Tanzania isitishe kupokea misaada toka Japan; Tuwapatie msaada katika saa yao ya giza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania isitishe kupokea misaada toka Japan; Tuwapatie msaada katika saa yao ya giza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 14, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Salaam!

  Ninapoangalia kina,uzito na uhatari wa kile kinachoendelea huko Japan kufuatia tetemeko kubwa la ardhi ambalo lilifuatiwa na Tsunami ninajikuta napata pendekezo linalohitaji ujasiri wa kiuongozi, maono ya mbali na kujali utu wa mwanadamu kwa kiwango cha pekee kabisa.

  Tanzania imekuwa mpokeaji mkubwa wa misaada kutoka Japan tangu wakati wa Uhuru. Tumepokea kila aina ya misaada na ukiondoa misaada ya kifedha, ufundi na sayansi vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kwenda kusoma huko chini ya mipango ya makubaliano kati ya nchi nzetu mbili. Usishangae kukuta kwa mfano madaktari wetu wengi wa wanyama wamesomea huko na wataalam wetu wa mambo mengine mengi pia wamesomea huko. Ni chini ya mwezi mmoja tu uliopita ambapo serikali ya Japan ilitoa msaada ya karibu shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kusaidia masuala ya chakula kwa nchi yetu. Na ilikuwa mapema mwezi huu ambapo serikali hiyo hiyo ilitoa msaada wa shilingi milioni 462 kwa taasisi kadhaa za elimu nchini. Hata hivyo sitaki kuelezea historia na kina cha misaada kwani mingi inafahamika na inaweza kufahamika kwa mtu kufanya kautafiti kadogo tu.

  Hata hivyo katika saa hii ya giza, ambapo wananchi wa Japan wamepatwa na baa kubwa kuliko yote yaliyowahi kutoka katika historia yao ni wazi kuwa mahitaji yao kama binadamu yanazidi sana uwezo wao wa kiteknolojia. Ni mahitaji ya kuonesha watu wanajali, wanawapenda na wanawashukuru kwa mema mengi ambayo wameyafanya kwa mataifa mengine tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia.

  Ni kwa sababu hiyo, ninaamini serikali yetu iamue kwa dhati kurudisha wema wa watu wa Japan kwa kurudisha misaada hiyo michache ambayo imetolewa na kusitisha mpango wowote wa mikataba na nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo kama kitu kidogo ambacho wananchi wa Tanzania wanaweza kuwasaidia ndugu zao wa Japan wanapoinuka kutoka katika msiba mkubwa wa kihistoria.

  Kwa kufanya hivyo nina uhakika watawala wetu wataweza kubuni njia nyingine za kufidia upungufu wowote utakaojitokeza ikiwemo usimamizi mzuri wa fedha zetu wenyewe, kuchukua mikopo toka taasisi ya ndani na kufanya jitihada ya haraka kurudisha fedha zilizofujwa kifisadi katika sehemu mbalimbali.

  Siyo tu turudishe misaada ambayo Wajapan wameitoa kwetu hasa ile iliyokuwa itekelezwe kuanzia mwaka huu bali pia ile ambayo imetolewa kuanzia mwaka jana! Pendekezo hili ni kali lakini linawezekana. Lakini juu ya hilo napendekeza serikali yetu itoe si chini ya shilingi bilioni 20 kusaidia Japan kama fedha kutoka "Kwa watu wa Tanzania" kuonesha imani yetu kuwa taifa hilo rafiki litaweza kupita salama katika saa hii ya giza ambayo inabakia katika historia ikigubikwa na huzuni isiyo kifani.

  Nakumbuka wakati wa janga la Haiti nilitoa pendekezo kama hili lakini halikufanyika aidha kwa sababu tumejiaminisha katika ubinafsi wetu kuwa sisi "tutapokea tu na hatutoi kamwe" au ni kwa sababu tumedekezwa mno katika mahitaji yetu kiasi kwamba hatuwezi kuona mahitaji mazito ya watu wengine. Ndugu zangu, Taifa lisilotoa halibarikiwi! - kanuni ya utoaji inayohusu binadamu inahusu vile vile mataifa!

  Ninaomba, tufanye kitu ambacho hakitoki katika umaskini wa vitu vyetu au hali zetu kama taifa bali kinatoka katika utajiri wa tunu za wema wetu kama binadamu.

  I know... I'm just fantasizing about greatness of our people.... kama tungekuwa na viongozi wenye uwezo wa kuona ukuu huo.

