Tanzania ipo kwenye kipindi cha mpito hivyo kunaweza kuwa na Try & Error

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,584
4,264
Baada ya kufuatilia Historia ya Nchi nyingi (zaidi ya 17) zenye uchumi mkubwa duniani; nimejiridhisha kuwa; Tanzania ipo kwenye kipindi cha mpito na inafanya vizuri ukilingalisha na nchi nyingingine zilivyo pita katika kipindi hiki.

1. Tanzania ipo kwenye kipindi cha mpito ambacho hata hizo Nchi zilizoendelea zimepitia hivyo tuwe makini tusidanganyike tukaendelea kubakia Vibarua.

2. Wanao jifanya wanatupenda wanatuambia tusijime nk kwani tunaumiza wananchi wakati wao walisha jinyima na kuendelea hivyo wana uwezo wa kuishi maisha mazuri. Chukulia mfano wa mtu anaye ishi kwenye nyumba ya Ghorofa anakuambia usijinyime ili ubakie kwenye nyumba ya Nyasi na kuendelea kuwa kibarua wake na wewe kwa ujinga/ mawazo mgando unamkubalia

3. Tuna mambo mengi tunatakiwa kuyaangalia kwa makini, sio kila walio endelea wana nia njema na sisi; Wakiona tunafungua Fursa za Kutukimbiza kwenye maendeleo; Huanza kuweka vikwazo mara uharibifu wa mazingira nk wakati wao wanaharibu mazingira naweza kusema zaidi ya mara 20 zaidi yetu (kwa uchafuzi wa hali ya hewa).

4. Nimefuatilia Nchi nyingi zilizo endelea wao Uzalendo kwanza bila kujali wazo zuri limetolewa na nani; hapa nyumbani tz baadhi ya watu wapo kupinga kila kitu eti kwa kuwa kimetolewana chama cha upinzani au Chama Tawala.

5. Kwa wanao weza kusoma wafuatilie Nchi nyingi zilizo endela zilikuwa na Transition na nyingine ilikuwa very hectic mf China, Korea, Ujerumani nk

6. Tudumishe amani na tutoe Ushikiano kwa serikali kwa kureport watu tunao watilia mashaka; Nchi itakuwa salama na kuendelea kuwa salama. Serikali ni mimi na wewe! Tusikubali kudanganywa na kubadilisha Dhahabu kwa kipande cha chupa eti kwa kuwa mwenye kipande cha chupa ana uwezo!!!

7. Nimelizia na hoja ya Amani/Usalama kwani bila hilo mengine yote hayafanikiwi

Huo ni mtazamo wangu
TUKIAMUA TUNAWEZA!!!
 
kujinyima hatukatai mkuu ila tunajinyima ili tutengeneze kitu gani/,kupata kitu gani chenye manufaa kwa wote?
huku unabana kule unatuhuniwa kununuawatu

Kubenea: CCM ilitenga billion 5 kwa ajili ya ununuzi wa wabunge na madiwani

unajinyima huku kule unajenga kiwanja ambacho bila mipango madhubuti kinaweza kisitumike kama ilivyo kusudiwa.

ushauri. Tuangalie vipaumbele vya taifa kama hao unaosema walijinyima kwa kuangalia kipi kitawavusha siku zijazo.
 
Back
Top Bottom