sababu ya uamuzi wa Gaddafi kutumia silaha kushambulia wananchi wake mwenyewe na hivyo kuinuka dhidi ya watu wake. Nilitoa pendekezo wakati ule kuwa Tanzania kama taifa ambalo kuundwa kwake kulitokana na uelewa wa utu wa binadamu basi tungesitisha uhusiano na Libya mara moja in protest. Of course, haikutokea na tukachagua na tumeendelea kuchagua upande mbaya wa historia. Lakini zaidi nilishangazwa - kama wengine - jinsi serikali yetu ilivyokuwa na haraka ya kukataa 'bendera ya waasi' na hata kurudia kutotambua NTC huko Zanzibar na kuomboleza wazi kuondolewa na hatimaye kifo cha Gaddafi na kuwalaumu wananchi wa Libya.

  Wakati huo huo tumeona kule Syria mambo yakiendelea na Assad akiwashambulia wananchi wake na kuwaua kama mtu anavyotungua ndege mtini. Yote ni kwa sababu wananchi wake wamechoshwa na utawala wake. Bahati mbaya sana kinachofanywa siyo operesheni ya kipolisi tena - kurudisha amani - bali ni operesheni ya kijeshi ambapo watu wengi wameuawa wanaume kwa wanawake, wazee kwa vijana ambao wamejaribu kuandamana kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.

  Arab League taasisi ambayo nayo ni kama AU ya Africa imejikuta ikijaribu kuingilia kati na kumbembeleza Assad kukubali 'road map' na Assad inaonekana hataki kabisa kwani licha ya kukubali bado jeshi lake linaendelea kushambulia wananchi. Hatimaye AL imeamua kuisimamisha Syria kutoka kwenye jumuiya hiyo na bila ya shaka kujaribu kui-isolate Syria.

  Tanzania iko upande gani na kwanini?
  Hadi hivi sasa hatujasikia kauli yoyote ya maana ya kuonesha kutofurahishwa kwetu kama taifa (kupitia serikali yetu) na mauaji ambayo utawala wa Assad unayafanya. Je, Tanzania haijali hilo au tunasubiri wengine waoneshe njia na sisi tufuate? Ni mantiki gani ambayo inatufanya tuendelee kuwa na uhusiano na serikali ambayo imeinuka dhidi ya wananchi wake, kuwaua kama kuku na kukataa kabisa kutafuta suluhisho la kisasa isipokuwa mpaka wananchi wapigishwe magoti kwanza?

  Lakini taarifa za leo kuwa balozi mbalimbali zimeshambuliwa huko Syria kingetufanya hata kumuita balozi wa Syria nchini "for consultation" lakini tulikuwa na haraka ya kumuita aliyepandisha bendera kusherehekea ukombozi wa watu wake badala ya hawa wanauua wananchi wao. Tumekasirishwa na bendera zaidi kuliko utu! Je, ni mpaka nani aseme kuwa kinachoendelea Syria ni kinyume na utu na haki za msingi za binadamu?

  Je yawezekana serikali yetu inashindwa kuchukua msimamo mkali dhidi ya serikali inayoua wananchi wake ya Assad kwa vile sisi wenyewe tayari tumeanza kuwa na serikali ya aina hiyo hiyo na yawezekana huko mbeleni tukaona vikosi vyetu vikishambulia mamia ya wananchi wetu wanaoandamana kama wale wa Syria dhidi ya serikali yao? Yawezekana hiki ndicho kinachotufanya tushindwe kuchukua msimamo. Je kama wale watu zaidi ya 3000 wangeuawa na vikosi vya NATO kule Syria ni kweli tungekaa kimya? Yawezekana kuna imani iliyopotoka kwamba kuuliwa na NATO ni kubaya zaidi kuliko kuuliwa na serikali yako?
   
 2. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Umemaliza yote kwenye red...they do not have such a moral authority....ni wale wale tu na ni bora wakae kimya kuliko wakaongea
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama Syria walikuwa wanatupa 'cheques' kama Ghadafi na kwa sababu hiyo tusitegemee cha maana kutoka serikali yetu. Sana sana kama Membe na wenzake watabwana kuhusu msimamo wa Tanzania na hakika watema "tunashauri pande mbili zinazopingana zikae kwenye meza ya mazungumzo".
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa siku za karibuni sijaona ukiukwaji wa haki za binadamu na udhalilishwaji wa utu wa mtu kama hapo Syria. Naunga mkono kwa wito huu kutekelezwa mara moja!! ... Na Viongozi na vyombo vya usalama vya Tanzania ... Vijifunze somo la msingi tokana na kinachoendela PALE!!
   
 5. B

  Bundajo JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uhusiano wa Syria na Tanzania ni mdogo sana kiasi cha kuanza kutoa kauli juu ya mambo yanayoendelea kule. Mimi binafsi hata sikumbuki kama walishawahi kutupa msaada hata wa kibajaji kimoja, sasa ya nini tuanze kuingilia? Cha muhimu kwa sasa ni kuangalia kama Lowassa ataweza kuchukua nchi 2015 au la. Haya mambo mengine ni ya kuyapotezea tu.
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Je yawezekana serikali yetu inashindwa kuchukua msimamo mkali dhidi ya serikali inayoua wananchi wake ya Assad kwa vile sisi wenyewe tayari tumeanza kuwa na serikali ya aina hiyo hiyo na yawezekana huko mbeleni tukaona vikosi vyetu vikishambulia mamia ya wananchi wetu wanaoandamana kama wale wa Syria dhidi ya serikali yao? Yawezekana hiki ndicho kinachotufanya tushindwe kuchukua msimamo. Je kama wale watu zaidi ya 3000 wangeuawa na vikosi vya NATO kule Syria ni kweli tungekaa kimya? Yawezekana kuna imani iliyopotoka kwamba kuuliwa na NATO ni kubaya zaidi kuliko kuuliwa na serikali yako?

  Mwanakijiji kwanini twende huko kote wkt serikali yetu nayo sasa hivi inafanya kama anavyofanya Rais wa Syria dhidi ya wananchi wake. Hapa, kwetu utamwona Membe akijalamba mdomo-ulimi na kushika shika mikono kama anaigiza vile lkn hakuna cha maana wanachoweza kufanya. Mimi ktk historia ya maisha yangu naamini kwasasa Tanzania ina serikali legelege kuliko nchi nyingi sana ikiwemo Syria.
   
 7. t

  toby ziegler Senior Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  what about uhusiano wetu na USA inaypdetain watu GUANTANAMO BAY without trial?

  what about uhusinao wetu na SAUDI ARABIA ambayo no moja kati ya nchi zinazoongoza na violations of human rights

  what about CHINA?

  What about IRAN?

  What about UK ambayo pia ina violate human rights za raia wake?

  where do we stop?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  inaonekana umemiss kabisa nilichosema au nilichojengea hoja. Siyo suala la 'human rights' in general. Kwani tulivunja uhusiano na Israeli kwa sababu gani? Au hukumbuki tuliwahi kuvunja uhusiano na Uingereza? au Ujerumani Mashariki? Tunaanzia kwenye hili hili la haki za binadamu na hususan serikali kuinua silaha kuwashambulia wananchi wake..
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  red n bolded: Duuuuuuuu, aisee hii kali kwelikweli. watu tunafikiri tofauti sana, wakuu
   
Loading...