  Napendekeza.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  We still need their support; Do u know that's Japanese GDP? it is 60 times bigger than Tanzanians it means they will not need to produce anything 4 sixty years 4 us to catch up...
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hao watawala wetu wenye tamaa ya fisi kila kiingiacho kwao haktoshi sembuse kurudi
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tuanze na fly-over ya Magufuli pale Ubungo. Japan waliahidi ku-finance hilo daraja, nadhani pesa tunayotaka kuwalipa Dowans inatosha kufanya hiyo kazi!
   
 5. LD

  LD JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kutoa ni mlango wa kupokea.
  Wakati mwingine tunakuwa maskini, na fedha na dhahabu yetu inaliwa na nondo na Madumadu na Kutu kwa sababu hatutoi.
  Tunapokea tunaweka kwenye mifuko iliyotoboka ambayo ni mafisadi.
  Kutoa ni kanuni ya Kimungu kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

  Naunga mkono hoja yako Mzee!!!
   
 6. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  nanga mkono hoja mzee mmkjj. pia rafiki wa kweli ni yule anae kujali ktk shida na raha pia
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu wazo jema... Hii nchi haina kabisa utaalamu wa majanga, mimi najaribu bufikiri kwa kweli kuwa umuhimu ya al least kupeleka waokoaji wasaidie kwenye kufukua maiti, maana uwezekano wa kupata watu hai kwa sasa ni finyu.

  Kama rais kila kukicha nahaha dunia nzima na kibakuli chake kama matonya, usitegee utashi wa viongozi wetu ufikie huko...

  I second 20bn to them!!! Maana kama tunazo za kulipa Dowans, kwa nini tushindwe kwa wenye shida!!!
   
 8. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  People have to understand this..Utoaji wa misaada na serikali ya Japan ni swala ambalo lipo kwenye bajeti zao sio kwamba leo kwa sababu ya janga hili basi watasitisha misaada. Marekani mbona na kuporomoka kwa uchumi bado waliendelea kutoa misaada?
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sifikiri kama tunatakiwa kuwasaidia hawa Wajapan kwa sababu kila wanachojidai kutupatia kinarudi kwao kwa mgongo wa chupa. Kumbuka jinsi wanavyotuingiza kwenye mkenge kwenye magari mabovu yaliyochakaa? Wanavyotugiriba ati wanatoa fweza za kujenga barabara etc. No to help Japan. Wametuibia kiasi cha kutosha.
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kufikiria kama kurudisha wema ni kutenda kile kile alichokutendea mwenzio.
  Yaani kwasababu japan walitusaidia eg bilioni moja na sisi tuwarudishie hiyo hiyo ili tuoneshe kuwa tumewatendea wema.

  Suala la kusitisha mikataba nafikiri ni suala la japan na tz kuongea kuona kama mikataba iliyobaki haitawaumiza wajapan.
  Tz tunahitaji kuwasaidia japan ndio lakini tusisaidie kwa sifa na kujionesha. Tusaidie kwa kiwango tutachoweza.
  Hata kama ni kidogo unapotoa kwa moyo na mungu pia atatubariki.
  Ni aibu leo tunawasaidia japan bilion 20 halafu kesho unaenda kuwaomba hao hao au nchi nyingine bil 10 kwa ajili ya kufinance project fulani.
  Tujikune tunapopafikia.
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ninapoangalia kina,uzito na uhatari wa kile kinachoendelea huko Japan
  kufuatia tetemeko kubwa la ardhi ambalo lilifuatiwa na Tsunami
  ninajikuta napata pendekezo linalohitaji ujasiri wa kiuongozi, maono
  ya mbali na kujali utu wa mwanadamu kwa kiwango cha pekee kabisa.

  Tanzania imekuwa mpokeaji mkubwa wa misaada kutoka Japan tangu wakati
  wa Uhuru. Tumepokea kila aina ya misaada na ukiondoa misaada ya
  kifedha, ufundi na sayansi vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kwenda
  kusoma huko chini ya mipango ya makubaliano kati ya nchi nzetu mbili.
  Usishangae kukuta kwa mfano madaktari wetu wengi wa wanyama wamesomea
  huko na wataalam wetu wa mambo mengine mengi pia wamesomea huko. Ni
  chini ya mwezi mmoja tu uliopita ambapo serikali ya Japan ilitoa
  msaada ya karibu shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kusaidia masuala ya
  chakula kwa nchi yetu. Na ilikuwa mapema mwezi huu ambapo serikali
  hiyo hiyo ilitoa msaada wa shilingi milioni 462 kwa taasisi kadhaa za
  elimu nchini. Hata hivyo sitaki kuelezea historia na kina cha misaada
  kwani mingi inafahamika na inaweza kufahamika kwa mtu kufanya
  kautafiti kadogo tu.

