Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,856
7,843
Wadau hivi Bongo ukiachana na Mortuary zilizopo ndani ya hospitali, Mbona hakuna Mortuary ambazo Mtu/Kampuni zinamiliki private? i.e high class/ VIP mortuary?

Mfano kwa wenzetu Kenya, hii fursa watu wameitumia kweli kweli na kuna private mortuaries nyingi tu watu wamezitengeneza, na wengi wanazitumia huduma hizo pale wanapofikwa na janga la msiba kwenye familia zao.

Kwa shida ya upungufu na ubora hafifu wa vyumba vya mortuary kwa hospitali nyingi ninayoiona kwenye hospitali nyingi za bongo, hii inaweza kuwa biashara nzuri tu bongo na ikalipa vizuri tu, kama watu wenye uwezo wakiwekeza huko.

Ni watu hawajaiona hiyo fursa au wabongo hawataweza kuzilipia?

Au taratibu zetu za kisheria haziruhusu? Kama sheria zetu haziruhusu, zifanyiwe marekebisho ziruhusu hilo, ni fursa nzuri sana. Watu watapata pesa na serikali itapata kodi.
 
Inatisha!
Haitishi mkuu. Ni huduma inayohitajika, ukizingatia kuwa hospitali zetu kwa kweli hazikidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa ubora na wingi. Kenya iko regulated vizuri, na inafanya vyema tu.

Cheki hapa chini kwenye link, moja ya kampuni inayotoa huduma ya private mortuary Kenya huko. Very lucrative!

Nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
 
Kwa nchi ambayo asilimia kubwa wananchi hawana bima utapata hasara Hadi ukome.

Asilimia kubwa watu wanakufa wakiwa na madeni Hadi migogoro na hospital inatokea. Bora watu wenye bima malipo utakata juu kwa juu.

Sasa wewe fungua tuje kukulalia.
Hahahahaha!

Hii nayo ni point nzuri mkuu. Ila mtanilaliaje? Kuingiza mwili hadi mtoe pesa, sio bure bure tu.

Mtu anaweza kuanzisha huduma hii aka target middle income eaners maeneo ya mjini kama Dar- Na akaweka huduma na bei ambazo ni za katikati (sio za juu sana). Anaweza kupata mid-income eaners wengi wafanyakazi na wafanyabiashara wa kati ambao watapenda kuhifadhi wapendwa wao kiheshima zaidi.

Au pia anaweza kutarget high income eaners wale matyta wa mjini hapa. The likes wanaotibiwa Aga Khan na zinazofanana na hizo.
Sio kwamba kitu kama hii mtu akajenge Sitimbi
 
nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest
unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
Ni kweli kabisa mkuu. Hii ni viable idea. Wasiwasi wangu mimi ni kama sheria zetu zinaruhusu hili. Nina wasiwasi sana na hilo. Ngoja nitafuatilia seriously kwa wadau wa Wizara ya Afya Tanzania kupata majibu mujarab juu ya hili.
 
Nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
Japokua mkuu kuna gharama zaidi hapo za kuufanyia mwili treatment.... Kwa hiyo kuna costs za kununua madawa yale ya kutreat mwili, na pia kuwa na wataalamu wa kuweza kutreat hiyo miili pia. Maana kuna zaidi ya kuiweka tu miili kwenye friji, ni lazima iwe treated!
 
Unajua bei ya zile jokofu za 4 in one? Si chini ya 50,000,000 kaka
 
Japokua mkuu kuna gharama zaidi hapo za kuufanyia mwili treatment.... Kwa hiyo kuna costs za kununua madawa yale ya kutreat mwili, na pia kuwa na wataalamu wa kuweza kutreat hiyo miili pia. Maana kuna zaidi ya kuiweka tu miili kwenye friji, ni lazima iwe treated!
Dr fursa hiyo, umejaribu omba kibali ukanyimwa? Hatukuzoea kuona Polyclinic hapo kabla ila for now zimejaa tele
 
Hahahahaha!

Hii nayo ni point nzuri mkuu. Ila mtanilaliaje? Kuingiza mwili hadi mtoe pesa, sio bure bure tu.

Mtu anaweza kuanzisha huduma hii aka target middle income eaners maeneo ya mjini kama Dar- Na akaweka huduma na bei ambazo ni za katikati (sio za juu sana). Anaweza kupata mid-income eaners wengi wafanyakazi na wafanyabiashara wa kati ambao watapenda kuhifadhi wapendwa wao kiheshima zaidi.

Au pia anaweza kutarget high income eaners wale matyta wa mjini hapa. The likes wanaotibiwa Aga Khan na zinazofanana na hizo.
Sio kwamba kitu kama hii mtu akajenge Sitimbi

Nasisimka navyosoma hii fursa dah
 
Back
Top Bottom