Tanzania iruhusu watu binafsi kujenga nyumba za kuhifadhia maiti (Mortuary rooms)

Najaribu kukuelewa the angle you are coming from.
Kwa hiyo suala hapa ni maneno yanayotumika na sio huduma husika per se?
Labda nikuulize huduma ni nini ? na kiasi gani cha kuchaji ni sawa 100%, 1000 % au kulingana na demand and supply ?, kama kuna embe moja kijiji kizima basi lazima kuwe na mchujo na kama wote wanalitaka hata likiuzwa kwa gharama ya mahindi lori zima ni sawa..., after all binadamu hawaishi kwa maembe pekee....

Ila kama kijijini una kisima na watu wanahitaji maji je utachaji kiasi gani ? (kiasi ambacho wanaweza kununua au kiasi ambacho itabidi wakupe hati zao za nyumba (kumbuka either wakae na majumba yao kama maiti au wakupe wewe ili waongeze siku moja ya kuishi (nadhani hapo tunakuja kwenye basic needs being a right for each and everyone) na kiumbe yoyote hatakiwi kuhodhi hizo basic needs (kumbuka hapa siongelei mortuary per-se bali kwamba tumehitimu na kuwa mabepari)
Maana kimsingi duniani hapa ili upate faida ni lazima uwe una solve shida fulani! Huwezi kutengeneza hela duniani if you are not offering solution/s to people's problems/needs.
Yap but you can even make profits by inciting problems, you can sell drugs to addicted people, create gambling joints as well as sell weapons to people so they can kill each other...

Kama ujuavyo first world countries wana-profit through marginalization of developing countries, kizazi chetu kinatengeneza toys na vitu vya kupita kwa mtaji wa mazingira ambayo ni urithi wa coming generations..., Well so long as if it makes dollars then it makes sense who cares.....
Mtu anahitaji sukari anywe chai, aweke kwenye uji pale kijijini alipo hakuna duka la sukari hadi kilomita 10 mbele, unachofanya wewe unainunua sukari kwa jumla, unaongeza gharama yako ya usafiri na faida, unamsogezea sukari ndani ya mita 60 toka ilipo nyumba yake. Umesolve shida yake, anakuja kununua sukari kwako unapata faida, unaendelea na biashara na yeye anakunywa chai yake yenye sukari safi kabisa! Hapo uliona
shida ya kutokwepo duka la sukari kijiji husika, wewe ukaigeuza fursa, maisha yanaenda. Sijaona ubaya hapo. Nimetumia mfano wa sukari, ila sukari inaweza ikawa maji, au chochote kile.
Naam Sukari..., akishindwa kutumia sukari basi atumie chumvi au anywe uji bila sukari sidhani kama atakufa..., ila hio ni tofauti na wewe sababu babu yako alirithi shamba robo tatu ya ardhi ya kijiji na umepanda mahindi hivyo kila mwanakijiji lazima aje kwako akuombe ili uchague kama aendelee kuishi au afe kwa njaa....
Kimsingi kama kungekua hamna shida ya kuwa solved, sijui tungetengenezaje pesa.
Kama kungekuwa hakuna shida pesa zingekuwa hazina faida na sio lazima mtu apate shida aumie ili wewe utoe huduma unaweza ukatunga kitabu au ukatunga wimbo / movie mtua akaenjoy hapo unaongeza furaha ambapo sio necessarily kulikuwa na maumivu
Maana tungeweza wote tukabaki tunalalamika kijiji hiki hatuna duka la sukari, lakini, kulalamika kutaleta sukari kijijini hapo?
Na mimi najaribu kukuelewesha hii concept ya kuangalia problem kwa jicho la fursa, si mbaya kila wakati kama unavyoi portray...!
Hapo umebadilisha maneno yangu sijasema kuangalia problem kwa jicho la fursa bali nimesema kuangalia kila Problem (key word hapa ni kila) is not sustainable...
 
Nilishawahi kumshauri mtu nimwandikie business plan ya biashara hii akaogopa ila ni biashara nzuri na kwa sasa inalipa sana kwa siku maiti ya mtu mmoja inalala kwa 30,000/- nje ya huduma nyingine hivyo ukiwa na 4 friji inayoweza kuhifandhi maiti tatu kila moja utahifadhi miili 12 zaidi ya mtu mwenye vyumba 10 vya guest unachofanya ni kutoa fungu la kumi ili ilinde biashara yako.
Very good business..
 
Hii ni fursa kubwa tu, zipo fursa mbili naona if you have money unaweza kufanya.
1. Mortuary
2. Cremation.

Unaweza kudhani wahindi wanaochomana wanakosea lakini it's a very good idea. Ukienda pale makumbusho, costs za kuchoma mwili ni shilingi 2,500,000. Imagine kama unafungua yako kwa 2,000,000 or less, inalipa.
Labda na wewe uwe muhindi mwenzao.. lasivo biashara itakufa
 
haya lete hela sasa wewe uendelee kuwazika wenda zao!
hapo nimetaja chache hii ninayo kwa zaidi ya miaka 8 sasa.
Arusha kuna sehemu niliziona plot za makaburi za wahindi zimepangwa vizuri nafikiri pale wanauza
Niko kuzisaka chief
 
Zitakuwa kama Sheli,Soko likizidi zitajengwa mpaka open space au masokoni.
 
Back
Top Bottom