  Hata hivyo katika saa hii ya giza, ambapo wananchi wa Japan wamepatwa
  na baa kubwa kuliko yote yaliyowahi kutoka katika historia yao ni wazi
  kuwa mahitaji yao kama binadamu yanazidi sana uwezo wao wa
  kiteknolojia. Ni mahitaji ya kuonesha watu wanajali, wanawapenda na
  wanawashukuru kwa mema mengi ambayo wameyafanya kwa mataifa mengine
  tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia.

  Ni kwa sababu hiyo, ninaamini serikali yetu iamue kwa dhati kurudisha
  wema wa watu wa Japan kwa kurudisha misaada hiyo michache ambayo
  imetolewa na kusitisha mpango wowote wa mikataba na nchi hiyo kwa
  miaka mitano ijayo kama kitu kidogo ambacho wananchi wa Tanzania
  wanaweza kuwasaidia ndugu zao wa Japan wanapoinuka kutoka katika msiba
  mkubwa wa kihistoria.

  Kwa kufanya hivyo nina uhakika watawala wetu wataweza kubuni njia
  nyingine za kufidia upungufu wowote utakaojitokeza ikiwemo usimamizi
  mzuri wa fedha zetu wenyewe, kuchukua mikopo toka taasisi ya ndani na
  kufanya jitihada ya haraka kurudisha fedha zilizofujwa kifisadi katika
  sehemu mbalimbali.

  Siyo tu turudishe misaada ambayo Wajapan wameitoa kwetu hasa ile
  iliyokuwa itekelezwe kuanzia mwaka huu bali pia ile ambayo imetolewa
  kuanzia mwaka jana! Pendekezo hili ni kali lakini linawezekana. Lakini
  juu ya hilo napendekeza serikali yetu itoe si chini ya shilingi
  bilioni 20 kusaidia Japan kama fedha kutoka "Kwa watu wa Tanzania"
  kuonesha imani yetu kuwa taifa hilo rafiki litaweza kupita salama
  katika saa hii ya giza ambayo inabakia katika historia ikigubikwa na
  huzuni isiyo kifani.

  Nakumbuka wakati wa janga la Haiti nilitoa pendekezo kama hili lakini
  halikufanyika aidha kwa sababu tumejiaminisha katika ubinafsi wetu
  kuwa sisi "tutapokea tu na hatutoi kamwe" au ni kwa sababu tumedekezwa
  mno katika mahitaji yetu kiasi kwamba hatuwezi kuona mahitaji mazito
  ya watu wengine. Ndugu zangu, Taifa lisilotoa halibarikiwi! - kanuni
  ya utoaji inayohusu binadamu inahusu vile vile mataifa!

  Ninaomba, tufanye kitu ambacho hakitoki katika umaskini wa vitu vyetu
  au hali zetu kama taifa bali kinatoka katika utajiri wa tunu za wema
  wetu kama binadamu.

  I know... I'm just fantasizing about greatness of our people.... kama
  tungekuwa na viongozi wenye uwezo wa kuona ukuu huo.

  Napendekeza.

  Ulanga Ally.
   
 12. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yenyewe ya Tanzania inayoongozwa na Mafisadi? Mafisadi wameiba pesa mpaka hazina haina pesa bado wanataka kuiba nyingine halafu Mwanakijiji unasema fisadi Mkwere alifikirie hilo swala la kurudisha misaada wakati wameshaiingiza kwenye maketi yao ya Ufisadi. Kama angekuwapo Rais ndio Nyerere ndio angeurudisha huo Msaada. Hawa majipapa Mkwere na wenzake uwaambie hivyo kama umewatusi vile
   
 13. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Unaonaje hawa wanaotuibia na kuturudishia? wanakuwa kama benki yetu basi. We have to show them some love.

  unaonaje mafisadi wetu,wanarudishaga wakituibia?! thubutuu...wapi EPA
   
 14. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Rais kikwete anatakiwa kutuma Japan wanajeshi kuisadia nchi hiyo kwa sasa. Hii itaongeza ushirikiano wetu na mapenzi yetu na Japan. Japan na Norway ni nchi kubwa zinazotusaidia na ni wakati wa kurudisha msaada.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Norway hapana unawasingizia.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  subiri Rwanda waanze na nina uhakika watatangulia kutuonesha njia.
   
Loading...