Tanzania ionyeshe uongozi Burundi

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SASA si siri tena kwamba hali katika nchi jirani ya Burundi imechafuka. Picha mbalimbali na habari tofauti kutoka nchini humo zinaonyesha kwamba kama hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa haraka na mapema, tunaweza kuwa tunachungulia katika maafa mengine makubwa.

Burundi ni jirani zetu sisi Watanzania. Kimsingi, wakati wa ukoloni wa Ujerumani, sisi na Burundi tulikuwa taifa moja. Tunapotazama madhila yanayowakumba jirani zetu hao, tunatazama madhila ya watu ambao pengine tuna undugu nao wa damu.


Ndiyo maana, Raia Mwema tunaamini kwamba Tanzania ina kila sababu ya kuchukua uongozi katika suala la utatuzi wa mgogoro huo. Kuna sababu mbalimbali za kufanya hivyo na tunaweza kuzitaja chache.


Kwanza, ni ukweli kwamba hata huu utulivu uliotamalaki katika nchi hiyo kwa miaka takribani kumi iliyopita ulisababishwa kwa sehemu kubwa na juhudi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, katika kutafuta chanzo na utatuzi wa kudumu wa uliokuwa mgogoro ndani ya nchi hiyo.


Amani Burundi ilipatikana baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Arusha ambao utekelezaji wake ndiyo angalau umefanya hata matukio yanayoendelea sasa kutokuwa makubwa zaidi ? ingawa hatari ya kuwa makubwa zaidi ingalipo.


Pili ni ukweli kwamba hata vinara wa matatizo ya sasa, kwa mfano Rais Pierre Nkurunziza, ni watu ambao wameishi hapa nchini kama wakimbizi wa kisiasa na wanaharakati. Tunaamini kwamba wapo watu hapa Tanzania ambao wanaweza kuwaambia jambo wahusika hawa na wakasikilizwa.


Kwa hapa mgogoro ulipofika, Tanzania haiwezi tena kuachia nchi nyingine kusuluhisha huu mgogoro. Sisi si Kenya wala Uganda na pia hatufanani na Rwanda. Sisi ni Tanzania ambayo siku zote imesimama juu ya majirani zake kwenye kulinda utu wa Mwafrika.


Ndiyo maana, tuliwakomboa Waganda kwenye makucha ya Iddi Amini, tuliwakomboa Msumbiji kwenye makucha ya Wareno, tuliisimamia Shelisheli kwenye wakati ilipokuwa imelegea na tulileta utulivu Comorro peke yetu hata kama wenzetu waliona hakuna haja ya kuingilia.


Ni wazi kuwa katika wakati huu wa madhila na shaka, Warundi wanatazama nje ya mipaka yao na kutazamia kuwa Tanzania itaona kinachoendelea na kuchukua hatua sahihi na madhubuti. Hatutashangaa kusikia kwamba hata majirani zetu wengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanasubiri suluhisho la Burundi litoke kwetu. Serikali yetu isisahau jambo moja; kwamba sisi ni TANZANIA !


Raia Mwema
 
SISI NI TANZANIA

SISI NI TUNU

SISI NI MWENGE......UMULIKAO......
(wabaadhirifu hawautaki mwenge kwani unawamulika)
 
Tanzania inapaswa kushughulikia kwanza masuala yanayoihusu kwa kumaliza mgogoro wa Zanzibar kabla ya kwenda kutoa kibanzi cha Burundi.

vilevile sikubaliana na kauli kuwa nchi nyingine za EAC zinaisubiri Tanzania ndio imalize mgogoro wa sasa wa Burundi. Rwanda inalalamikiwa kwa kutoa hifadhi kwa waasi wa Burindi waliojificha kwenye kambi za wakimbizi nchini Rwnada na kufanya mazoezi ya kijeshi kabla ya kuvamia Burundi. Vile vile Kagame naye anatuhumiwa kwa kuwaunga mkono wapinzania wa Nkurunzinza.

jambo lamsingi ni kuwa EAC haikuundwa kwenye msingi wa wenye nchi, bali kwa msingi wa viongozi wa nchi hizo ambao leo kwao hakuna hata mmoja mwenye moral authority ya kumwambvia Nkurunzinza mbele ya uso wake kuwa unachofanya sio sahihi!

Vinginevyo Tanzaia ingekuwa na viongozi imara ingeweza kunufaika na ujio wa wakimbizi hao kutoka burundi lakini ninachotegemea ni kuongezeka tena kwa vitendo vya uhalifu na kuongezwa kwa idadi ya askari kaskakazini magharibi mwa nchi. Mkapa aliwahi kuja na wazo kuwa yanayopotea machafuko nchi jirani zitume jeshi kwenda kulinda eneo maalum ndani ya nchi yenye machafuko ambako wakimbizi watakuwa wakiishi badala ya kwenda nchi nyingine.
 
Back
Top Bottom